Magonjwa ya ndani ya mwili

MAUMIVU YA MGONGO:Sababu,dalili,matibabu,kuzuia

Maelezo ya jumla

Maumivu ya mgongo ni tatizo kuumwa mgongo linalowapata watu wengi sana. Katika kipindi chote cha maisha ya mwanandamu ,watu 8 kati ya 10 huathiriwa na tatizo hili. Maumivu yanaweza kuwa ya kawaida,mengine yanaweza kuwa ya kawaida lakini yanayodumu kwa muda mrefu au yanaweza kuwa maumivu makali ya ghafla.

kuumwa mgongoNini dalili za maumivu ya mgongo?

Ni muhimu kuelewa kwamba maumivu ya mgongo si ugonjwa, ni dalili ya kuwepo ugonjwa/tatizo fulani mwilini. Maumivu yanaweza kuwepo yenyewe, au pamoja na dalili nyingine. Maumivu yanaweza kuwa ya ghafla/ya muda mfupi  au maumivu ya muda mrefu/Sugu.
Maumivu unayopata ghafla baada ya kuanguka kutoka kwenye ngazi, au baada ya kuanguka uwanjani ukicheza mpira, au baada ya kunyanyua kitu kizito sana ndio maumivu ya muda mfupi. Maumivu ya ghafla hutokea haraka na mara nyingi hupoa baada ya muda mfupi pia. Maumivu ya muda mfupi hayapaswi kuzidi zaidi ya wiki 6. Maumivu ya mgongo ya muda mfupi ndio maumivu yanayowapta watu wengi zaidi.
Maumivu ya muda mrefu/sugu, kwa upande mwingine, yanaweza kuanza ghafla au polepole na kisha kudumu kwa muda mrefu. Kwa ujumla, maumivu haya hudumu kwa zaidi ya miezi 3. Maumivu ya mgongo ya muda mrefu huwapata watu wachache ukilinganisha na maumivu ya muda mfupi.

Ni nini husababisha maumivu ya mgongo?

Matatizo ya kitabibu yanayoweza kusababisha maumivu mgongoni ni pamoja na yafuatayo:

  • Matatizo yanayosababisha kupungua kwa mjongeo wa mgongo: Tatizo linalowapata watu wengi ni la kusagika kwa gegedu linalotenganisha pingili za uti wa mgongo (intervertebral disk degeneration),hili ni tatizo la uzeeni. Kadri umri unapoongezeka gegedu linalotenganisha pingili za uti wa mgongo husagika na kusababisha maumivu. Tatizo lingine ni kukaza kwa misuli na kupasuka kwa gegedu linalotenganisha pingili za uti wa mgongo (ruptured disk) .
  • Majeraha: Majeraha kama vile kuteguka au kuvunjika mgongo yanaweza kusababisha maumivu ya muda mfupi au maumivu sugu ya muda mrefu. Kuteguka ni kuchanika kwa Kano (ligaments) zinazoutegemeza mgongo, kuchanika huko kunaweza kutokea baada ya kupinda sana mgongo au baada ya kubeba vibaya mzigo mzito. Kuvunjika/kupasuka kwa pingili za uti wa mgongo mara nyingi ni matokeo ya osteoporosis (ugonjwa huu husababisha kudhoofika kwa mifupa). Kwa mara chache maumivu ya mgongo yanaweza kusababishwa na majeraha mabaya yanayotokana na ajali.
  • Magonjwa au hali zinazoweza kuchangia kuwepo kwa maumivu ya mgongo, Ni pamoja na:
    • Uti wa mgongo uliopinda (Scoliosis), kupinda kwa mgongo mara nyingi hakusababishi maumivu ,lakini ,mgonjwa anapofikia umri wa kati huanza kuhisi maumivu.
    • Spondylolisthesis – ni hali inayotokea baada ya pingili moja ya uti wa mgongo kuteleza juu ya nyingine na kutoka mahala pake.
    • Aina mbalimbali za yabisi kavu (arthritis), ikiwa ni pamoja na:
      • Osteoarthritis (yabisi inayosababishwa na kusagika viungio kwenye maungo)
      • Rheumatoid arthritis (Yabisi baridi)
      • Spinal stenosis– safu ya uti wa mgongo huwa nyembamba na kuubana uti wa mgongo na mishipa ya fahamu.
    • Mawe kwenye figo au magonjwa/maambukizi kwenye figo
    • Endometriosis- tishu za mji wa mimba (uterini) zinapopatikana katika sehemu nyingine ya mwili.
    • Osteoporosis – huu ni ugonjwa wa kudhoofika kwa mifupa. Ugonjwa huu wenyewe hausababishi maumivu, lakini unaweza kusababisha kupasuka kwa urahisi pingili za uti wa mgongo na kusababisha maumivu. Mara nyingi ujauzito husababisha maumivu ya mgongo pia.
    • Maambukizi na uvimbe: japo ni kwa nadra, maambukizi na uvimbe kwenye uti wa mgongo husababisha maumivu. Maambukizi husababisha maumivu ya mgongo kwa kushambulia pingili za uti wa mgongo (osteomyelitis), au gegedu za uti wa mgongo (diskitis). Kwa mara chache sana uvimbe unaweza kutokea kwenye uti wa mgongo na kusababisha maumivu ya mgongo.
    • Kihisia: Japo sababu nyingi za maumivu ya mgongo ni za kimwili, msongo wa mawazo pia unaweza kusababisha maumivu makali ya mgongo. Msongo unaweza kuathiri mwili kwa njia nyingi sana. Msongo unaweza kusababisha misuli ya mgongo kukaza sana na kusababisha maumivu makali.

Nani yuko kwenye hatari zaidi ya kupata maumivu ya mgongo?

Japo mtu yeyote anaweza kuwa na maumivu mgongo, mambo kadhaa yanaongeza  hatari ya kupata maumivu.

  • Umri: Tukio la kwanza la kuumwa mgongo mara nyingi hutokea kati ya umri wa miaka 30 na 40. Maumivu ya mgongo huwapata watu zaidi kadri umri unapoongezeka.
  • Uwezo wa kimazoezi: Mara nyingi maumivu mgongoni huwapata zaidi watu wasiofanya mazoezi mara kwa mara. Misuli ya mgongo isiyofanyishwa mazoezi hulegea na inaweza kushindwa kuutegemeza uti wa mgongo. Watu wanaofanya mazoezi magumu sana baada ya kukaa bila kufanya mazoezi kwa kitambo, huongeza uwezekano wa kuumwa mgongo. Kwa mf: watu wanaofanya mazoezi weekend baada ya kukaa wiki nzima bila mazoezi wako kwenye hatari zaidi ya kuumwa mgongo kuliko watu wanaofanya mazoezi kila siku. Tafiti zinaonesha kuwa mazoezi mepesi yanaimarisha gegedu za uti wa mgongo na mifupa inayounda uti wa mgongo.
  • Mlo: Kula mlo wenye kiwango kikubwa cha kalori na mafuta , pamoja na kutofanya mazoezi kunaongeza uwezekano wa kupata kitambi. Kitambi huuongezea mzigo uti wa mgongo.
  • Kurithi: Baadhi ya sababu za maumivu ya mgongo ni za kurithi. Ankylosing spondylitis ni aina ya yabisi kavu inayoathiri uti wa mgongo,aina hii ya yabisi husababisha uti wa mgongo kugangamara na kupunguza mjogeo. Tatizo hili huongeza uwezekano wa kuumia mgongo.
  • Asili: Asili ya mtu pia inaweza kuchangia katika kuwepo kwa matatizo ya mgongo. Kwa mfano : Wanawake weusi hupata spondylolithesis mara mbili mpaka tatu zaidi ya wanawake wa kizungu . Spondlolithesis ni hali ambayo husababishwa na kuteleza kwa pingili ya sehemu ya chini ya uti wa mgongo na kutoka nje ya mahala pake.
  • Kuwepo kwa magonjwa mengine: Magonjwa mengi yanaweza kusababisha au kuchangia kutokea kwa maumivu mgongoni. Magonjwa haya ni pamoja na yabisi kavu,yabisi baridi, yabisi inayosababishwa na kusagika kwa mifupa na saratani iliyotapakaa mpaka kwenye uti wa mgongo.
  • Kazi: Kuwa na kazi ambayo inakuhitaji kuinua vitu vizito, kusukuma, au kuvuta, hasa kama kazi hiyo inakulazimu kukunja sana mgongo, inaweza kusababisha kuumia mgongo na maumivu. Kazi inayokulazimu kukaa sana pia inaweza kusababisha maumivu ya mgongo,hasa kama haukai katika mkao au kiti kizuri.
  • Uvutaji wa sigara : Ingawa kuvuta sigara hakuwezi kusababisha maumivu moja kwa moja, lakini huongeza hatari ya kupata maumivu ya mgongo. Kwa mfano kuvuta sigara kunaweza kusababisha maumivu kwa kuziba mishipa unaopeleka chakula kwenye diski/gegedu la mgongo. Kukohoa sana kwa sababu ya uvutaji wa sigara uliopindukia husababisha maumivu. Kwa mara nyingi watu wanovuta sigara hawafanyi mazoezi ya kutosha, hii huongeza uwezekano wa kuumwa mgongo. Kuvuta sigara pia huongeza hatari ya kudhoofika kwa mifupa ya mwili (oesteoporosis),hali hii huongeza uwezekano wa kuvunjika uti wa mgongo. Zaidi ya hayo, kuvuta sigara kunapunguza uwezo wa kupona majeraha na kusababisha maumivu ya muda mrefu mtu anapofanyiwa upasuaji au kuvunjika mifupa

Ukiwa na maumivu ya mgongo ni wakati gani utafute matibabu ya haraka?

Katika hali nyingi, si lazima kuonana na daktari kwa sababu ya maumivu mgongo, hii ni kwa sababu mara nyingi maumivu hupoa yenyewe bila matibabu yoyote. Hata hivyo kumwona daktari ni wazo zuri kama unahisi ganzi au mchonyoto(tingling), kama maumivu ni makali na hayapoi kwa dawa za kupunguza maumivu, au kama una maumivu makali baada ya kuanguka au kuumia.
Ni bora kumwona daktari wako akupatie tiba, lakini akigundua kuwa tatizo lako ni kubwa zaidi atakupeleka kwa daktari bingwa akuangalie pia.
Ni muhimu pia kumwona daktari wako ikiwa una maumivu ya mgongo na mojawapo ya dalili zifuatzo: Kupata shida kukojoa, udhaifu,maumivu au ganzi kwenye miguu, homa, au kupungua kwa uzito. Dalili hizo zinaweza kuashiria tatizo kubwa zaidi linalohitaji matibabu mapema.

Utambuzi ukiwa na tatizo la maumivu ya mgongo

Ili kugundua sababu ya maumivu ya mgongo, historia ya matabibu na uchunguzi wa mwili unahitajika. Wakati wa uchunguzi wa mwili ,daktari anaweza:

  • Kukuchunguza ukiwa umesimama au ukitembea.
  • Kuchunguza matendohiari (reflexes) ili kuangalia kama yameongezeka au yamepungua, moja wapo ya hayo inaweza kuashiria matatizo kwenye neva.
  • Kuchunguza uwezo/ nguvu za misuli na hisia.
  • Kuangalia kama kuna ishara za kuharibika kwa mizizi ya neva.

Mara nyingi daktari anaweza kupata sababu ya maumivu yako kwa uchunguzi wa mwili na historia pekee. Hata hivyo wakati mwingine kulingana na historia na matokeo ya uchunguzi wa mwili, daktari wako anaweza kuagiza vipimo kadhaa ili kusaidia kupata sababu. Vipimo hivi vinaweza kujumuisha:

  • X-rays
  • MRI scan
  • CT scan
  • Vipimo vya damu

Uchaguzi wa matibabu kama una tatizo la kuumwa mgongo

Matibabuhutegemea unapata maumivu ya aina gani: maumivu ya muda mfupi/papo hapo au muda mrefu/sugu.
Maumivu ya muda mfupi mara nyingi hupoa yenyewe bila matibabu yoyote, lakini unaweza kujaribu kutumia dawa kama Acetaminophen/paracetamol, asprini au ibuprofen kujaribu kutuliza maumivu. Ushauri bora zaidi ni kuwa ,uendelee na shughuli zako kama kawaida na maumivu yako yatapoa tu baadae. Usilale sana,kuamka na kutembeatembea husaidia kupunguza kukakamaa kwa misuli ya mgongo na maumivu . Katika hali ya kawaida, mazoezi na upasuaji hayapendekezwi kwa mgonjwa mwenye maumivu ya muda mfupi.
Matibabu ya maumivu sugu ya mgongo yamegawanywa katika makundi mawili: Yanayohitaji upasuaji  au yasiyohitaji upasuaji. Mara nyingi maumivu ya mgongo hayahitaji upasuaji. Madaktari daima watajaribu kutumia njia nyingine za matibabu kabla ya kupendekeza upasuaji. Kwa mara chache upasuaji huhitajika mapema ili kuzuia matatizo zaidi mf: Maumivu yaliyosababishwa na uvimbe, maambukizo au tatizo kwenye mzizi wa neva linaloitwa Cauda equina syndrome.
Ifuatayo ni orodha ya baadhi ya matibabu ambayo hutumika kutibu maumivu sugu ya mgongo:

  • Kukanda kwa kitambaa cha moto au baridi,au kwa wakati mwingine vyote viwili, hupunguza maumivu na kukakamaa kwa misuli ya mgongo.
  • Mazoezi na kujinyoosha: Japo mazoezi kwa kawaida hayapendekezwi kwa mtu mwenye maumivu ya muda mfupi, mazoezi yanaweza kupunguza maumivu sugu ya mgongo na hata kupunguza uwezekano wa maumivu hayo kujirudia.
  • Madawa: Madawa mbalimbali yanaweza kupunguza maumivu ya mgongo. Aina za dawa zinazotumiwa ni pamoja na:
      • Dawa za kupunguza maumivu
        • NSAIDs
      • Dawa za kulegeza misuli (muscle relaxants) na dawa za kupunguza sonona (antidepressants) zinaweza kutumika pia.
  • Kuvuta mgongo (Traction) : kuvuta mgongo kwa kutumia mfumo wa roda (pulleys) na uzito ili kuunyoosha. Kuuvuta mgongo huwa na lengo la kuachanisha pingili za uti wa mgongo ili gegedu lilioteleza na kutoka mahala pake, lirudi mahala pake.
  • Wakati mwingine mgonjwa anaweza kupewa vifaa vya kuutegemeza mgongo, kwa mfano; mkanda wa kuvaa kiunoni unaoutegemeza mwili (Corsets na braces)
  • Sindano: Kama dawa za kumeza na kupaka hazisaidii, madaktari wanaweza kupendekeza sindano ili kupunguza maumivu.
  • Tiba mbadala: Maumivu sugu ya mgongo yanaposhindwa kuthibitiwa na tiba ya kawaida,watu wengi huanza kutumia tiba mbadala ili kupata nafuu. Japo njia hizi haziwezi kutibu tatizo linalosababisha maumivu, huwasaidia baadhi ya watu. Tiba mbadala ni pamoja na:
  • Acupuncture
  • Kuchua (massages)
  • Tiba ya upasuaji: Kwa ujumla upasuaji huwa pendekezo la mwisho kabisa baada ya njia za kawaida kushindwa. Hii ni kwa sababu upasuaji mara nyingi matokeo yake si ya uhakika. Japo unaweza kuondoa maumivu kabisa katika hali fulani ,unaweza pia kuongeza maumivu kwa watu wengine au kuyapunguza kwa kiasi kidogo tu.

Baadhi ya hali zinazoweza kuhitaji upasuaji ni pamoja na:

  • Herniated disk – gegedu/disk iliyo katikati ya pingiliza uti wa mgongo inapokandamizwa na kutokeza nje
  • Spinal stenosis –uti wa mgongo unapobanwa na kukandamizwa baada ya safu za mgongo kusinyaa na kuwa nyembamba.
  • Spondylolisthesis – upasuaji hufanyika ili kurudisha pingili ya uti wa mgongo iliyoteleza mahala pake.
  • Kupasuka kwa pingili za uti wa mgongo

maumivu ya mgongoNini cha kutarajia ukiwa na maumivu ya mgongo ?

Matarajio ni mazuri sana kwa maumivu ya mgongo ya muda mfupi. Mara nyingi maumivu hupoa bila matibabu yoyote. Maumivu ya muda mrefu, kwa upande mwingine, yanaweza kuanza kwa ghafla au polepole na kudumu kwa muda mrefu. Matarajio yake hutegemea ugonjwa uliyoyasababisha na kama kuna tiba ya ugonjwa huo.

Matatizo yanayoweza kutokea ukiwa na maumivu ya mgongo

Kwa kuwa maumivu ni dalili ya ugonjwa fulani, matatizo yanayoweza kutokea hutegemea ugonjwa/jeraha lililosababisha maumivu. Kila upasuaji huwa na athari mbaya zinazoweza kujitokeza. Kama daktari wako anapendekeza upasuaji ,jadiliana nae kuhusu athari nzuri na mbaya kabla ya upasuaji.

Vyanzo

    • 5 months ago (Edit)

    Ahsanteni sana kwa maelezo yenu MUNGU awabariki maana mnaandika mpaka dawa dahh mko vyema sana

    • 5 months ago (Edit)

    Congratulations maelezo makin Sana🙏

    • 5 months ago (Edit)

    Asanteni kwa elimu nzuri sana. Je maumivu ya mgongo ni hatari kiasi gani? Yanaweza kusababisha kifo?

    • 6 months ago (Edit)

    Naukubali Sana elimu mnayoitoa kwakweli inasaidia mnooh keep it up🤝🤝

      • 5 months ago (Edit)

      Habari, naomba msaada. Tatizo langu limejitokeza hiv karibuni la kupata maumivu makali sana ya mgongo hasa kuanzia muda wa saa 10 alfajiri kiasi kwamba hata kunyanyuka kitandani ni tabu tupu, maumivu huendelea hadi saa 4 asubuhi na kupungua.

        • 5 months ago

        pole sana, inategemea umefanya kazi gani, kama ni maumivu makali yaliyotea kwa ghafla, hii hutokana na shughuli ngumu au mshtuko wa mgongo aina hii ya maumivu yanapungua baada ya kupumzika kwa muda wa wiki 1-3. pole sana. tumia dawa ya maumivu itapunguza karaha. kama ni maumivu makali sana mwone daktari afanye vipimo kama eksirei

      • 6 months ago

      Karibu sana, endelea kuwa nasi

    • 6 months ago (Edit)

    Mimi nina maumivu ya mgongo tangu nilivokuwa na umri wa Miaka 10 ilianza polepole sana ilikuwa ikiuma na kuacha, hali hiyo iliendelea lkn kila ikiuma unakuta imeambatana na ugonjwa mwingine kwa sababu nikienda kupima naambiwa nina Typhoid, mda mwingne UTI. Lakini hali hiyo imekuwa endelevu mpk sasa nina Miaka 24 ila ni mgongo tu sasa unasumbua hayo magonjwa mengine nikipima hamna.

    • 6 months ago (Edit)

    Mbarikiwe kwa elimu nzuri.Hivi kwa mwanamke mwenye tatizo la maumivu ya mgongo Kuna usalama katika kubeba ujauzito na mtoto akazaliwa mzima?

      • 6 months ago

      Inategemea ni tatizo gani, kama una wasiwasi kuhusu hili, onana na daktari wa magonjwa yanwanawake au daktari yoyote

      Atakufanyia uchunguzi wa mwili na kisha kukupatia ushauri unaofaa zaidi, itakusaidia kufanya maamuzi pia

    • 7 months ago (Edit)

    Mimi pia Nina maumivu yamgongo nmefanya x Ray nmeambiwa misuli imekaza hembu nishaurini dawa itakayonisaidia

    • 7 months ago (Edit)

    Nina tatizo LA kukaza kwa misuli ya chini ya uti wa mgongo tiba take ni nini?

    • 7 months ago (Edit)

    mimi nilibend nikiwa nimebeba kitu kizito mabaad ya siku chache kukatoka kama pingili za mgongo zimepinda na nikaanza kuhisimaumivu kiukweli sijatumia dawa yeyote ila maumivu huwa
    yanapungu an kuiludia tena naomba ushauri

    • 8 months ago (Edit)

    Nina maumivu ya mgongo yanayojitokeza kwa muda flani na kupoa , nikifanya mazoezi maumivu yanatoka naomba msaada nina wiki tatu sasa.

      • 8 months ago

      Pole sana, kwa watu wengi hasa vijana walio na umri kati ya 23 na 35 wanapata maumivu ya mgongo kwa sababu ya shughuli wanazofanya na mkao. mara nyingi maumivu haya huyasikia zaidi wanapokuwa wamejilaza wametulia. lakini wakiwa wanafanya kazia au kufanya mazoezi huwa yanapoa. aina hii ya maumivu huwa inaisha tu yenyewe baada ya muda kama kazi au mkao uliosababisha utarekebishwa. angalia mkao au kazi unayofanya kama inaweza kuchangia na kisha rekebisha. kama sivyo mwone daktari. wakati ukisubiiri yaish, kama unaona unasumbuka sana. tumia dawa ya maumivu kama paracetamol, ibuprofen zitasaidia.

    • 9 months ago (Edit)

    Mimi naumw mgong jamn takriban miak miwili sas na bado umri wang mdogo jamn ss sielew kam barid inawez sababish maumivu ya mgongo????

      • 8 months ago

      Hapana baridi haiwezi kusababisha maumivu ya mgongo, ila wakati wa baridi misuli inaweza kukaza zaidi na kuongeza maumivu kwa baadhi ya watu wenye tatizo la maumivu ya mgongo. Wasiliana na daktari wetu ili kupata maelezo zaidi. Pole sana

    • 9 months ago (Edit)

    Mie nilbeba kitu kizito baada ya siku mbili pingili zkatokeza kwa mbali kwa chini?

      • 9 months ago (Edit)

      Ulipata matibabu na je umepona

      • 9 months ago

      Ni vizr kumwona daktari akufanyie uchunguzi

    • 1 year ago (Edit)

    Asante kwa elimu nzuri hakina nimeilewa…mnatoa matibabu pia??

      • 1 year ago

      Hapana , kwa sasa tunatoa elimu na ushauri

      • 1 year ago

      Tovuti hii ipo kwa ajili ya kutoa ushauri pekee. kama ungependa kuongea nasi .piga namba ya dharura iliyopo hapo.

    • 1 year ago (Edit)

    Ninalo tatizo sugu la kuumwa mgongo. Nisaidie namba yako ili nikufikie kwa urahisi na niweze kusaidika.
    Ahsante sana kwa maelezo mazuri na ya kina.

      • 1 year ago

      Asante wa mrejesho

      • 1 year ago

      asante kwa mrejeshi

    • 2 years ago (Edit)

    asante je vip kuhusu madhara na namna ya kuacha punyeto?

    • 2 years ago (Edit)

    Nimependa maelezo lakini ninaswali
    Vipi mama anaenyonyesha kuwa na maumivu ya mgongo Mara kwa mara

      • 2 years ago

      asante, ni ngumu kujua ana shida gani kwa maelezo haya machache. ningependa kushauri aangalie mkao anaokaa wakati wa kunyonyesha. Ni vizuri mama anayenyonyesha kukaa vizuri akiwa amenyoosha mgogo wakati wa kunyonyesha na si kujipinda muda wote. Kumtegemeza mtoto ni muhimu pia

    • 2 years ago (Edit)

    Mpovizuri Maelezo Excellent thanks for It

      • 2 years ago

      Asante sana
      Na karibu uendelee kujifunza nasi

    • 2 years ago (Edit)

    Mnatoa maelezo mazuri ya kitaalam hongeren sana ,aMungu awabariki

      • 2 years ago

      Asante sana, endelea kuwa nasi

Leave feedback about this

  • Quality
  • Price
  • Service

PROS

+
Add Field

CONS

+
Add Field
Choose Image
Choose Video
X