MAUMIVU YA MIGUU:Sababu,dalili,matibabu

Maelezo ya jumla

Mguu ”foot” unahimili mikwaruzo na shinikizo kubwa sana. Baada ya kusimama au kutembea kwa muda mrefu, unaweza kuwa na maumivu ya miguu na hata kuvimba. Miguu ikitumika sana inaweza kuwa na maumivu ya uwayo, maumivu ya kisigino, maumivu ya misuli ya miguu au kukaza kwa kano “tendons” za miguu. Viatu ambavyo havikutoshi, vinavyobana au ambavyo havikai vizuri miguuni, vinaweza kuongeza matatizo.
Tatizo linaloitwa ‘’Morton’s neuroma’’ linasababisha kuvimba kwa mishipa ya neva iliyopo katikati ya mifupa ya dole gumba na kusababisha maumivu kwenye kifundo cha mguu. Baadhi ya hali zinazoathiri mwili mzima, kama vile jongo ‘’gout’’, kisukari na yabisi kavu ‘’arthritis’’, zinaweza kusababisha maumivu ya miguu.

Mwone daktari kama

Ni vizuri kupanga kumwona daktari:

 • Kama una kisukari au tatizo lolote linalosababisha mzunguko hafifu wa damu miguuni
 • Kama maumivu ya mguu yametokana na kuumia au jeraha

Unachoweza kufanya mwenyewe ukiwa na maumivu ya miguu

Kuna mambo kadhaa unayoweza kufanya ili kupunguza au kuondoa kabisa maumivu ya miguu

 • Vaa viatu vinavyotoshea kwenye miguu, unavyoweza kuchezesha vidole vya mguu bila shida. Epuka viatu vilivyochongoka kwa mbele au vyenye kisigino kirefu kuzidi 5cm. Badilisha badilisha aina ya viatu unavyovaa siku hadi siku ili kupumzisha miguu.
 • Unapotaka kununua viatu, nunua jioni, kwa sababu wakati huu ndio miguu huwa minene zaidi. Usinunue viatu vinavyokubana sana ukitegemea kuwa vitatanuka
 • Kwa michezo au shughuli nyingine nzito, chagua viatu vinavyotoshea vizuri na vinavyofaa kwa shughuli husika.
  • Viatu vya mazoezi vinapaswa kukutosha kabisa kuanzia mwanzo. Kama unafanya mazoezi mara kwa mara, chagua viatu vilivyoundwa kwa kusudi hilo; kwa mfano, kama unakimbia kwenye barabara ngumu. Unahitaji viatu vinavyotegemeza sehemu ya ndani ya mguu na vyenye ‘’cushion’’ kwenye kisigino.

Maumivu ya miguuUnapokuwa unanunua viatu vipya, fuata hatua zifuatazo ili kuhakikisha viatu vinakutosha vizuri

   • Vijaribu viatu unavyotaka kununua ukiwa umevalia ‘’socks’’ utakazovaa navyo
   • Angalia kama viatu vinatoshea vizuri na kushika kisigino na vinakuachia nafasi ya kuchezesha vidole kwa uhuru. Funga kamba za viatu mwenyewe upya ili vibane vizuri na kuongeza shinikizo kwenye sehemu ya juu ya mguu
   • Tembea au kimbia hatua kadhaa ili kuamua au kungalia kuwa viatu havikutii karaha yoyote
 • Unaweza kubadili na kuvaa ‘’sneakers’’, wakati ukiwa unaenda au wakati wa kutoka kazini kama hairuhusiwi kuvaa viatu vingine kazini
 • Kwa ajili ya kutegemeza na ‘’cushining’’ unaweza kuongeza ‘’insole’’ ndani ya kiatu ili kupunguza karaha. Kuna ‘’insole’’ ambazo zimetengenezwa maalumu kwa ajili ya matumizi ya wana michezo, zitafute kwenye maduka ya viatu vya michezo.
 • Kama miguu inauma tumia dawa ya maumivu. Madawa kama vile ‘’ibuprofen’’ au ‘’acetaminophen’’ husaidia kupunguza maumivu ya misuli na maungio. Kama maumivu hayatapungua baada ya kuzitumia kwa siku kadhaa, acha kuzitumia na upange kumwona daktari
 • Loweka miguu ndani ya maji kwa muda mfupi tu, la sivyo itasababisha ngozi kuwa kavu sana. Baada ya hapo paka ‘’moisturizer’’ ili kuiacha ngozi ikiwa nyororo na kuzuia kukauka kwa ngozi. Paka “moisturizer” mara tu baada ya kuoga ili kuufungia unyevu ndani ya ngozi.
 • Kama maumivu yanasababishwa na mazoezi au shughuli fulani unayoifanya, ipunguze au acha kabisa mpaka maumivu yatakapoondoka

Ukiwa na maumivu ya miguu mwone daktari kama

Panga kumwona daktari kama:

 • Una maumivu ya miguu baada ya wiki 2-3 ya kutumia njia zilizoelekezwa hapo juu

Vyanzo

https://medlineplus.gov/ency/article/003183.htm

Leave a Reply

Your email address will not be published.

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.

Jiunge Nasi