Magonjwa ya wanaume

MAUMIVU YA PUMBU:Sababu, matibabu

Last Updated on October 13, 2023 by Dr Mniko

Maelezo ya jumla

Maumivu ya pumbu – jeraha dogo tu kwenye pumbu halisababishi matatizo ya kudumu, lakini maumivu makali yanaweza kutokea kwa sababu ya kujipinda ‘’torsion’’ kwa moja ya korodani iliyo kwenye pumbu, na hii inaweza kusababisha matatizo ya kudumu. Maumivu makali ya pumbu, na wakati mwingine kuvimba kwa pumbu, kunaweza kusababishwa na maambukizi ‘’epididymitis’’. Unaweza pia kuwa na homa na maumivu wakati wa kukojoa. Sababu nyingine za maumivu ni pamoja na matubwitubwi ‘’mumps’’ na kwa mara chache saratani ya korodani.

Unapokua na maumivu ya pumbu unapasawa kumwona daktari haraka

Tafuta usaidizi wa kitabibu haraka kama:

  • Utaanza kuona ghafla tu, maumivu makali ya pumbu
  • Maumivu yataendelea kuwepo kwenye eneo la pumbu uliloumia baada ya saa 1

Panga kumwona daktari mapema kama:

  • Una maumivu ya kadri au ya kawaida kwenye pumbu kwa zaidi ya wiki 2
  • Unadhani una maambukizi kwenye pumbu
  • Unaona kuna uvimbe usioufahamu kwenye pumbu au korodani

Unachoweza kufanya wewe mwenyewe ukiwa na maumivu ya pumbu

Jaribu kufanya mambo yafuatayo  mwenyewe nyumbani ili kupunguza karaha. Unaweza pia kuyafanya sambamba na matibabu yaliyotolewa na daktari.

  • Ili kupunguza maumivu na kuvimba kwa pumbu weka barafu. Chukua barafu iliyo kwenye kifuko, itwange kisha ifunike kwa kitambaa laini na iweke kwenye korodani inayouma. Shikilia hapo kwa dakika 10. Fanya hivi angalau mara 2 kwa siku.
  • Unaweza pia kutumia dawa za maumivu. Dawa za maumivu kama vile ‘’ibuprofen’’ zinapunguza maumivu, uvimbe na hata homa kama utakuwa nayo.
  • Lalia mgongo, kunja taulo vizuri uiweke katikati ya miguu na chini ya pumbu ili kuzinyanyua na kupunguza karaha. Unapotaka kutembea, hasa kama pumbu zimevimba, hakikisha unategemeza pumbu. Usiache pumbu kuning’inia, vaa chupi mbili kwa pamoja zinazoweza kubeba vizuri uzito wa pumbu. Kama zimevimba sana, nunua au tengeneza kibebeo cha kubeba pumbu (pichani)

maumivu ya pumbu

Jinsi ya kuchunguza pumbu zako mwenyewe

Kama maumivu yamepungua, kagua pumbu mara kwa mara kwa kutumia njia ifuatayo

  • Wanaume wote wanapaswa kukagua pumbu mara kwa mara ili kutambua kama kuna uvimbe wowote kwenye korodani au kama kuna mabadiliko yoyote ambayo yanaweza kuwa dalili za mwanzo za saratani
  • Jichunguze angalau mara moja kwa mwezi baada ya kuoga maji ya uvuguvugu, pumbu zikiwa zimelegea. Kagua kama kuna vivimbe au uvimbe. Pande zote za korodani zinapaswa kuwa laini ‘’smooth’’ isipokuwa sehemu ya juu ya korodani na nyuma, ambapo utaushika mrija laini unaobeba na kutunza manii.
  • Linganisha korodani moja na nyingine kama unadhani au una wasiwasi kuwa kuna shida (huwa sio kawaida kupata kansa kwenye korodani zote mbili kwa wakati mmoja).
  • Kama ukiona kuna utofauti au mabadiliko yoyote kwenye korodani, mwone daktari mapema iwezekanavyo ili atambue shida ni nini.

Maumivu ya pumbu

Mwone daktari kama

Panga kumwona daktari kama:

  • Maumivu yanazidi au hayajaanza kupungua baada ya siku 2

Vyanzo

https://medlineplus.gov/ency/article/003160.htm

Leave feedback about this

  • Quality
  • Price
  • Service

PROS

+
Add Field

CONS

+
Add Field
Choose Image
Choose Video
X