Last Updated on October 13, 2023 by Dr Mniko
Maelezo ya jumla
Maumivu ya tumbo ni maumivu yanayotokea popote kati ya kifua na kinena.
Dalili za maumivu ya tumbo?
Karibu kila mtu hupata maumivu ya tumbo kwa wakati mmoja au mwingine, na mara nyingi maumivu haya hayasababiswi na ugonjwa mkubwa. Ukali wa maumivu ya tumbo hauashirii kuwa ugonjwa wako ni mkubwa au la.
Kwa mfano, unaweza kuhisi maumivu makali sana ya tumbo ukiwa na gesi tu tumboni au maumivu ya tumbo yanayosababishwa na kuvimba kwa utando-ute wa tumbo unaosababishwa na virusi.
Kwa upande mwingine, hali zinazoweza kutishia maisha kama vile saratani ya utumbo mpana au kibole zinaweza kusababisha maumivu ya kawaida tu au yasiwepo kabisa.
Njia nyingine za kuelezea maumivu ya tumbo ni pamoja na:
- Maumivu yanaweza kuwa kwenye tumbo lote. Hii ni kawaida kwa mtu aliyevimbiwa au mwenye gesi tumboni. Maumivu yanaweza kuwa makali sana baada ya kuziba kwa utumbo.
- Maumivu ambayo yako kwenye sehemu maalumu huashiria kuwa kuna tatizo katika kiungo kimojawapo tumboni, kama vile kidole tumbo, mfuko wa nyongo, au tumbo.
- Maumivu na tumbo kubana si tatizo kubwa, na mara nyingi husababishwa na kuvimbiwa ambako mara nyingi hufuatiwa na kuhara. Ishara zinazoonesha kuwa hali ni mbaya ni pamoja na maumivu yanayotokea mara kwa mara, yanayokuwepo kwa zaidi ya masaa 24, na kutokea kwa homa.
- Maumivu menine huja na kuondoka. Maumvu haya huanza na kukatika ghafla, na mara nyingi ni makali sana.Mara nyingi aina hii ya maumivu husababishwa na mawe kwenye figo au mfuko wa nyongo.
Ni nini husababisha maumivu ya tumbo?
Hali nyingi zinaweza kusababisha maumivu ya tumbo. Kitu muhimu ni kujua ni wakati gani unahitaji kupata huduma za matibabu ya haraka.
Sababu za maumivu kwenye tumbo ni pamoja na:
- Kufunga choo
- Mzio wa chakula (kama vile mzio wa bidhaa za maziwa)
- Kula chakula kichafu
Sababu nyingine ni pamoja na:
- Kibole
- Kuziba kwa utumbo au tumbo
- Saratani ya tumbo, koloni, na viungo vingine
- Kuvimba kwa mfuko wa nyongo au mawe kwenye mfuko wa nyongo
- Kupungua kwa mtiririko wa damu kwenye tumbo au utumbo
- Kiungulia, kuvimbiwa, au Kucheua
- Ugonjwa wa kuvimba utando ute wa tumboMatumbo ya uchochezi (Crohn’s disease au ulcerative colitis)
- Mawe kwenye figo
- Kuvimba kwa kongosho
- Vidonda vya tumbo
Wakati mwingine maumivu ya tumbo yanaweza kusababishwa na tatizo mahali pengine mwilini, kama vile kifuani au eneo la nyonga. Kwa mfano, unaweza kuwa na maumivu ya tumbo kama una:
- Mshtuko wa moyo
- Kukaza kwa misuli
- Ugonjwa wa kuvimba kwa mirija ya kizazi na kizazi (PID)
- Nyumonia
- Maumivu makali yanayosababishwa na hedhi
- Mimba iliyotungwa nje ya mji wa mimba
- Maambukizi kwenye njia ya mkojo
Utambuzi wa maumivu ya tumbo
Mtoa huduma ya afya atafanya uchunguzi wa mwili na kuuliza maswali kuhusu dalili zako na historia ya tatizo lako. Ukali wa dalili, mahali maumivu yalipo na muda yanapotokea. Majibu ya maswali haya na mengine mengi yatamsaidia daktari kufanya utambuzi.
Unaweza kuulizwa maswali yafuatayo:
- Unahisi wapi maumivu?
- Je, maumivu yametapakaa kwenye tumbo lote au mahali fulani maalumu?
- Je, maumivu yanatapakaa kwenda kwenye mgongo, kinena, au miguu?
- Je, maumivu ni mkali sana, yanakata, au kubana?
- Je, unapata maumivu wakati wote au yanakuja na kuondoka ?
- Je, maumivu yanakuamsha usiku toka usingizini?
- Je, umewahi kupata maumivu kama hayo hapo zamani? Yalidumu kwa muda gani?
- Je! Maumivu hutokea wakati gani? Kwa mfano, kabla ya kula, baada ya kula au wakati wa hedhi?
- Ni nini husababisha maumivu kuwa makali zaidi? Kwa mfano, kula, msongo, au kulala chali?
- Ni nini hufanya maumivu kupungua? Kwa mfano, kunywa maziwa,na kula chakula?
- Je! maumivu hupungua baada ya Kuharisha, au kutumia dawa za kupunguza asidi tumboni?
- Je, unatumia dawa gani?
- Umekuwa na jeraha la hivi karibuni?
- Je! Una ujauzito?
- Una dalili gani nyingine?
Vipimo vinavyoweza kufanyika ni pamoja na:
- Barium enema
- Vipimo vya damu, mkojo, na kinyesi
- Colonoscopy au sigmoidoscopy
- CT scan
- EKG (electrocardiogram)
- Ultrasound ya tumbo
- Eksirei ya tumbo
Ukiwa na maumivu ya tumbo ni wakati gani utafute matibabu ya haraka?
Tafuta usaidizi wa haraka kama:
- Uko kwenye matibabu ya saratani
- Una mimba au kuna uwezekano ukawa mjamzito
- Hupati kinyesi, hasa ikiwa unatapika pia
- Unatapika damu au kuna damu kwenye kinyesi chako (hasa ikiwa ni cheusi au chenye rangi kama lami)
- Umepata jeraha tumboni hivi karibuni
- Una maumivu kifuani, shingoni, au kwenye mabega
- Unapata shida kupumua
- Una maumivuma ndani, au katikati ya bega yako na kichefuchefu
- Umepata maumivu makali ya tumbo ghafla
- Tumbo lako linauma likiguswa au limekuwa gumu na lililokakamaa sana
Mwone daktari kama una:
- Usumbufu tumboni unaodumu kwa wiki 1 au zaidi
- Maumivu ya tumbo ambayo hayapoi baada ya masaa 24 – 48, au yanakuwa makali zaidi, yanatokea mara kwa mara na una kichefuchefu na kutapika
- Kuvimbiwa kunakodumu kwa zaidi ya siku 2
- Maumivu wakati wa kukojoa au unakojoa mara kwa mara kuliko ilivyo kawaida, hasa usiku
- Kuharisha kwa zaidi ya siku 5
- Homa (zaidi ya 100 ° F kwa watu wazima au 100.4 ° F kwa watoto)
- Kukosa hamu ya chakula kwa muda mrefu
- Kutokwa damu ukeni kwa muda mrefu
- Kupungua kwa uzito bila sababu maalumu
Uchaguzi wa matibabu ukiwa na maumivu ya tumbo
Kama una maumivu ya tumbo ya kawaida tu, vidokezo vifuatavyo vinaweza kusaidia:
- Kunywa maji kidogo au kinywaji kingine chepesi.
- Epuka kula chakula kigumu kwa masaa kadhaa ya mwanzo.
- Kama unatapika, subiri masaa 6, kisha kula kiasi kidogo cha chakula chepesi kama vile wali, ndizi, au uji. Bidhaa za maziwa zinapaswa kuepukwa.
- Maumivu yakiwa kwenye sehemu ya juu ya tumbo na yakiwa yanatokea baada ya kula chakula, antacids zinaweza kusaidia, hasa kama unapata kiungulia au umevimbiwa . Epuka kula vitu vichachu , yakula vyenye mafuta mengi, bidhaa za nyanya, kahawa, na vinywaji baridi.
- Epuka kutumia aspirini, ibuprofen au dawa nyingine za kupunguza uvimbe au maumivu kama haujaagizwa na daktari.
Dawa za kuepuka
Wagonjwa wanaopata maumivu ya tumbo bila kuharisha wanapaswa kuepuka kutumia dawa zifuatazo:
- Loperamide
Kama unapata maumivu ya tumbo bila kuharisha, ongea na daktari kabla ya kuanza au kuacha kutumia moja ya dawa hizi.
Kuzuia
Hatua zifuatazo zinaweza kusaidia kuzuia aina fulani za maumivu ya tumbo:
- Epuka kula vyakula vyenye mafuta mengi .
- Kunywa maji ya kutsha kila siku.
- Kula chakula kidogo kidogo mara kwa mara.
- Fanya mazoezi mara kwa mara.
- Punguza kula vyakula vinavyozalisha gesi.
- Hakikisha kwamba unakula mlo kamili. Kula matunda na mboga kwa wingi.
Leave feedback about this