MAUMIVU YA UUME:Sababu, matibabu…

Maelezo a jumla

Maumivu ya uume – ngozi inayoufunika uume ni nyepesi na ni rahisi kuumia. Mikwaruzo midogo midogo inaweza kutokea wakati wa michezo au wakati wa ngono. Maumivu kwenye kichwa cha uume yanaweza kusababishwa na usafi duni au kwa sababu ya harara inayosababishwa na sabuni au maambukizi, hii ni pamoja na maambukizi ya magonjwa ya ngono. Dalili nyingine za magonjwa ya ngono ni pamoja na upele, uchafu kutoka kwenye uume na maumivu wakati wa kukojoa. Kwa wale ambao hawajatahiriwa, wanaweza kupata maumivu uume ukisimama au wakati wa ngono kwa sababu ya govi kubana sana ‘’overtight’’.

Ukiwa na maumivu ya uume mwone daktari haraka sana kama

Tafuta usaidizi wa kitabibu haraka kama:

 • Una maumivu na uume umesimama kwa muda mrefu japo msisimko wa tendo la ngono umeisha
 • Unashindwa kurudisha govi mbele baada ya kujirudisha nyuma wakati wa ngono au wakati mwingine wowote

Panga kumwona daktari mapema kadri unavyoweza kama:

 • Unadhani kwamba una ugonjwa wa ngono au kama hauna uhakika ni nini kinasababisha maumivu

Maumivu ya uume

Unachoweza kufanya wewe mwenyewe unapokuwa na maumivu ya uume

Kuna mambo kadhaa unayoweza kufanya ili kupunguza karaha na kuzuia maumivu ya uume

 • Hakikisha kuwa uume ni msafi. Oga kila siku. Kama haujatahiriwa, vuta nyuma govi na safisha kichwa cha uume taratibu kwa kutumia maji na sabuni ya kawaida. Kausha vizuri kichwa cha uume kwa kutumia taulo safi.
 • Ili kupunguza karaha, vaa chupi isiyo bana sana
 • Kama kichwa cha uume kitakuwa kimevimba au kinauma wakati wa ngono, unaweza kuzuia hili kutokea kwa kupaka kilainishi kwenye kichwa cha uume kabla ya tendo.
  • ‘’Water soluble lubricating jelly’’ zinapatikana madukani na zitakupunguzia karaha. Zinasaidia kuzuia maumivu ambayo yanaweza kutokea kwa sababu ya msuguano unaotokana na shughuli ya ngono
  • Osha vizuri uume baada ya tendo la ngono
  • Kama unadhani tatizo linatokana na kondomu unazozitumia, badili ujaribu kutumia ambazo hazijatengenezwa kwa ‘’latex’’.
  • Kama una jeraha dogo kwenye kichwa cha uume, subiri lipone kabla ya kufanya ngono tena.
  • Kama unadhani tatizo ni sabuni unayoogea au bidhaa unazoumia kufulia, badili utumie ambazo sio kali au zinazodufaa mzio ‘’nonallergenic’’ kufua nguo za ndani.
 • Kama una ugonjwa wa ngono, kuoga kwa kutumia maji yaliyo tiwa chumvi inaweza kusaidia kupunguza dalili
  • Kusafisha uume mara 2 au 3 kwa siku kwa kutumia maji ya uvuguvugu yaliyotiwa chumvi, husaida kupunguza uvimbe na maumivu.
  • Chukua chumvi kwa viganja na utie kwenye maji yaliyo kwenye beseni. Jaza beseni mpaka kufikia theluthi mbili (2/3). Oga maji yake huku ukiosha uume taratibu.
  • Kama unapata karaha unapokuwa unakojoa. Kaa kwenye beseni lenye maji ya uvuguvugu na chumvi na jaribu kukojoa ukiwa umekaa humo. Kumbuka kuoga na kuosha vizuri beseni baada ya kumaliza.

Mwone daktari kama

Panga kumwona daktari au mwone mtaalamu wa magonjwa ya mfumo wa mkojo ‘’urologist’’ kama:

 • Maumivu kwenye uume yataendelea kuwepo, au kamaunaanza kuona dalili nyingine zinajitikeza

Vyanzo

https://medlineplus.gov/ency/article/003166.htm

Comments

Leave a Reply

Your email address will not be published.

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.

Jiunge Nasi