MAWE KWENYE MFUKO WA NYONGO:Sababu, dalili

Mawe kwenye mfuko wa nyongo ni nini?

Mawe kwenye mfuko wa nyongo – Mfuko wa nyongo ni kiungo kinachotumika kutunzia kimiminika kinachoitwa nyongo kinachosaidia katika umeng’enyaji wa chakula. Mawe kwenye mfuko wa nyongo hutokana na lehemu na vitu vingine ndani ya nyongo vinapoungana na kutengeneza mawe mawe. Mawe haya yanaweza kuwa madogo sawa na vijiwe vidogo au vikubwa sawa na ukubwa wa mpira wa golf.

mawe kwenye mfuko wa nyongoMawe kwenye mfuko wa nyongo husababisha dalili zipi?

Watu wengi hawafahamu kama wana mawe kwenye mfuko wa nyongo. Wakati mwingine, mawe yanaweza kupita kutoka kwenye mfuko wa nyongo na kuingia kwenye utumbo. Kama jile likikwama wakati wa kuteremka, linaweza kusababisha maumivu makali sana upande wa kulia juu mwa tumbo. Maumivu yanaweza kuwa yanakuja na kuondoka, au yanaweza kubakia muda wote. Wakati mwingine maumivu yanaweza kuanza baada tu ya kula. Unaweza pia kuwa na homa au kutetemeka kama mfuko wa nyongo umepata maambukizi.

Ni nini huongeza hatari ya kupata mawe kwenye mfuko wa nyongo?

Uko kwenye hatari zaidi ya kupata mawe kwenye mfuko wa nyongo kama una uzito mkubwa sana wa mwili, una ugonjwa wa kisukari, una kiwango cha juu cha mafuta mwilini, umefunga, au kama umeamua kupunguza uzito wa mwili haraka sana. Watu wa umri wa kati na wanawake  (hasa wajawazito au wanaotumia dawa za kupanga uzazi) wako kwenye hatari zaidi ya kupata mawe kwenye mfuko wa nyongo. Kama kuna mtu kwenye familia ana mawe kwenye mfuko wa nyongo, basi nawe upo kwenye hatari pia.

mawe kwenye mfuko wa nyongoJe, tatizo la mawe kwenye mfuko wa nyongo linatibiwaje?

Kama una mawe kwenye mfuko wa nyongo na hauna maumivu yoyote, unaweza usihitaji matibabu yoyote. Ukipata maumivu mara moja, kuna uwezekano kuwa yatajirudia tena. Kwa kisa kama hiki, daktari anaweza kupendekeza upasuaji ufanyike ili kuondoa kabisa mfuko wa nyongo.

Yanaweza pia kutumika mawimbi ya sauti kuvunja vunja mawe kwenye mfuko kwa watu ambao hawataki au hawawezi kufanyiwa upasuaji. Aina hii ya matibabu inavunjavunja mawe ili yateremke na kuingia kwenye utumbo bila kukwama. Lakini, njia hii haiwezi kuzuia mawe mengine mapya kutengenezeka.

Unaweza pia kujaribu kutumia dawa ili kuyeyusha haya mawe. Inaweza kufanya kazi kwa baadhi ya watu, lakini sio kwa watu wote. Wewe na daktari mnapaswa kuongea na kukubaliana mpango sahihi wa matibabu utakaokufaa wewe mwenyewe.

Angalizo

Taarifa zilizotolewa katika ukurasa huu zimetoa muhtasari na zinaweza zisimfae kila mtu. Ongea na daktari ili kung’amua kama taarifa hizi zinakufaa wewe au jaribu kutafuta habari zaidi kuhusu shida hii.

Vyanzo

https://medlineplus.gov/gallstones.html

Leave a Reply

Your email address will not be published.

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.

Jiunge Nasi