MENO: Yanaota lini, matundu, usafi, matibabu

Ni lini meno ya mwanao yatakapo tokeza?

Kila mtoto ni tofauti, lakini meno kwa kawaida huanza kuota anapofikia umri wa miezi sita, japo mwanao anaweza kuanza kutokwa mate mengi anapofikia miezi minne. Meno yanapoanza kuota, yanaweza kusababisha maumivu na kusababisha mtoto asitulie.

Meno yenye afya ni muhimu

Meno yenye afya ni muhimu kwa afya ya mtoto kwa ujumla. Meno humsaidia mtoto kutafuna chakula na husaidia katika kuumba maneno/sauti anapoongea. Yanaathiri pia namna taya za mtoto zinapokua.

Nifanye nini ili kumsaidia mtoto anayeota meno?

Unaweza kumpatia mwanao kipande cha nguo au ring ya plastic ili aendelee kukutafuna. Kuota meno hakusababishi homa. Kama mwanao ana homa, ni vizzuri kuongea na daktari wake.

Mashimo kwenye meno ni nini?

Usafi wa meno unazuia matundu kwenye menio

Mashimo au matundu kwenye meno yanaweza kusababisha maumivu na hata maambukizi mabaya. Matundu ya meno husababishwa na tindikali (asidi) inayotengenezwa na bakteria wanaomeng’enya mabaki ya chakula yanayobakia kwenye meno. Tindikali hizi zinapobakia kwenye meno kwa muda mrefu huchimba chimba na kuharibu jino. Matundu ya meno ndio tatizo la meno linalowasumbua zaidi Watoto. Usafi mzuri wa meno unaweza kumkinga mtoto kupata tatizo hili.

Je, mwanangu yuko kwenye hatari ya kupata tundu kwenye jino?

Mwanao anaweza kuwa katika hatari ya kupata mashimo au matundu kwenye meno kama anakula sana vyakula vyenye sukari nyingi (kama vile pipi, keki, peremende) na vinywaji  vyenye sukari nyingi (kama vile juisi ya matunda, soda, maziwa na vinywaji vingine vya viwandani). Mwanao anweza kuwa kwenye hatari kama ana mambo yafuatayo yanayoongeza hatari:

  • Alizaliwa mapema ( mtoto njiti) au alizaliwa na uzito mdogo sana (chini ya kilo 2.8)
  • Ana mahitaji maalumu ya kiafya anayoendelea kupata
  • Kama ana mabaka meupe au ya kahawia kwenye meno
  • Kama haujampeleka kwa dakatari wa meno mara kwa mara

Kwa nyongeza, Watoto wanaozaliwa kwenye familia ambayo Watoto wakubwa wanakula vyakula vya sukari nyingi, wana matundu kwenye meno na hawaendi kuonana mara kwa mara na dakatari wa meno wako kwenye hatari kubwa ya kupata matundu kwenye meno.

Unaweza kuzuia vipi matundu kwenye meno?

Kitu cha kwanza ni kwa kila mtu kwenye familia kuanza kujali afya ya kinywa. Wanafamilia wenye matundu mengi kwenye meno wanaweza kuwaambukiza  watoto bakteria wanaosababisha matatizo kwenye meno.

Meno yanapashwa kusafishwa (kwa mswaki) mara 2 kwa siku na kwa watu wazima wanapaswa kutumia nyuzi za hariri kuondoa uchafu kwenye meno angalau mara 1 kwa siku. Kila mwanafamilia anapaswa kuonana na daktari wa meno angalau mara 2 kwa mwaka. Ongea na daktari wa meno akufundishe namna nzuri ya kusafisha meno yako.

Mama anamfundisha mwanae kusafisha meno

Dhibiti matumizi ya vyakula vyenye sukari nyingi. Kula vyakula na vitafunwa kwa wakati maalumu kila siku. Kula vyakula vyenye sukari mara kwa mara kunaweza kusababisha matundu. Vyakula vinavyochangia afya ya meno ni pamoja na matunda, mbogamboga na jibini.

Vipi kuhusu kunyonyesha maziwa ya mama, maziwa ya chupa?

Kunyonya maziwa ya mama kunaongeza afya ya meno ya mwanao. Kama unampatia mwanao maziwa ya kopo, mpatie ukiwa umemshikilia. Usiache chupa ya maziwa karibu na sehemu aliyolala. Usiongeze juisi kwenye chupa ya maziwa.

Kama mwanao ana umri wa mwaka mmoja au zaidi, mpatie maji pekee au maziwa badaya ya vinywaji vingine katikati ya mlo. Kama unampatia juisi au maziwa yenye sukari, mpatie anapokuwa anakula chakula. Maziwa yaliyowekwa ladha yana sukari nyingi ndani.

Nianze lini kusafisha meno ya mtoto wangu?

Anza kusafisha meno ya mwanao mara 2 kwa siku baada tu ya jino la kwanza kuota. Muda mzuri wa kusafisha meno ni kabla ya kulala. Tumia mswaki laini wa Watoto. Weka dawa ya meno kidogo kwenye mswaki. Weka dawa ya meno kidogo kama punji ya mchele. Unaweza kumuuliza daktari wa meneo ni dawa gani inafaa zaidi kwa mwanao. Anaweza kupendekeza utumie dawa ya mswaki yenye fluoride (madini joto) ili kukinga meno ya mwanao.

Baadhi ya dawa za kusafisha meno zilizotengenezwa kwa ajili ya Watoto hazina fluoride. Kama unatumaia aina ya dawa ya meno isiyo na fluoride, hakikisha unabadilisha na kutumia yenye fluoride mwanao anapofika umri wa miaka 2. Mwanao anaweza kuhitaji msaada wakati wa kusafisha meno mpaka atakapofikia umri wa miaka 8.

meno
Anapaswa kumwona daktari wa meno

Ni wakati gani nimpeleke mwanangu kwa dakatari wa meno?

Mwanaoa anapaswa kumwona daktari wa meno anapofika mwaka wa kwanza wa maisha yake, hasa kama mtoto yuko kwenye hatari zaidi ya kupata matundu ya meno au matatizo mengine ya meno. Ni vizuri mwanao kuonana na daktari mapema kabla hajaanza kuwa na matatizo ya meno. Kama unapenda kusubiri mpaka mwanao afike miaka 2 au 3, hakikisha unafuatilia vizuri ushauri uliotolewa hapa.

Vyanzo

https://medlineplus.gov/ency/article/002045.htm

Leave a Reply

Your email address will not be published.

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.

Jiunge Nasi