MAGONJWA YA MOYO: Mlo/Chakula/Ulaji unaofaa

Magonjwa ya moyo

Magonjwa ya moyo yanahusisha yale magonjwa yote yanayoathiri moyo na mishipa yake. Magonjwa ya moyo yanajumuisha magonjwa yanayoathiri mishipa ya moyo, mshtuko wa moyo, kushindwa kwa moyo kufanya kazi na kuziba kwa mishipa ya moyo. Tafiti zimeonesha kuwa magonjwa ya moyo huanza pale ambapo sehemu ya ndani ya kuta za mishipa ya damu zimeharibiwa.

Mambo yanayochangia katika kuharibu mishipa ya damu ni pamoja na: ­

mgonjwa ya moyo

Kuta za mishipa ya damu zikiharibiwa, mafuta hujikusanya katika sehemu ya mishipa iliyoharibiwa na kutengeneza utando wa mafuta (plaque). Kadiri muda unavyoendelea ndivyo mafuta haya yanavyozidi kujijenga katika sehemu hiyo hadi kufanya mishipa kuwa myembamba na hivyo kupunguza kiasi cha damu kinachobeba hewa ya oksijeni na virutubishi kwenda kwenye misuli ya moyo. Hatimaye sehemu hiyo ya mshipa inaweza kupasuka. Kama sehemu hiyo ikipasuka, chembe-sahani za damu ambazo husaidia m

wili kuponya kidonda hujigandisha kwenye mpasuko na hivyo kuanza kujikusanya. Hali hii huongeza mkusanyiko wa chembe-sahani, hivyo kuendelea kufanya mishipa hiyo kuwa myembamba zaidi na hali hiyo husababisha moyo kushindwa kufanya kazi na mtu hupata ugonjwa wa moyo uitwao shambulio la moyo (heart attack). Mkusanyiko wa mafuta na chembesahani wakati mwingine huweza kumeguka kama mabonge madogo madogo na kusafiri kwenda kuziba mishipa midogo ya damu ya kichwani. Hali hii ikitokea mtu hupata kiharusi na mabonge yakienda kwenye mishipa ya moyo mtu hupata shambulio la moyo.

Hali ya kujijenga kwa mafuta na chembe-sahani hutokea polepole, huchukua muda mrefu na huweza kujitokeza kwa dalili kama kupanda kwa shinikizo la damu.

Mambo yanayoongeza uwezekano wa magonjwa ya moyo

Mambo yanayoongeza uwezekano wa kupata magonjwa ya moyo ni pamoja na: ­

Dalili za magonjwa ya moyougonjwa wa moyo

Dalili za magonjwa ya moyo hutofautiana kutegemeana na aina ya ugonjwa wa moyo. Hata hivyo, dalili za magonjwa haya ni pamoja na: ­

Katika shambulio la moyo hakuna dalili inayojitokeza hadi pale moyo unaposhindwa kufanya kazi ghafla (heart attack), au mtu anapopata kiharusi. Hata hivyo, hadi mtu anapoanza kupata dalili hizo huwa amekuwa ameishi na ugonjwa huo kwa muda mrefu. Hivyo, njia bora ya kugundua mapema dalili ya ugonjwa ni kuchunguzwa afya yako mara kwa mara kabla hujaugua.

Ulaji unaoshauriwa kwa watu walioathirika na magonjwa ya moyo

Ni muhimu sana kwa mgonjwa wa moyo kufuata kwa makini taratibu za matibabu kama alivyoshauriwa na daktari. Mtindo bora wa maisha utachangia sana kupunguza tatizo. Punguza mambo yanayoongeza uwezekano wa kupata ugonjwa wa moyo ikiwa ni pamoja na kufanya yafuatayo: ­

 • Kupunguza matumizi ya mafuta na epuka mafuta yatokanayo na wanyama, pamoja na nyama yenye mafuta; ­
 • Kupunguza ulaji wa nyama hususan nyama nyekundu (isizidi nusu kilo kwa wiki); ­
 • Kupunguza vyakula vyenye lehemu kwa wingi kwa mfano mayai, maini, moyo, figo, mafuta yenye asili ya wanyama (kama samli na siagi) na nyama nyekundu; ­
 • Kuepuka vyakula au vinywaji vinavyosababisha ongezeko la uzito, ikiwa ni pamoja vyakula vyenye sukari nyingi au mafuta mengi, soda, juisi bandia na pombe; ­
 • Kupunguza kiasi cha chumvi unachotumia na epuka vyakula vyenye chumvi nyingi; ­
 • Kufanya mazoezi ya mwili angalau dakika 30 kila siku; ­
 • Kuhakikisha una uzito unaoshauriwa kutegemeana na urefu wako; ­
 • Epuka vyakula vilivyosindikwa kwa mafuta na chumvi nyingi; ­
 • Kula mbogamboga na matunda kwa wingi katika kila mlo; ­
 • Kupendelea zaidi kula vyakula vya nafaka zisizokobolewa kama dona na ngano; vilevile ulezi na mtama; na ­
 • Kupendelea zaidi kula vyakula vya jamii ya kunde.

Mbinu za kupunguza uwezekano wa kupata magonjwa ya moyomagonjwa ya moyo

Unaweza kupunguza uwezekano wa kupata magonjwa ya moyo kwa kufuata mtindo bora wa maisha, ikiwa ni pamoja na: ­

 • Kutumia mafuta kwa kiasi kidogo na kuepuka yale yanayotokana na wanyama; ­
 • Kupunguza ulaji wa nyama nyekundu, hususan zenye mafuta; ­
 • Kuongeza matumizi ya nafaka hasa zile zisizokobolewa kama unga wa dona, unga wa atta, ulezi na mtama; ­
 • Kuongeza ulaji wa vyakula vya jamii ya kunde, mbogamboga na matunda; ­
 • Kufanya mazoezi ya mwili angalau dakika 30 kila siku; ­
 • Kudhibiti uzito wa mwili; ­
 • Kuepuka msongo wa mawazo; ­
 • Kuepuka uvutaji wa sigara au utumiaji wa tumbaku; ­
 • Kutumia dawa za shinikizo kubwa la damu bila kukosa kama ilivyoelekezwa na mtaalam wa afya;
 • Kuepuka au kupunguza matumizi ya pombe; ­
 • Kuwa na tabia ya kupima afya yako mara kwa mara ili kujua hali yako ya afya na kugundua mapema kama kuna tatizo.

Inawezekana usiweze kutimiza yote kwa mara moja, lakini kila unapopiga hatua ni mchango mzuri kwa maisha yako. Jiwekee malengo na anza kuyatimiza hatua kwa hatua.

Vyanzo

https://www.tfnc.go.tz/publications/9

 

Leave a Reply

Your email address will not be published.

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.

Jiunge Nasi