UMUHIMU WA MLO KAMILI

Mlo kamili na umuhimu wake

Mlo kamili ni ule ambao hutokana na chakula mchanganyiko kutoka katika makundi yote ya chakula. Mlo huu unapoliwa kwa kiasi cha kutosha kulingana na mahitaji ya mwili angalau mara tatu kwa siku huupatia mwili virutubishi vyote muhimu na huupa mwili afya bora

Jinsi ya kupanga mlo kamili ­mlo kamili

  • Mlo kamili hupangwa kwa kuchagua angalau chakula kimoja kutoka katika kila kundi la vyakula na kuliwa kwa pamoja ­
  • Tumia vyakula vinavyopatikana katika mazingira unayoishi na vile ambavyo vipo kwenye msimu, kwani ni freshi na bei huwa nafuu.
  • Ili mtu awe na afya na hali nzuri ya lishe anapaswa kuzingatia ulaji bora.
  • Mlo kamili humwezesha mtu kula vyakula mchanganyiko ili kuupatia mwili mahitaji yake ya kilishe kikamilifu. Mtu anapokula chakula kwa kiasi cha kutosha kulingana na mahitaji yake, mwili hupata virutubishi vyote muhimu.
  • Mara nyingi mlo wako ukiwa na vyakula vyenye rangi mbalimbali pia huwa na virutubishi vingi; hivyo chagua vyakula, matunda na mbogamboga zenye rangi mbalimbali.

Umuhimu wa kula vyakula mchanganyiko (mlo kamili)mlo kamili

Ni muhimu kula vyakula mchanganyiko kwa sababu baadhi ya virutubishi hutegemeana ili kuweza kufanikisha kazi zake mwilini. Mfano wa virutubishi vinavyotegemeana ni: ­

  • Madini chuma na vitamini C: Aina ya madini chuma (non – haem) yanayopatikana kwenye vyakula vya mimea kama mboga-mboga za kijani na vyakula vya jamii ya kunde hufyonzwa kwa ufanisi mwilini iwapo katika mlo huo kuna vitamini C ambayo hupatikana kwa wingi kwenye matunda, mfano chungwa, pera, nanasi, pesheni, ubuyu. ­
  • Vitamini zinazoyeyuka kwenye mafuta (A, D, E na K) hutumika kwa ufanisi mwilini kutegemea uwepo wa mafuta katika mlo. Hivyo basi, ni muhimu kutumia mafuta kidogo wakati wa kupika hususan mboga-mboga.

Vyanzo

https://www.tfnc.go.tz/publications/9

Leave a Reply

Your email address will not be published.

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.

Jiunge Nasi