Kuhusu WikiElimu

Kwa Nini Tuliamua Kuanzisha WikiElimu

Inaumiza sana unapotafuta ugonjwa uliombiwa kuwa unaumwa na daktari kwenye mtandao ili upate habari zake na haupati taarifa zake kokote kwa lugha ya kiswahili. Jambo hili linaumiza sana. WikiElimu iliundwa ili kujibu kilio hiki cha jamii.WikiElimu inalenga kuwapa watoa huduma za afya uwanja wa kuelimisha jamii yao kwa lugha ya kiswahili.

Teknolojia ya habari imefungua uwanja mpana wa kutoa habari na ukiritimba wa kutoa habari unapungua. Watu wako huru kutuma na kupokea habari kwa uhuru zaidi.

Ninatambua pia kuwa jamii zinazo tuma na kupokea habari na kugawana ujuzi kwa uhuru zaidi, hukua na kuendelea kwa haraka zaidi. Kujifunza kwa kushirikishana ujuzi na habari ni ufunguo wa maendeleo ya sasa na baadae.

Huduma ya afya huhitaji kukuza roho ya ushirikiano kati ya watoa huduma za afya ,wagonjwa na jamiii kwa ujumla na huu ndio msingi wa WikiElimu. Watoa huduma za afya wanaoandika na kuhariri makala/ibara katika tovuti hii hujitolea kuandika ili kuhakikisha kuwa taarifa za kuaminika za kiafya zinakuwepo mtandaoni kwa lugha ya kiswahili,ili mwanajamii atakapohitaji kuzipata azipate kwa lugha atakayoielewa kwa urahisi.

Tovuti hii inatoa nafasi pia kwa mwanajamii kuongea moja kwa moja na daktari kwa njia ya mtandao ili kupata matibabu, majibu ya maswali kuhusu afya na ushauri

WikiElimu inalenga kutoa fursa kwa jamii inayozungumza kiswahili kupata habari za kiafya kwa lugha ya kiswahili.

Jiunge Nasi