MZIO

MZIO

 • October 26, 2020
 • 0 Likes
 • 143 Views
 • 0 Comments

Maelezo ya jumla

Mzio (allergy) ni muuitikio (reaction) wa kinga ya mwili usio kawaidMa, unaotokea kwa kitu ambacho kwa kawaida hakidhuru. Kuna aina nyingi za mzio, aina hizi hugawanywa kulingana na vitu vinavyousababisha au mahali unapotokea. Kwa mfano: Mzio unaosababishwa na vumbi,manyoya ya wanyama, madawa, chakula au nyasi kavu, Mzio kwenye ngozi, pua au macho.

Je, nini dalili za mzio?

Dalili hutofautiana, lakini zinaweza kujumuisha:

Namna dalili zinavyotokea huchangiwa sana na sehemu iliyokutana na kizio. Kwa mfano:

 • Unapovuta hewa yenye kizio, husababisha kuziba kwa pua,kuwashwa pua na koo,kutoa makamasi, kukohoa, au kukorota.
 • Macho yanapoguswa na kizio husababisha kuwashwa,kutoa machozi ,macho kuvimba na kuwa mekundu.
 • Kula kitu ambacho una mzio nacho husababisha kichefuchefu, kutapika, maumivu ya tumbo, kuhara na reaction inayoweza kutishia maisha.
 • Kizio kinachogusa ngozi kinaweza kusababisha upele kwenye ngozi, kuwashwa, malengelenge na hata kuchubuka ngozi.
 • Dawa zingine zinaweza kusababisha shida hii, inaweza kuathiri mwili mzima na kusababisha dalili mbalimbali.

Mzio husababishwa na nini?

Mfumo wa kinga ya mwili huulinda mwili dhidi ya vitu hatarishi kama bakteria na virusi. Mfumo huu hupambana na kitu chochote kigeni kinachoingia mwilini. Kwa watu wengine mfumo huu hupambana hata na vitu vya kawaida kabisa ambavyo katika hali ya kawaida haviwadhuru watu wengine, vitu hivi huitwa kizio (allergen). Mfumo wa kinga ya mwili unapogundua kuwa kuna kizio mwilini hutoa kemikali kama vile histamines ambazo hupambana na kizio hicho. Hii husababisha kuwashwa ,kuvimba, kutokwa na makamasi, misuli kubana, vipele na dalili nyingine, ambazo hutofautiana kati ya mtu na mtu.

Mifano ya kizio ni pamoja na chavua (pollens), kutu, manyoya ya wanyama ,vumbi na mzio wa chakula. Mjibizo wa mzio unaweza kusababishwa na aina fulani za wadudu, mapambo, vipodozi, viungo vya jikoni, na vitu vingine.

Kwa mara nyingi aina hizi maalumu za mzio sio za kurithi. Lakini kama wazazi wako wote wawili wana mzio ,kuna uwezekano mkubwa wa kuwa na tatizo hili pia. Uwezekano wa kuwa na mzio ni mkubwa zaidi kama mama anao pia. Tatizo hili linaweza kufanya aina fulani za magonjwa kuwa mbaya zaidi, kwa mfano Pumu na ukurutu.

Utambuzi

Mtoa huduma ya afya atafanya uchunguzi wa mwili na kuuliza maswali kadhaa, mf:wakati gani mzio hutokea?.

Upimaji wa allergy unaweza kuhitajika ili kuhakikisha kuwa dalili zinasababishwa na mzio wa aina fulani na sio ugonjwa mwingine. Kwa mfano, kula chakula kichafu (chakula chenye sumu) kunaweza kusababisha dalili zinazofanana na mzio wa chakula. Dawa nyingine (kama vile aspirini na ampicillin) zinaweza kusababisha athari zinazofanana na mzio. Kutokwa na kamasi puani kunaweza kuwa kumesababishwa na maambukizi fulani.

Upimaji wa ngozi ndio njia inayotumika zaidi kupima Mzio. Njia moja wapo ya kupima ngozi ni ile ya kutoboa ngozi (prick test) na kuweka kiwango kidogo cha kitu kinachohisiwa kuwa kizio na kisha ngozi kuangaliwa kwa ukaribu ili kuoana ishara za mjibizo (reaction), ambazo hujumuisha uvimbe na wekundu. Kupima ngozi ni chaguo zuri kwa watoto wadogo.

Aina nyingine za vipimo vya ngozi ni pamoja na patch testing (kupima kwa kubandika kitambaa chenye kizio husika kwenye ngozi) na intradermal testing (kuweka kizio chini ya ngozi).

Vipimo vya damu vinaweza kupima kiwango cha kemikali maalumu inayohusiana na mzio kwenye damu, hasa inayoitwa immunoglobulin E (IgE).

Complete blood count (CBC) – Kipimo hiki huhesabu kiwango cha seli kwenye damu. Aina ya seli nyeupe inayoitwa eosinophil  huongezeka sana wakati wa shida hii.

Katika hali fulani, daktari anaweza kukuambia uepuke vitu fulani fulani ili uone kama utapata nafuu, au kutumia vitu fulani unavyovihisi ili kuona kama hali itakuwa mbaya zaidi. Hii mara nyingi hutumiwa kuchunguza mzio wa chakula au dawa.

Wakati gani utafute tiba haraka?

Mwone mtoa huduma ya afya kama:

 • Umepata dalili kali za mzio.
 • Matibabu ya kudhibiti allergy hayafanyi kazi tena

Uchaguzi wa matibabu

Athari kali za mzio (anaphylaxis), zinahitaji kutibiwa na dawa inayoitwa epinephrine, dawa hii huokoa maisha ikitolewa mara moja baada ya ”reaction”.

Njia bora ya kupunguza dalili ni kujaribu kuepuka kizio kinachosababisha tatizo hili. Hii ni muhimu hasa kwa mzio unaosababishwa na chakula au dawa.

Kuna aina kadhaa za dawa zinazokinga na kutibu mzio. Kulingana na aina ya uliyonayo, makali ya dalili ,umri na afya yako kwa ujumla, daktari atapendekeza dawa mojawapo.

Magonjwa maalum yanayosababishwa na mzio (kama pumu, kikohozi/mafua yaletwayo na vumbi (hay fever), na Ukurutu (eczema)) yanaweza kuhitaji matibabu mengine.

Madawa yanayoweza kutumika kutibu mizio ni pamoja na:

ANTIHISTAMINES

Antihistamines zinapatikana kwenye maduka ya dawa,katika hali nyingi, ikiwa ni pamoja na:

 • Vidonge na dawa
 • Matone ya jicho
 • Sindano
 • Dawa ya kunywa
 • Dawa ya kupuliza puani

CORTICOSTEROIDS

Dawa hizi hupunguza uchochezi unaosababisha kuvimba, zinapatikana katika aina nyingi, ikiwa ni pamoja na:

 • Creams na mafuta ya kujipaka kwenye ngozi
 • Matone ya jicho
 • Dawa ya kupuliza puani
 • Dawa za kuvuta kwa inhaler

Wagonjwa wenye dalili kali za tatizo hili wanaweza kupewa dawa za kumeza za corticosteroid au sindano kwa muda mfupi.

DECONGESTANTS

Decongestants zinaweza kupunguza kuziba kwa pua. Dawa za kupuliza puani  hazipaswi kutumiwa kwa zaidi ya siku kadhaa , kwa sababu zikitumiwa kwa muda  mrefu zinaweza kusababisha athari mbaya (rebound effect ) na kusababisha tatizo kuwa baya zaidi. Decongestants za vidonge hazina tatizo hili.

MADAWA MENGINE

Leukotriene inhibitors ni madawa ambayo huzuia vitu vinachochochea kutokea kwa shida hii.  Zafirlukast na montelukast zinatumika kwa wale walio na pumu na mizio ya ndani na nje ya nyumba.

Kuzuia

Kunyonyesha watoto maziwa ya mama pekee kwa kipindi kisichopungua miezi minne husaidia kuzuia ukurutu, mzio wa maziwa ya ng’ombe na kukorota utotoni.

Hata hivyo, kubadili mlo wa mama wakati wa ujauzito au wakati wa kunyonyesha hakusaidii kuzuia kutokea kwa shida hii au hali zinazohusiana na mzio.

Kwa watoto wengi, kubadilisha chakula au kutumia ”formula” maalum havionekani kuzuia matatizo haya. Kama kuna historia ya ukurutu katika familia na mzio kwa mzazi, kaka au dada, jadiliana na daktari wako kuhusu lishe. Muda wa kuanzishwa vyakula vigumu, pamoja na matumizi ya vyakula kadhaa maalum, inaweza kusaidia kuzuia mzio fulani.

Pia kuna ushahidi kwamba watoto wachanga wanaokua katika mazingira yenye vizio vingi kwenye hewa (kama vile vumbi na manyoya ya paka) huwa na uwezekano mdogo wa kupata allergy. Hii inaitwa “hygiene hypothesis “. watoto wanaokulia mashambani hupata allergy mara chache sana ulinganisha na wale waliokulia mazingira masafi.

Mara baada ya kutokea kwake, kutibu mzio na kuepuka vitu vinavyosababisha reaction inaweza kuzuia tatizo katika siku zijazo.

Nini cha kutarajia?

Aina nyingi hutibiwa kiurahisi tu kwa dawa. Watoto wengine wanapokuwa na shida hii hupona. Hii ni kweli hasa kwa mzio wa chakula. Hata hivyo mara nyingi, kitu kinaposababisha mzio kwa mtu ,k itaendelea kufanya hivyo siku zote.

Matatizo yanayoweza kutokea

 • Anaphylaxis (hii ni aina kali sana inayoweza kutishia maisha).
 • Matatizo ya kupumua na wasiwasi wakati wa mjibizo wa mzio (allergic rection ).
 • Kusinzia sinzia na madhara mengine ya madawa.

Vyanzo

http://www.nlm.nih.gov/medlineplus/ency/article/000812.htm

 • Share:

Leave Your Comment