MZUNGUKO WA KIUNO:Njia ya kutathmini uzito wa mwili

Mzunguko wa kiuno

Kipimo kingine kinachoweza kuonesha kama mtu ana uzito uliozidi na kumuweka katika uwezekano mkubwa wa kupata magonjwa sugu yasiyo ya kuambukiza ni kipimo cha mzunguko wa kiuno. Kipimo hiki husaidia kuonyesha kiasi cha mafuta kilichohifadhiwa tumboni. Mafuta yanapohifadhiwa kwa wingi sehemu ambazo ni karibu na moyo ni hatari zaidi kuliko yanapohifadhiwa sehemu nyingine za mwili.

Mzunguko wa kiuno hupimwa kwa kuzungusha futi kamba kupitia mfupa wa nyonga kwa kufuata hatua zifuatazo: ­mzunguko wa kiuno

  • Kwa usahihi wa vipimo ni vyema usijipime mwenyewe; ­
  • Mtu anayepimwa avue nguo ikiwa ni pamoja na zile zinazobana isipokuwa nguo nyepesi za ndani; ­
  • Mtu anayepimwa asimame akiwa amenyooka na miguu yake iwe pamoja na asiegemee upande mmoja; ­
  • Apumue kama kawaida na kipimo kichukuliwe akiwa anatoa pumzi. Hali hii huwezesha misuli ya tumbo kulegea na hivyo kuwezesha kupata vipimo sahihi; ­
  • Mpimaji asimame pembeni mwa mtu anayepimwa na azungushe futi kamba kwenye mfupa wa nyonga na kukutanisha futi kamba tumboni usawa wa kitovu. Utepe usibane wala usilegee; na ­
  • Kipimo kichukuliwe na kurekodiwa katika kadirio la karibu la sentimita 0.5.

Tafsiri ya vipimo kulingana na viwango vya rejea vya Shirika la Afya Duniani

  • Mwanamke: Mzunguko usizidi sentimita 88
  • Mwanamume: Mzunguko usizidi sentimita 102

Endapo mzunguko wa kiuno ni mkubwa kuliko viwango vilivyopendekezwa na WHO unapaswa kupewa ushauri kuhusu ulaji unaofaa na mtindo bora wa maisha.

Vyanzo

https://www.tfnc.go.tz/publications/9

Leave a Reply

Your email address will not be published.

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.

Jiunge Nasi