NAMNA YA KUPIMA KIMO NA UREFU WA MTOTO

Kupima kimo au urefu wa mtoto

Kupima kimo au urefu wa mtoto husaidia kutambua yafuatayo:

Kupima kimo au urefuMtoto wa umri chini ya miezi 24 hupimwa urefu akiwa amelala katika ubao wa kupimia urefu. Mtoto wa umri zaidi ya miezi 24 na watu wazima hupimwa kimo wakiwa wamesimama.

Kumbuka:  Kwa kuzingatia taratibu za Shirika la Afya Duniani; Iwapo mtoto ana umri chini ya miezi 24 na amepimwa kimo akiwa amesimama ni lazima kuongeza sentimita 0.7 katika kimo chake ili kupata urefu wake.

Iwapo mtoto ana umri wa miezi zaidi ya 24 na amepimwa urefu kwa kulala ni lazima kutoa sentimita 0.7 katika urefu wake ili kupata kimo chake

Kwa mujibu wa Shirika la Afya duniani (WHO) upimaji wa urefu wa watoto wenye umri chini ya miezi 24 hufanyika kwa kuzingatia taratibu zifuatazo;

 • Nawa mikono kwa maji safi na sabuni kabla na baada ya kumshika mtoto au mazingira wanayokaa. Endapo maji safi na sabuni hayapatikani, tumia dawa ya kuuwa vimelea vya magonjwa.
 • Mbembeleze mtoto atulie kama analia au anasumbua
 • Vua kofia, soksi, viatu na nguo nzito, kibanio cha nywele
 • Weka ubao wa kupimia urefu wa mtoto kwenye sehemu tambarare na isiyobonyea lakini mbali na kingo
 • Mtoto alazwe katikati ya kibao na kichwa kielekezwe mbele ya ubao
 • Mkao wa kichwa: Shikilia kichwa cha mtoto sehemu za masikio, hakikisha shingo imenyooka na msaidizi au mama amshike mtoto ipasavyo.
 • Mkao wa mwili na miguu: Hakikisha mtoto anakaa katikati ya ubao, nyoosha magoti yake taratibu huku umeyashikilia na hakikisha yamenyooka bila ya kulazimisha
 • Hakikisha nyayo za mtoto zimenyooka na zinagusa kibao cha kupimia
 • Soma na kuandika urefu wa mtoto katika desimali ya karibu ya sentimita 0.1

Kwa watu wazima au watoto wenye umri wa zaidi ya miezi 24, tunatumia ubao wa kupima kimo au kifaa cha kupima kimo na uzito. Ni muhimu ubao huo ukawekwa sehemu sahihi isiyo na mabonde, iliyonyooka na ya utulivu kama vile ukutani. Soma na kuandika kimo kwa desimali ya karibu ya sentimeta 0.1. Kwa mujibu wa Shirika la Afya Duniani (WHO)

upimaji wa kimo cha watoto wenye umri zaidi ya miezi 24 hufanyika kwa kuzingatia taratibu zifuatazo;

 • Nawa mikono kwa maji safi na sabuni kabla na baada ya kumshika mtoto au mazingira wanayokaa. Endapo maji safi na sabuni hayapatikani tumia dawa ya kuuwa vimelea vya magonjwa
 • Mbembeleze mtoto atulie kama analia au anasumbua
 • Mpunguzie mtoto soksi, nguo nzito, kofia, viatu au vitu vyovyote ambavyo vinaweza kuleta kikwazo katika kupima
 • Hakikisha mtoto anasimama katikati ya sehemu ya ubao wa kupima kimo ambayo haina kikwazo,
 • Miguu imenyooka na imetenganishwa sawa kati ya mguu mmoja na mwingine.
 • Makalio, Mabega na visigino vya mtoto viguse ubao.
 • Weka kichwa cha mtoto katika mstari ulionyooka huku akitazama mbele
 • Mwelekeze asimame akiwa amenyooka, nyoosha magoti yake taratibu ili miguu inyooke
 • Soma na kuandika kimo cha mtoto kwa desimali ya karibu ya sentimeta 0.1

Tafsiri: ili kutafsri matokeo ya kupima urefu; unahitaji kulinganisha urefu na umri wa mtoto ili kuona kama ni sahihi – Jedwali la kulinganisha bado linaandaliwa, litakuwepo baada ya siku 2

Vyanzo

https://www.tfnc.go.tz/publications/9

Leave a Reply

Your email address will not be published.

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.

Jiunge Nasi