Last Updated on October 13, 2023 by Dr Mniko
Kupima uzito wa mtoto
Shirika la Afya Duniani linashauri kupima uzito wa mtoto kwa kutumia mizani yenye sifa zifuatazo:
- Mizani iliyo imara
- Mizani ya kidigitali
- Kukadiria uzito wa kilo kwa nukta 0.1 (gramu 100)
- Kupima mtoto na mama kwa pamoja kama mtoto hawezi kusimama.
Mizani mingine inayotumika kupimia uzito kwa watoto ni:
- Mizani ya kupimia uzito watoto wachanga: Mizani hii hufaa kupima watoto wakiwa wamelala au wamekaa, lakini kwa kuzingatia uzito wa juu ambao mzani unaweza kupima
- Mzani wa kuning’iniza: Maranyingi mzani huu hutumika katika jamiii au katika mazingira ya dharura kupimia watoto wadogo. Mzani huu huweza kupima mpaka kilo 25.
- Mzani wa kupima uzito wa watoto kwa kutumia mawe maalumu: Mzani huu huweza kupima uzito wa watoto kwa usahihi. Pia ipo mizani ya aina hii ambayo huweza kupima mpaka uzito wa kilo 65.
- Mzani wa kupima watoto kwa kusimama: Mzani huu hutumika kupimia uzito wa watoto ambao wanaweza kusimama wenyewe bila usaidizi
Kupima uzito wa mtoto mwenye umri chini ya miezi 24
Mzani wa watoto wachanga wa kulala
Kwa mujibu wa Shirika la Afya duniani (WHO) upimaji wa uzito wa watoto wenye umri chini ya miezi 24 hufanyika kwa kuzingatia taratibu zifuatazo:
- Nawa mikono kwa maji safi na sabuni kabla na baada ya kumshika mtoto au mazingira wanayokaa. Endapo maji safi na sabuni hayapatikani, tumia dawa ya kuua vimelea vya magonjwa
- Mvue nepi na nguo nzito: Inashauriwa avuliwe nguo zote kama hali ya hewa inaruhusu na inakubalika katika jamii
- Mbembeleze mtoto atulie kama analia au anasumbua
- Weka mzani sehemu ngumu isiyo na mwinuko au kizuizi
- Rekebisha mzani usomeke sifuri
- Mlaze mtoto kwenye mzani akiwa amelalia mgongo uso ukitizama juu. Kaa karibu na mtoto huku mkitazamana
- Soma uzito wa mtoto na andika kipimo kwa desimali ya karibu ya kilogramu 0.1 (Gramu 100).
- Mizani ya kuning’inia
Mzani wa kuninginia
Kwa mujibu wa Shirika la Afya duniani (WHO) upimaji wa uzito wa watoto wenye umri chini ya miezi 24 kwa kutumia mzani wa kuning’inia hufanyika kwa kuzingatia taratibu zifuatazo:
- Nawa mikono kwa maji safi na sabuni kabla na baada ya kumshika mtoto au mazingira wanayokaa. Endapo maji safi na sabuni hayapatikani, tumia dawa ya kuuwa vimelea vya magonjwa
- Rekebisha mshale wa mzani usomeke sifuri
- Ning’iniza mzani kwa kutumia ndoano, mzani uwe katika usawa wa macho yako (isiwe juu au chini).
- Rekebisha mzani usomeke sifuri
- Mvue nepi na nguo nzito (inashauriwa avuliwe nguo zote kama hali ya hewa inaruhusu na inakubarika katika jamii
- Mvalishe kaptula maalumu ya kupimia kisha mning’inize kwenye mzani
- Hakikisha mtoto ananing’inia mwenyewe bila kushika kitu chochote
- Soma uzito wa mtoto akiwa ametulia na kadiria uzito katika desimali ya karibu ya kilo 0.1 (Gramu 100)
- Baada ya kuchukua vipimo mtoe taratibu na kwa uangalifu ili asiumie
Mzani wa kusimama
Kwa mujibu wa Shirika la Afya duniani (WHO) upimaji wa uzito wa watoto wenye umri zaidi ya miezi 24 kwa kutumia mzani wa kusimama hufanyika kwa kuzingatia taratibu zifuatazo:
- Nawa mikono kwa maji safi na sabuni kabla na baada ya kumshika mtoto au mazingira wanayokaa. Endapo maji safi na sabuni hayapatikani, tumia dawa ya kuuwa vimelea vya magonjwa
- Mvue nguo nzito na viatu (inashauriwa avuliwe nguo zote kama hali ya hewa inaruhusu na inakubalika katika jamii)
- Mbembeleze atulie kama analia au anasumbua
- Weka mzani mahali pagumu pasipo na mwinuko au kizuizi
- Rekebisha mzani usomeke sifuri
- Mwelekeze jinsi ya kusimama katikati ya mzani
- Mtoto asishike kitu chochote au kumshika mtu yeyote
- Soma uzito wa mtoto na andika kipimo kwa desimali ya karibu ya kilogramu 0.1 (Gramu 100).
Leave feedback about this