NDOTO ZA KUTISHA: Ni nini cha kufanya

Maelezo ya jumla

Ndoto za kutisha ni ndoto zinazotokea ukiwa umelalal zinazoamsha hisia kali za hofu, woga, msongo na za kutisha. Ndoto za kutisha mara nyingi hutokea wakati wa sehemu ya pili ya usiku na kusababisha aliyelala kuamka, na anaweza kukumbuka alichoota.

Nini sababu ya ndoto za kutisha?ndoto za kutisha

Zifuatazo ni sababu ya ndoto za kutisha:

 • Woga uliopitiliza na msongo ndio sababu zilizozoeleka zaidi
 • Kunakuwepo na tukio kubwa na gumu lililomtokea mgonjwa kabla ya ndoto za kutisha kuanza.

Sababu nyingine za ndoto za kutisha ni pamoja na:

 • Kuacha ulevi wa pombe ghafla
 • Kuwa na tatizo la kuacha kupumua ukiwa usingizini – sleep apnea
 • Kifo cha mtu unayempenda (kuomboleza)
 • Kunywa kiasi kikubwa cha pombe
 • Kuwa na ugonjwa unaosababisha homa
 • Kuacha kutumia ghafla kutumia dawa /dawa za kulevya, kama vile dawa za kuleta usingizi
 • Madhara mabaya ya dawa
 • Matatizo ya usingizi (kwa mfano, tatizo la usingizi ono “narcolepsy” au matatizo mengine ya usingizi)
 • Kula muda mfupi kabla ya kulala, hii inasababisha kiwango cha uchakataji “metabolism” na shughuli ya ubongo kuongezeka

Mambo ya kuzingatia kama una ndoto za kutisha

 • Ndoto za kutisha mara nyingi zinawapata zaidi watoto na kupungua kadri unavyokua mtu mzima
 • Karibi 50% ya watu wazima wanapata ndoto za kutisha kwa wakti mmoja au mwingine, wanawake wanapata zaidi ndoto za kutsha kuliko wanaume.

Ni wakati gani unapaswa kutafuta msaada wa kitabibu?

Ongea na daktari kama:

 • Una pata ndoto za kutisha zaidi ya mara moja kwa wiki
 • Kama ndoto za kutisha zinakuzuia kupumzika vizuri usiku, au kama zinasababisha unashindwa kutekeleza majukumu yako ya kila siku

Utambuzi wa ndoto za kutisha

Daktari atakufanyia uchunguzi na kukuuliza maswali, na yawezekana akaagiza ufanye vipimo. Unaweza kuulizwa maswali yafuatayo:

 • Mwenendo wa ndoto za kutisha
  • Unapata ndoto za kuisha mara kwa mara
  • Unapata ndoto hizi wakati wa sehemu ya pili ya usiku?
 • Ubora: Je unaamka ghafla kutoka usingizini
 • Matatizo mengine:
  • Je ndoto hizi za kutisha zinakusababishia hofu na woga kupita kiasi?
  • Je unakumbuka ndoto hizi zinahusu nini (kumbuka moja yenye picha na hadithi)?
 • Mambo yanayosababisha au yanayochangia kutokea kwake:
  • Je, umepatwa na ugonjwa wowote hivi karibuni?
  • Je, umepata homa kali?
  • Je, umekuwa katika hali iliyokusababishia msongo hivi karibuni?
 • Mambo mengine unayoweza kuulizwa:
  • Je, Unatumia sana pombe? Kiasi gani?
  • Je, Unatumia dawa gani?
  • Je, Unatumia dawa za kulevya? Kama ndio, ni zipi?
  • Je, unatumia dawa za asili?
  • Je, Una dalili nyingine zozote?
 • Vipimo vinavyoweza kufanyika ni pamoja na:
  • Kupima kiwango cha seli za damu
  • Kupima ini kuona kama linafanya kazi
  • Kupima tezi dundumio (tezi ya shingo kuna kama inafanya kazi
  • Kipimo cha EEG (Kipimo hiki husaidia kupima mawimbi ya umeme yanayopita kwenye ubongo ukiwa umelala) – kipimo hiki hakisababishi maumivu yoyote – vidaka umeme “electrodes” huwekwa kwenye kichwa tayari kwa kipimo.

Uchaguzi wa matibabu ya ndoto za kutisha

 • Kama una msongo mkubwa wa mawazo, omba msaada kwa maafiki au ndugu. Kuzungumza kinachokusumbua kunaweza kusaidia.
 • Fanya mazoezi. Utajikuta unapata usingizi haraka, unapata usingizi mzito, na kuamka ukijihisi kupumzika kabisa.
 • Jifunze njia za kupunguza mkazo wa misuli (njia za kulegeza misuli “relaxation therapy”), hii inaweza kusaidia kupunguza msongo
 • Kuwa na mpango mzuri wa kulala. Lala wakati uleule kila usiku, na amka wakati ule ule kila asubuhi. Epuka kutumia dawa za usingizi kwa muda mrefu, acha pia kutumia kahawa na viamsha mwili vingine.
 • Kwa ndoto za kutisha zinzosababishwa na dawa za kulevya au utumizi wa pombe, ongea na daktari ili kupata njia bora zaidi ya kuacha.

Vyanzo

Leave a Reply

Your email address will not be published.

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.

Jiunge Nasi