Kupunguza au kudhibiti uzito ni nini?
Ili kusema umeweza kudhibiti uzito wako wa mwili, ni lazima uwe umeweza kupunguza uzito kwa angalau 10% na kubaki bila kuongezeka kwa angalau mwaka mzima.
Ni ipi njia nzuri ya kudhibiti uzito?
Sio rahisi kudhibiti uzito wa mwili. Unaweza kupunguza uzito na kudhibiti usiongezeke tena kwa kufanya mambo yafuyatayo:
- Dhibiti kiwango cha chakula unachokula kila siku
- Fuatilia kiwango cha kalori na mafuta unachokula kila siku
- Dhibiti au punguza ulaji wa vyakula vyenye kiwango kikubwa cha mafuta na sukari
- Panga unachopaswa kula mapema
- Kula kifungua kichwa kila siku
- Ni vizuri kuhakikisha mlo wako unafanana (kiwango, muda wa kula n.k)
- Kula sawa siku za wikiendi sawa na siku za wiki
- Usibadili ulaji unapokuwa mapumziko, likizo au sherehe
- Ongeza kiwango cha mazoezi unachofanya
- Ongeza kiwango cha shughuli unazofanya
- Kupata angalau dakika 30 za mazoezi kila siku, inasaidia
- Ni vizuri kupima uzito wa mwili angalau mara 1 kwa wiki
- Usiangalaie TV kwa zaidi ya masaa 10 kwa wiki
Je, matumizi ya dawa za kupunguza uzito yanasaidia?
Ukiunganisha mazoezi na mlo wa afya na dawa za kupunguza uzito kama vile sibutramine na orlistat zinaweza kusaidia kudhibiti uzito kwa angalau miaka miwili. Kwa baadhi ya watu, kutumia dawa za kupunguza uzito husaidia sana kudhibiti uzito kuliko kufanya mazoezi na kula mlo sahihi pekee. Lakini kwa sababu za kiafya, watu wengi hawatakiwi kutumia dawa hizi kwa zaidi ya miaka miwili. Watu wengi wanaongezeka tena uzito baada tu ya kuacaha kutumia dawa za kupunguza uzito.
Vipi kuhusu upasuaji wa kupunguza uzito?
Upasuaji wa kupunguza na kudhibiti uzito unaanza kuwa wa kawaida katika nchi nyingi. Upasuaji unaweza kumsaidia mgonjwa kudhibiti uzito kwa muda mrefu. Lakini unapaswa kujua kuwa, mabadiliko ya mfumo wa Maisha (mazoezi, mlo n.k) yanaweza kutoa matokeo hayo hayo. Muulize daktari kama kufanya upasuaji ili kudhibiti uzito ni chaguo sahihi kwako.
Leave feedback about this