NJIA ZINAZOTUMIKA KUPIMA KAMA UNA KITAMBI

NJIA ZINAZOTUMIKA KUPIMA KAMA UNA KITAMBI

 • November 17, 2020
 • 0 pendwa
 • 9 Wameona
 • 0 Maoni

Maelezo ya jumla

Kuchunguza kama una kitambi kunashauriwa kwa watoto wenye umri zaidi ya miaka sita, na angalau mara moja kwa mwaka kwa watu wazima. Njia kuu za kupima kama una kitambi ni pamoja na kupima Body mass index (BMI), kupima mzunguko wa kiuno, na kupima kiwango cha mafuta mwilini.

Body mass index (BMI)

Uchunguzi wa kitambi unapaswa kufanyika angalau mara moja kwa mwaka kwa watu wazima.

Body mass index ni hesabu za kihisabati ambazo hufanyika ili kutathmini hatari za kiafya zinazohusiana na uzito wa mwili. Tafiti mbalimbali zimeonesha kuwa uzito wa mwili chini au juu ya kiwango fulani huongeza hatari ya kupata matatizo ya kiafya kama magonjwa ya moyo, kisukari na hata kansa.

Body mass Index hutoa uwakilishi wa kiasi cha mafuta yaliyomo mwilini, kadri kiasi cha mafuta kinapoongezeka mwilini, ndivyo na  hatari za kiafya zinavyoongezeka. Wataalamu wa afya wanajua kuwa, kuongezeka uzito wa mwili unaosababishwa na mafuta mengi mwilini, ndio sababu kuu ya magonjwa ya moyo.

Wanaume na wanawake wenye urefu na uzito sawa wana BMI sawa.

BMI =

 • BMI inayokubalika kiafya na jumuiya ya kitabibu ni kati ya 5 hadi 24.9. Kiwango hiki kinawakilisha uwiano kati ya uzito na urefu ambao haukuweki katika hatari ya kupata madhara kiafya.
 • BMI chini ya 5 inaonyesha kuwa uko katika hatari kubwa ya kupata matatizo ya kiafya yanayosababishwa na uzito mdogo sana (underweight).
 • BMI kuanzia 25 hadi 9 inaashiria kuwa uzito wako ni mkubwa kwa 10-15% zaidi ya kiwango kinachokubalika, na kwa sababu hiyo uwezekano wa kupata shinikizo la juu la damu huongezeka mara mbili zaidi.
 • BMI zaidi ya 30 huonyesha uzito wa mwili ambao ni 20% zaidi ya uzito wa kawaida. Uwezekano wa kupata magonjwa ya moyo, huongezeka mara 2-6 kwa mtu mwenye kiwango hiki cha BMI.
 • BMI zaidi ya 35 , Mtu mwenye kiwango hiki cha BMI mara nyingi atakuwa na matatizo ya kiafya yanayohusiana na uzito tayari. Matatizo hayo ni pamoja na Shinikizo la juu la damu, magonjwa ya mishipa ya moyo na kushindwa kwa moyo.
1.BMI [Kg/m2 ] MATOKEO USHAURI
18.5 mpaka 24.9 Uzito wako ni wa kawaida Una hali njema, endelea kujitunza ili usiongezeke uzito
25 mpaka 29.9

 

Uzito wako ni mkubwa

 

Haupaswi kuongezeka uzito. Unapaswa kupunguza uzito hasa kama una hatari zinazoongeza uwezekano wa kupata magonjwa ya moyo
Zaidi ya 30 Una kitambi Unapaswa kupunguza uzito. Punguza uzito taratibu. Mwone daktari kwa msaada Zaidi kuhusu kupunguza uzito

 

Mzunguko wa kiuno

BMI haizingatii uwiano na utofauti wa mafuta katika sehemu mbalimbali za mwili. Mafuta yanayojaa sehemu ya tumbo na kusababisha kitambi cha tumbo, huhusanishwa kwa ukaribu zaidi na magonjwa ya moyo kuliko ilivyo kwa mafuta mengine yanayojaa sehemu zingine za mwili na kusababisha mtu kuwa mnene. BMI  haiwezi kutofautisha hili.

 • Mzunguko wa kiuno zaidi ya 102 sm kwa wanaume na zaidi ya 88 sm kwa wanawake humaanisha kuwa una kitambi

au

 • Uwiano wa kiuno- nyonga wa zaidi ya 9 kwa wanaume na zaidi ya 0.85 kwa wanawake humaanisha una kitambi

Upimaji wa mafuta ya Mwili

Njia mbadala ya kutambua kama una kitambi ni kupima asilimia ya mafuta mwilini. Madaktari na wanasayansi kwa ujumla wanakubaliana kuwa wanaume wenye mafuta zaidi ya 25% ya mwili na wanawake wenye mafuta zaidi ya 30% wana kitambi.  Hata hivyo, ni vigumu kupima mafuta ya mwili kwa usahihi. Njia inayokubaliwa zaidi ni ile ya kupima uzito wa mtu akiwa ndani ya maji, lakini njia hii hufanyika tu kwenye maabara zenye vifaa maalumu.

Njia nyingine ya kupima asilimia za mafuta mwilini, ni ile ya kukata kipande kidogo cha ngozi na kupima kiasi cha mafuta yaliyo kwenye safu ya ngozi. Matumizi ya njia hizi hayashauriwi sana.

 • Shirikisha:

Leave Your Comment