Sera ya faragha

Sera hii ya faragha ilihaririwa kwa mara ya mwisho 6 januari 2022 kama kutakuwa na marekebisho au mabadiliko yeyote kwenye sera yetu ya faragha, mabadiliko hayo yatachapishwa kwenye ukurasa huu

Taarifa binafsi

Kwa sababu tunaamini kwamba haipaswi kutoa taarifa binafsi ili kushiriki katika harakati huru za kutoa na kupokea habari/ujuzi, unaweza:

 • Kusoma makala yoyote toka WikiElimu bila kusajili akaunti.
 • Unaweza kuhariri,kutengeneza kurasa au kuandika makala katika tovuti ya WikiElimu baada ya kujisajili, kuhakikiwa na kuwa na akaunti ya kutumia username.

Kwa sababu tunataka kuelewa jinsi Tovuti ya WikiElimu inavyotumika, ili tuweze kuifanya iwe bora kwako, tunakusanya taarifa kadhaa kadhaa wakati:

 • Unapochangia katika maada iliyo wazi kwa umma.
 • Unaposajili akaunti au unaposahihisha ukurasa wako wa mtumiaji.
 • Unapotumia tovuti ya WikiElimu.
 • Unapotutumia barua pepe au unaposhiriki katika utafiti au kutoa maoni.

Tumedhamiria:

 • Kukueleza jinsi habari zako zinavyoweza kutumika au kushirikishwa katika Sera hii ya faragha.
 • Kuchukua hatua madhubuti ili kuweka habari/taarifa zako binafsi salama.
 • Hatutauza taarifa zako binafsiau kuzigawa/kushirikisha/kuzitoa kwa watu/kampuni/yeyote kwa madhumuni ya kupata faida.
 • Tutatoa taarifa/habari zako binafsi kwa kiasi kinachokubalika pale tu mazingira yatakaporuhusu, kama vile kusaidia kuboresha tovuti ya WikiElimu, kufuata sheria, au kukulinda wewe na wengine.
 • Kutunza data zako kwa muda mfupi iwezekanavyo ambayo ni sawa na muda unaotosha kukarabati, kuelewa, na kuboresha tovuti ya WikiElimu, na kutekeleza majukumu yetu chini ya sheria.Jihadhari:
 • Maoni yoyote unayoongeza au mabadiliko yoyote unayofanya kwenye tovuti ya WikiElimu yatakuwa wazi na ya kudumu kwa umma wote kuona.
 • Ukiongeza maudhui, maoni au kufanya mabadiliko kwenye tovuti ya WikiElimu bila kuingia kwenye akaunti, maudhui au mabadiliko yatawasilishwa kwa umma kwa anwani ya IP iliyotumiwa wakati huo badala ya jina la mtumiaji.
 • Jumuiya yetu ya wahariri wa kujitolea na wafadhili ni kundi linalojitegemea. Watawala ‘admin’ fulani wa WikiElimu, waliochaguliwa, hutumia zana ambazo huwapa upendeleo kidogo, ili kuweza kutambua na kufuatilia mabadiliko yoyote yanayofanyika katika tovuti,watawala hawa huilinda tovuti na kusaidia kutiisha utekelezaji wa sera.
 • Kwa ajili ya ulinzi wa WikiElimu na watumiaji wengine, ikiwa hukubaliana na Sera hii ya Faragha, tafadhali usitumie tovuti ya WikiElimu

Jiunge Nasi