Utoaji wa chanjo zaidi ya moja kwenye kila hudhurio
- Katika ratiba ya chanjo Tanzania watoto hupata chanjo zaidi ya moja wakati wa hudhurio inauhusu mtoto kupata kinga kamili haraka iwezekanavyo. Hii hutoa ulinzi wakati wa miezi ya kwanza ya hatari ya maisha ya mtoto. Kwa kupata chanjo zaidi ya moja kwa kila hudhurio humpunguzia mzazi/mlezi mahudhurio ya mara kwa mara katika kituo cha huduma.
- Ni salama kwa mtoto kupokea chanjo za sindano zaidi ya moja kwa wakati mmoja.
Umuhimu wa kuchanja
- Chanjo huokoa maisha ya mtoto kwa kumkinga dhidi ya maradhi ambayo yanazuilika kwa chanjo
- Tafiti mbalimbali zilizofanywa na wataalamu wa afya duniani zimeonesha kwamba chanjo ni salama
- Jamii iliyopata chanjo huwa imekingwa dhidi ya milipuko ya magonjwa kama vile Surua
- Chanjo huokoa muda na gharama ambazo zingetumika na mgonjwa/mzazi au mlezi pindi anapopata maradhi ambayo yangeweza kuzuilika hapo awali
- Chanjo hulinda pia kizazi kijacho dhidi ya magonjwa yanayozuilika kwa chanjo kwani baadhi ya magonjwa yameweza kutokomezwa kama ilivyotokomezwa ndui (small pox)
Je, mtoto wako amekamilisha chanjo?
- Kufuata ratiba ya chanjo Tanzania kwa watoto ni muhimu, mpeleke mtoto katika kituo cha kutolea huduma kwa kuzingatia ratiba ili aweze kupewa chanjo zote zinazostahili ikiwemo chanjo ya IPV
- Chunguza kadi ya chanjo au muulize mhudumu wa afya ili kufahamu kama mtoto amekamilishachanjo zote kulingana ratiba ya chanjo Tanzania kwa watoto
- Chanjo ni haki ya kila mtoto, mteja au mlengwa mpeleke mwanao/nenda kwenye kituo cha huduma za afya akapate chanjo
Ratiba ya chanjo
UMRI WA KUTOLEWA | AINA YA CHANJO | NJIA | KIWANGO |
Mara baada ya kuzaliwa | BCG | Ndani ya ngozi, Bega la kulia | 0.05mls |
OPV 0 | Mdomoni | Matone mawili | |
Wiki 6 | OPV1 | Mdomoni | Matone mawili |
Pentavalent 1 | Ndani ya msuli, paja la kushoto (nje) | 0.5mls | |
PCV 1 | Ndani ya msuli, paja la kulia (nje) | 0.5mls | |
Rota 1 | Mdomoni | 1.5mls | |
Wiki 10 | OPV2 | Mdomoni | Matone mawili |
Pentavalent 2 | Ndani ya msuli, paja la kushoto (nje) | 0.5mls | |
PCV 2 | Ndani ya msuli, paja la kulia (nje) | 0.5mls | |
Rota 2 | Mdomoni | 1.5mls | |
Wiki 14 | OPV3 | Mdomoni | Matone mawili |
Pentavalent 3 | Ndani ya msuli, paja la kushoto (nje) | 0.5mls | |
PCV 3 | Ndani ya msuli, paja la kulia (nje) | 0.5mls | |
IPV | Ndani ya msuli, paja la kulia (nje) | 0.5mls | |
Miezi 9 | MR 1 | Chini ya ngozi, mkono wa kushoto (nje) | 0.5mls |
Miezi 18 | MR 2 | Chini ya ngozi, mkono wa kushoto (nje) | 0.5mls |
Miaka 9 | HPV 1 | Ndani ya msuli, mkono wa kushoto (nje) | 0.5mls |
Miezi 6 baada ya HPV1 | HPV2 | Ndani ya msuli, mkono wa kushoto (nje) | 0.5mls |
Vyanzo
Imetoholewa kutoka katika kipeperushi kilichotayarishwa na wizara ya afya , maendeleo ya jamii, jinsia , watoto na wazee
Leave feedback about this