Saratani ya koo (umio) ni nini?
Saratani ya koo (umio) ni saratani inayotokea kwenye bomba linalounganisha mdomo na tumbo linaloitwa umio. Chakula kinapitia kwenye koo na umio kabla ya kuingia tumboni.
Ni zipi dalili za kansa ya koo (umio)?
Dalili ni pamoja na maumivu wakati wa kumeza chakula. Chakula kinaweza kukwama na kushindwa kufika tumboni. Unaweza kupungua uzito wa mwili. Unaweza kuwa na kiungulia hata kama unatumia dawa za kupunguza aside tumboni.
Unaitambuaje saratani ya koo (umio)?
Saratani ya koo inatambuliwa kwa kuingiza kamera ndogo kupitia mdomoni mpaka kwenye umio – hii inaitwa endoscopy. Hii inaweza kuchukua dakika 15. Utapewa dawa ya nusu kaputi ili usinzie kabisa. Kama kansa itagunduliwa, utahitaji vipimo Zaidi ili kutambua kama saratani imesambaa zaidi.
Saratani ya koo (umio) inatibiwaje?
Matibabu yanategemea kama saratani imekwisha kusambaa. Kama haijasambaa kutoka kwenye koo/umio – upasuaji ni matibabu yanayopendelewa zaidi. Kama imekwisha kusambaa, lakini haijaenda mbali – mchanganyiko wa upasuaji, tiba kemikali na tiba mionzi huhitajika. Kama imesambaa kuelekea sehemu nyingine za mwili, mara nyingi inakuwa ngumu kutibu aina hii ya kansa. Lakini daktari atakupatia matibabu ili kupunguza maumivu na kukusaidia uishi vyema maisha yako yaliyobakia.
Leave feedback about this