Magonjwa ya wanaume

SARATANI YA KORODANI :Sababu, dalili, matibabu

Saratani ya korodani na inampata nani?

Saratani ya korodani ni saratani inayoanzia kwenye moja au korodani zote. Korodani zinakaa ndani ya mifuko inayoitwa pumbu.

Saratani ya korodani inawapata zaidi wanaume wenye miaka 20 mpaka 35. Uko kwenye hatari zaidi ya kupata saratani ya korodani kama kuna mtu kwenye familia yako mwenye shida hii au kama uliwahi kufanyiwa upasuaji ili kuweka sawa korodani zako ukiwa mtoto.saratani ya korodoni

Nitajuaje kama nina kansa ya korodani?

Mwone daktari kama una maumivu kwenye korodani moja au zote, kama una uvimbe kwenye pumbu, au kama unaona pumbu zimekuwa nyekundu au zimevimba.

Daktari atakuuliza kuhusu dalili na kuchunguza pumbu na korodani kama zina uvimbe. Kama una uvimbe, unaweza kuhitaji vipimo zaidi ili kuhakiki kama una kansa

Saratani ya korodani inatibiwaje?

Unaweza kuhitaji upasuaji ili kuondoa korodani zenye saratani. Kama saratani imesambaa kuelekea maeneo mengine ya mwili, unaweza kuhitaji kufanyiwa uchunguzi kila mwenzi, tiba mionzi, tiba kemikali, au kufanyiwa upasuaji zaidi.

Upasuaji ni njia bora zaidi kama saratani imegundulika mapema kabla haijasambaa. Hata kama saratani imesambaa, kuna uwezekano mkubwa kuwa utapona.saratani ya korodani

Nifanye nini baada ya kupata matibabu ya saratani ya korodani?

Mwanzoni utahitaji kumwona daktari kila mwezi kwa uchunguzi. Baadae utahitaji kufanyiwa uchunguzi mara moja tu kwa mwaka.

Unapaswa pia kujichunguza mwenye kila mwezi. Ili kujichunguza mwenyewe, weka dole gumba juu ya korodani na kidole cha chanda na cha kwanza kwa chini. Zungusha korodani katikati ya gumba na vidole mara kadhaa. Rudia pia kwenye korodani nyingine.

Mwone daktari kama utapata uvimbe, ugumu, au mabadiliko mengine kwenye korodani.

Vyanzo

https://medlineplus.gov/testicularcancer.html

Leave feedback about this

  • Quality
  • Price
  • Service

PROS

+
Add Field

CONS

+
Add Field
Choose Image
Choose Video
X