SARATANI YA MIFUPA: Sababu,dalili,matibabu

Saratani ya mifupa ni nini?

Saratani ya mifupa – Kuna aina nyingi ya saratani zinazoweza kusambaa kwenda kwenye mifupa. Lakini kuna aina tatu za kansa zinazoanzia kwenye mifupa; Osteosarcoma, Ewing sarcoma na Chondrosarcoma. Osteosarcoma na Ewing sarcoma zinawapata Zaidi Watoto na vijana wadogo. Chondrosarcoma inawapata Zaidi watu wazima walio kwenye umri wa kati. Saratani hizi ni nadra kuzipata, lakini ni muhimu sana kuzitambua mapema kadri inavyowezekana ili kupata matibabu.

Dalili za saratani ya mifupa?

Dalili za mwanzo za saratani ya mifupa ni za kawaida na zinaweza kuchanganywa na dalili za matatizo mengine. Dalili zinazowapata watu wengi ni maumivu na uvimbe, hasa kwenye mifupa mirefu ya miguu na mikono au karibu ya mifupa ya nyonga. Maumivu yanaweza kuanza baada ya kuumia kidogo tu kwenye michezo au baada ya kuanguka. Homa, maumivu wakati wa usiku, au maumivu yanayosababisha kuchechemea yanaweza pia kuwa dalili ya saratani ya mifupa. Ni vizuri kumwona daktari kama una dalili hizi na una wasiwasi.

Daktari atajuaje nina saratani ya mifupa?

Daktari atachukua historia ya matibabu, atakuchunguza mwili na kuagiza ufanye kipimo cha eksirei. Anaweza pia kuagiza upige picha za computed tomography (CT) scan au magnetic resonance imaging (MRI) ili kuchunguza sehemu nyingine za mwili, hasa mapafu yako. Kama vipimo hivi vitaonesha kuwa una saratani, daktari atachukua nyama ndogo kutoka eneo hilo na kwenda kuipima maabara (biopsy)

Saratani ya mifupa inatibiwa vipi?

Watu wenye saratani ya mifupa wanatibiwa katika hospitali maalumu zenye uwezo wa kutoa matibabu hayo. Aina ya matibabu inategemea hali ya kiafya ya mgonjwa, aina ya sarani ya mifupa aliyonayo na kama imesambaa sana. Wewe na daktari mtazungumza na kukubaliana mpango sahihi wa matibabu unaokufaa. Matibabu ya kawaida wanayopewa wagonjwa wengi wa kansa ya mifupa ni:

  • Tiba kemikali – Haya ni madawa makali yanayoweza kuua, kuharibu na kupunguza seli za kansa. Tiba kemikali inatumika kutibu saratani ya mifupa na seli za kansa zinazosambaa kwenda kwenye mapafu au sehemu nyingine za mwili. Tiba kemikali mara nyingi inatolewa kabla na baada ya upasuaji wa kuondoa uvimbe wa kansa kwenye mifupa.
  • Upauaji – Hii ndiyo njia inayopendelewa zaidi kutibu saratani ya mifupa. Kwa kawaida upasuaji unafanyika baada ya tiba kemikali.

Tiba mionzi – Hii ni tiba inayotumia mionzi kuharibu seli za kansa. Inaweza kutumiwa kama mbadala kwa watu wenye Ewing sarcoma. Tiba ya mionzi haiwezi kutumika kutibu Osteosarcoma.

Nini hutokea baada ya matibabu ya kansa ya mifupa

Baada ya matibabu utahitajika kuonana na daktari mara kwa mara. Kama umefanyiwa upasuaji, unaweza kuhitaji mazoezi tiba. Daktari atazungumza na wewe ngapi na baada ya muda unapaswa kufanya kipimo cha eksirei na CT scan ili kuhakikisha kuwa kansa haijarejea tena.

Nini kitatokea kama saratani itarudi tena?

Wewe na daktari mtazungumza na kukubaliana mpango wa matibabu utakaofuata. Kuna uwezekano mkubwa kuwa utapata matibabu sawa sawa na uliyopata mwanzo.

Vyanzo

https://medlineplus.gov/bonecancer.html

Leave a Reply

Your email address will not be published.

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.

Jiunge Nasi