SARATANI YA TUMBO: Sababu, dalili, matibabu

Maelezo ya jumla

Saratani ya tumbo ni aina ya saratani za mfumo wa chakula zinazowapata zaidi watu katika maeneo kadhaa ya Asia kama vile Japan na China. Saratani ya tumbo ni aina ya saratani inayotokea kwenye tumbo. Tumbo huhusika na kupokea chakula, kutunza chakula na kusaidia kukivunjavunja na kisha kukimeng’enya. Ugonjwa huu unaanzia kwenye utando uteute wa tumbo. Dalili kwa kawaida hujumuisha maumivu ya tumbo, kupoteza hamu ya kula, kupungua kwa uzito wa mwili, kichefuchefu, kutapika n.k. Kama usipotibiwa, saratani inavamia zaidi kwenda kwenye misuli na viungo vilivyo karibu. Saratani inaweza kusambaa kwa kumeguka na kusafiri kwenye mishipa ya damu au mishipa ya limfu na kujipandikiza katika sehemu yoyote ya mwili. Kujipandikiza kwa seli za saratani katika kiungo kingine husababisha saratani kukua hapo.

Ni zipi dalili za saratani ya tumbo?saratani ya tumbo

Saratani ya tumbo inapoanza haina dalili. Saratani inapokua kubwa, mgonjwa anaweza kuona dalili moja au zaidi ya zifuatazo:

 • Dalili za tumbo
  • Maumivu ya tumbo – mwanzoni maumivu yanaweza kuwa juu au katikati mwa tumbo. Mara nyingi ni maumivu mepesi yanayoweza kuvumilika. Kadri saratani inavyoendelea kukua, maumivu yanaweza kuzidi kuongezeka.
  • Kupoteza hamu ya chakula – Baadhi ya wagonjwa wanaanza kukosa hamu ya chakula bila sababu ya msingi
  • Kichefuchfu na kutapika – Hii pia inasababisha na kuwepo uvimbe. Uvimbe huvuruga mfumo wa kawaida wa chakula kupita.
  • Kutapika damu – Kwa mara chache, unaweza kuvuja damu sana katika mfumo wa kumeng’enya chakula
  • Kujihisi tumbo limejaa – Hii ni kwa sababu uvimbe unaendelea kukua
  • Kuwahi kushiba chakula – kujihisi umeshiba japo umekula kidogo tu. Hii husababishwa na kupungua kwa nafasi kwenye tumbo kwa sababu uvimbe umekua mkubwa sana.
  • Uvimbe tumboni – Kwa kawaida, mwanzoni mwa ugonjwa uvimbe hauoekani. Kadri uvimbe unavyoendelea kukua unaweza kuuona
 • Dalili za mifumo mbalimbali ya mwili
  • Kudhoofika kwa afya kwa ujumla – Hii ni kwa sababu inachukua sehemu kubwa ya malighafi zinazoingia mwilini
  • Uchovu na kuchoka – hii ni kwa sababu, saratani inasababishwa kupungua kwa nguvu za mwili

Maambukizi au matatizo mengine ya afya yanaweza kusababisha pia dalili hizi. Ni daktari pekee anayeweza kutofautisha. Mtu mwenye dalili yoyote kati ya hizi, anapaswa kuongea na daktari ili tatizo litambuliwe na kupatiwa matibabu haraka.

Baadhi ya matatizo au magonjwa yenye dalil sawa na saratani ya tumbo ni pamoja na:

Ni nani yuko kwenye hatari zaidi ya kupata saratani ya tumbo?

Saratani ya tumbo inawapata zaidi wanaume walio na umri zaidi ya mika 40. Aina hii ya sartani inapatikana zaidi katika nchi ya Japn, Chile na Iceland

Tafiti zimeweza kugundua baadhi ya mambo yanayoweza kuongeza uwezekano wa kupata saratani ya tumbo. Katika miaka ya hivi karibuni, wanasayansi wametambua kuwa maambukizi ya bakteria aina Helicobacter pylori huchangia kwa kiasi kikubwa kutokea kwa kansa hii. Maambukizi ya bateria wa Helcobacter pylori hushirikiana pamoja na sababu nyingine kuongeza uwezekano maradufu.

 • Kuwa na maambukizi yahelcobacter pylori
 • Kuwa na kuvimba kwa utando ute unaofunika tumbo
 • Mwanaume
 • Kula chakula chenye chumvi, chakula kilichokaushwa kwa moshi
 • Kuvuta sigara
 • Kuwa na historia ya kuwa na mtu mwenye saratani ya tumbo katika familia

Ni wakati gani unapaswa kutafuta msaada wa kitabibu haraka?

Onana na daktari kama unaona una dalili za saratani ya tumbo. Kama una dalili zifuatazo, onana na daktari haraka inavyowezekana:

 • Maumivu makali sana ya tumbo – Sababu ya mtu mwenye saratani kuwa na maumivu makali sana ya tumbo, yawezekana ukuta wa tumbo umetoboka. Hii inaweza kutokana na saratani kuvamia ukuta na kuutoboa. Upasuaji unahitajika haraka ili kurekebisha.
 • Kutapika damu nyingi – Hii inatokana na kansa kuvamia mishipa ya damu iliyo kwenye ukuta wa tumbo. Kama itavuja nyingi, mgonjwa anaweza kupteza maisha.

Uchaguzi wa matibabuSaratani ya tumbo

Sio rahisi kuitambua saratani ya tumbo inapokuwa katika hatua za mwanzo. Matatizo mengine ya afya yanaweza kusababisha dalili sawa kama vile kujisikia vibaya tumboni au kuvurugika tumbo. Kama una dalili hizi, unapaswa kwenda kwa daktari mapema inavyowezekana. Daktari anaweza kuagiza ufanye vipimo vya maabara, vpimo vya picha na endoscopy. Pamoja na vipimo vingine, kipimo cha kuingiza kamera tumboni kuitia mdomoni – endoscopy – ndio muhimu zaidi katika utambuzi wa kansa.

 • Kipimo cha endoscopy na kuchukua sampuli – Ni kipimo kikuu kinachopendelewa katika kutambua saratani ya tumbo kama mtu ana viashiria kuwa anaweza kuwa nayo. Baada ya kupewa dawa ya nusu kaputi (dawa ya kukulaza usingizi), kamera ndogo iliyowekwa kwenye mrija mdogo – endoscope – huingiza kupitia kwenye koo na kumpatia nafasi daktari kukagua ukuta wa umio, tumbo na sehemu ya mwanzo ya utumbo katika kompyuta. Kama daktari atakuta sehemu yenye tatizo, anaweza kuchukua sampuli kwa kutumia endoscope. Sampuli hii hupelekwa maabara na wataalamu kuikagua kama ina seli za saratani.
 • Upper gastrointestinal series – Hiki ni kipimo cha eksirei kinachohusishwa mtu kuchomwa sindano ambayo husaidia kupunguza kasi ya chakula kupita kwenye tumbo na utumbo ili iwe rahisi kuonekana kwenye picha za eksirei. Kwa ajili ya kipimo hiki, mgonjwa hupatiwa uji wa barium ili anywe. Anina ya eksirei inayoitwa fluoroscopy hufuatilia jinsi uji wa barium unavyopita kwenye umio, tumbo na utumbo mwembamba. Picha zinapigwa katika mikao mbalimbali. Kipimo kinachukua kama saa 3 au zaidi ili kukamilika.
 • Kipimo cha kuangalia idadi ya seli kwenye damu – complete blood count – kipimo hiki husaidia kutambua kama mgonjwa wa saratani ya tumbo ana upungufu wa damu.
 • Kipimo cha kinyesi – Kipimo hiki husaidia kutambua kama kuna damu kwenye mfumo wa chakula.

Watu wenye saratani ya tumbo wana changuzi nyingi za matibabu. Chaguzi ni upasuaji, tiba ya mionzi, tibakemikali, au muungano wa njia hizi. Njia inayoweza kuponesha kabisa ni ya kufanya upasuji wa kuondoa tumbo kabisa (gastrectomy). Tiba ya mionzi au tiba ya kemikali inaweza kusaidia. Tafiti za hivi karibuni zinaonesha kuwa, kupewa tibamionzi na tibakemikali baada ya upasuaji huongeza uwezekano wa kupona, lakini kwa wagonjwa wenye saratani ya tumb iliyosambaa, tibakemikali na/au tiba ya mionzi inaweza kupunguza dalili na kuboresha maisha ya mgonjwa lakini inaweza isiponye.

Kwa wagonjwa ambao tumbo limeziba kabisa na chakula hakipiti, wanawea kufanyiwa upasuji wa kuweka njia mbadala ya chakula kupita ili kupunguza dalili. Kabla matibabu hayajaanza, muulize daktari kuhusu madhara unayowea kupata wakati na baada ya tiba na jinsi yatavyobadili mfumo wako wa maisha.

Kwa sababu matibabu ya saratani kwa kawaida huharibu tishu zenye afya, madhara ni kawaida. Madhara yanaweza yasifanane kati ya mtu na mtu na yanaweza kubadilika katika kila hatua ya tiba.

Kuzuia saratani ya tumbo

Takwimu za kiepidemiolojia zinaonesha kuwa ukifanya mambo yafuatayo yataongeza uwezekano wa kutokupta saratani ya tumbo.

Matarajio

Matarajio yanatofautiana sana. Yanategemea:

 • Mahala uvimbe au kansa ilipo kwenye tumbo
 • Je, ni kwa kiasi gani imevamia ukuta wa tumbo
 • Je, imesambaa au haijasambaa kwenda sehemu nyingine za mwili

Matatizo yanayoweza kutokea

 • Kujaa kwa maji kwenye tumbo – ascites
 • Kuvuja damu kwenye mfumo wa chakula
 • Kusambaa kwa saratani kwenda kwenye viungo au tishu
 • Kupungua uzito

Vyanzo

https://medlineplus.gov/ency/article/000223.htm

Leave a Reply

Your email address will not be published.

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.

Jiunge Nasi