SARATANI YA UKE: Sababu, dalili, matibabu

Maelezo ya jumla

Saratani ya uke ni kansa inayotokea kwa nadra sana. Haina dalili za awali. Uke unaanzia kwenye mlango wa kizazi mpaka kwenye k*ma. Uke una urefu wa kati ya sentimeta 3 mpaka 4.   Unapokuwa na kansa ya uke, dalili za kawaida ni pamoja na kutokwa na damu ukeni, kutokwa na uchafu ukeni, unaweza kuhisi uvimbe na maumivu wakati wa ngono. Kufanyiwa kipimo cha “pap test” husaidia kutambua seli za kansa zilizopo. Matibabu ya kawaida ya kansa hii ni pamoja na matumizi ya laser, tiba ya mionzi, tibakemikali na upasuaji.

Ni zipi dalili za saratani ya uke? saratani ya uke

Saratani ya uke iliyo katika hatua za mwanzo haina dalili. Kadri uvimbe unavyoendelea kukua, watu wanaweza kuona moja au zaidi ya dalili zifuatazo:

Yapo matatizo mengine ya kitabibu yanayoweza kusababisha dalili kama hizi. Ni daktari pekee anayeweza kuthibitisha kwa hakika. Mtu yeyote mwenye dalili yoyote kati ya hizi, anapaswa kuongea na daktari ili afanyiwe utambuzi na kupata matibabu mapema inavyowezekana.

Ni nani yuko kwenye hatari zaidi ya kupata saratani ya uke?

Kulingana na takwimu za kitabibu zilizopo, zinaonesha kuwa, kutokea kwa saratani ya uke kunategemea baadhi ya mambo

 • Kuwa na saratani ya shingo ya mlango wa kizazi – hii inaweza kuwa ni kwa sababu mambo mengi yanayoongeza hatari ya kansa hizi mbili yanafanana
 • Kukutana na diethylstilbestrol (DES) – takwimu za kitabibu zinaonesha wanawake ambao mama zao walitumia diethylstilbestrol wako kwenye hatari kubwa zaidi ya kupata kansa ya uke kuliko ilivyo kawaida
 • Maambukizi ya virusi wa human papillomavirus – Aina ya 16 na 18 ya virusi vya HPV inaonekana kuhusiana sana na saratani ya uke
 • Maambukizi ya virusi vya ukimwi – Tafiti za kitabibu zinaonesha kuwa maambukizi ya VVU yanaongeza hatari ya kupata kansa ya uke
 • Mtindo usio bora wa maisha – Kuvuta sigara na kunywa pombe kupindukia kunaongeza hatari ya saratani ya uke
 • Umri – Saratani ya uke mara nyingi inawapata zaidi wanawake wenye umri zaidi ya mika 70

Ni wakati gani unapaswa kutafuta matibabu haraka?

Mpigie au nenda kamwone daktari kama una dalili yoyote ya saratani ya uke. Kama ukipata dalili yoyte kati ya zifuatazo, nenda kamwone dakatari haraka sana.

Utambuzi wa saratani ya ukesaratani ya uke

Sababu ya saratani ya uke inapaswa kutambuliwa, kama inawezekana, daktari anaweza kuamua kufanya vipimo vifuatavyo:

 • Kipimo cha “pap test” – wakati wa kipimo hiki daktari huingiza kifaa chenye mdomo kama wa bata “speculum” ili kufungua uke na kufanya iwe rahisi kufanya uchunguzi. Daktari atakwangua tishu kutoka kwenye ukuta wa uke na kwenda kuipima kwa darubini kwenye maabara.
 • Kipimo cha Computed tomography (CT) Scan – Kipimo hiki kinaweza kuhaiki sehemu ilipo saratani na kuonesha viungo vilivyo karibu na uke, na kama kansa imesambaa. Kipimo hiki ni muhimu kwa kutambua hatua ya ugonjwa na kama upasuaji utafaa kama moja ya matibabu
 • Kipimo cha Magnetic resonance imaging (MRI) – Mashine hii inatumia nguvu ya sumaku kutengeneza picha tofauti na zile za CTscan, picha hizi husaida zaidi katika utambuzi wa kansa hii.
 • Kipimo cha eksirei ya kifua – Kipimo hiki hufanyika ili kuangalia kama saratani imesambaa kwenda kwenye mapafu.

 Uchaguzi wa matibabu ya saratani ya uke

Wagonjwa wenye saratani ya uke wanaweza kutibiwa wa njia tofauti. Aina ya matibabu inategemea hatua ya saratani. Unaweza kutibiwa kwa kutumia laser, tiba ya mionzi, tiba ya kemikali, upasuaji au muunganiko wa njia hizi. Kabla matibabu hayajaanza, ni vizuri kumuuliza daktari madhara ya kila njia kabla haujayapokea. Matibabu ya saratani mara nyingi huharibu pia seli zenye afya na hii inaweza kusababisha matatizo. Matatizo yanayoweza kujitokeza kwa sababu ya tiba, hayafanani kwa kila mgonjwa, na yanaweza kubadilika kwa kila hatua ya matibabu unayopitia.

 • Upasuaji unatumia laser – upasuaji huu unatumia miali ya mwanga mkali wenye nguvu ili kuyeyisha seli za kansa.
 • Tiba ya mionzi – hii hutumia miali ya eksirei ili kudumaza seli za saratani zisiendelee kukua
 • Tiba kemikali – hii hutumia kemikali kali ili kuua au kuzuia seli za saratani kuendelea kukua
 • Upasuaji – hii hutumika katika hatua za mwanzo za saratani na kwa kansa ambazo zimeshindwa kutibiwa na mionzi.

Je, matibabu ya saratani ya uke yataathiri uwezo wa kushiriki ngono?

Athari kwa uwezo wa kushiriki ngono hutofautiana kwa kila mtu, baadhi ya watu hawana matatizo kabisa na baadhi wanayo kidogo – ya kimwili na msongo unaotokana na tiba. Wengine wanajisikia kuwa karibu zaidi na wenzi wao na inaongeza hamu ya ngono zaidi katika kipindi hiki. Japo, kushika mimba kunawezekana wakati wa matibabu, haishauriwi kwa sababu baadhi ya dawa zinaweza kusababisha matatizo kwa mtoto.

Tiba ya mionzi kwa ajili ya matibabu ya kansa ya uke husababisha ukomo wa hedhi kwa mwanamke kuwahi, unaweza kupata makovu, kukauka na kupungua kwa upenyo wa uke kunakoweza kusababisha maumivu wakati wa ngono. Daktari anaweza kushauri utumie vifaa vya kupanua uke “dilators” ili kuzuia upenyo wa uke kupungua na anaweza kushauri kutumia gels na creams ili kupunguza kukauka kwa uke.

Matarajiosaratani ya uke

Matarajio ya mtu mwenye saratani ya ukeni hutegemea mambo yafuatayo:

 • Mahali ulipo uvimbe kwenye uke
 • Uvimbe umeingia ndani kiasi gani kutoka kwenye ukuta wa uke
 • Hatua ya saratani
 • Hali ya kiafya ya mgonjwa kwa ujumla

Matatizo yanayoweza kutokea

Saratani ya uke inaweza kusambaa kwenda maeneo mengine ya mwili. Matatizo yanaweza pia kutokana na tiba ya mionzi, upasuaji na tibakemikali.

Kuzuia saratani ya uke

Japo sababu za kutokea kwa saratani ya uke hazifahamiki vizuri, takwimu za kitabibu zinaoesha kuwa yafuatayo yanaweza kupunguza uwezekano wa kupata saratani hii:

 • Kepuka kupata maambukzi ya HPV – Kuepuka ngono nzembe, kutumia kondomu au kupata chanjo ya HPV
 • Kubadili mfumo wa maisha – acha kutumia pombe au kuvuta sigara

Vyanzo

https://medlineplus.gov/ency/article/001510.htm

Leave a Reply

Your email address will not be published.

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.

Jiunge Nasi