Last Updated on October 12, 2023 by Dr Mniko
Maelezo ya jumla
Saratani ya uume ni kansa inayoanzia kwenye uume. Uume ni moja ya viungo vinavyotengeneza mfumo wa uzazi wa mwanamme.
Ni zipi dalili za saratani ya uume?
Zifuatazo ni dalili za saratani ya uume:
- Kidonda/uvimbe kwenye uume
- Kidonda kisicho na maumivu kwenye uume (kwa mara chache, kidonda kinaweza kuwa na maumivu)
- Maumivu ya uume na kuvuja damu kutoka kwenye uume (hii inaweza kutokea kama saratani imekua sana)
Ni nini husababisha saratani ya uume?
Sababu mahususi bado haifahamiki, lakini;
- Kuwa na uchafu, mweupe unaotengenezeka chini ya govi (kama haujatahiriwa), unaweza kuongeza hatari ya kupata saratani ya uume
- Watu ambao hawajatahiriwa na hawasafishi vizuri chini ya govi na wanaume wenye masundosundo/vigwaru kwenye uume au wenye maambukizi ya virusi vya human papillomavirus (HPV) wako kwenye hatari kubwa ya kupata kansa ya uume.
Utambuzi
- Daktari atafanya uchunguzi wa mwili, anaweza kuona kidonda kisicho na maumivu kinachoonekana kama chunusi au masundosundo/vigwaru. Mara nyingi uvimbe huu unapatikana karibu na kichwa cha uume.
- Sampuli ya tishu za uvimbe itachukuliwa ili kutambua kama ni kansa.
Ni wakati gani unapaswa kutafuta matibabu haraka?
Onana na daktari haraka kama unadhani una dalili za saratani ya uume.
Uchaguzi wa matibabu
Uchaguzi wa matibabu utategemea mambo yafuatayo:
- Ukubwa na mahala ulipo uvimbe kwenye uume
- Matokeo ya vipimo vya maabara
- Hatua na kiasi ambacho saratani imesambaa
- Afya ya mgonjwa kwa ujumla na nini unachopendelea
Kwa ujumla, matibabu ya saratani ya uume hujumuisha:
- Tibakemikali – hii hutumia dawa kali zinazoweza kuua au kuzuia seli za kansa kuendelea kukua na kupunguza uwezekano wa kusamba kwenda sehemu nyingine za mwili
- Tiba ya mionzi – Hii hutumia kiwango kikubwa cha mionzi kuua au kudumaza seli za kansa zisiendelee kukua
- Upasuaji – Hii ndio njia inayopendelewa zaidi kutibu saratani ya uume, kukata na kuondoa kansa
- Kama kansa ni ndogo na iko karibu na kichwa cha uume, upasuaji unaweza kufanyika ili kuondoa sehemu yenye saratani pekee.
- Kwa saratania mabzo zimesambaa sana, inaweza kulazimu kukata na kuondoa kabisa uume. Tobo jipya huundwa/ kutengenezwa kwenye kinena ili kuruhusu mkojo kutka mwilini.
- Tibakemikali inaweza kutumiwa pamoja na upasuaji. Bleomycin, cisplatin, au methotrexate hutumika kutibu saratani ya uume.
- Tiaba ya mionzi mara nyingi hupendekezwa kwa pamoja na upasuaji.
Kuzuia saratani ya uume
- Kutahiriwa kunapunguza hatari ya kupata kansa ya uume. Wanaume ambao hawajatahiria wanapswa kufundishwa umuhimu wa kusafisha chini ya govi kama sehemu ya usafi
- Usafi binafsi na kufanya ngono salama, kama vile kugunga kabisa, kuwa na mpenzi mmoja mwaminifu, na kutumia kondomu ili kuzuia virusi wa HPV, kunaweza kupunguza uwezekano wa kupata kansa ya uume
Matarajio
Matokeo yanaweza kuwa mazuri kama kansa imetambuliwa mapema na kutibiwa. Uwezekano wa kuishi miaka 5 kwa mtu mwenye saratani ya uume ni 65%. Uwezo wa kukojoa na kushiriki ngono kunaweza kuendelea kuwepo hata baada ya kiasi kikubwa cha sehemu ya uume kuondolewa.
Matatizo yanayoweza kutokea
Kansa ya uume mara nyingi husambaa kwenda sehmu nyingine za mwili katika hatua za mwanzo za ugonjwa.
Leave feedback about this