Last Updated on October 12, 2023 by Dr Mniko
Seli ni kama kiwanda?
Seli za mwili ni kama kiwanda.
Kila seli ni msingi kwa uhai wa kiwanda kizima.
Mwili wa mwanadamu umetengenezwa kwa seli trilioni 30.
Kuna aina mbali mbali za seli zaidi ya 200
Kila seli imetengenezwa kufanya kazi maalumu
Seli za mifupa, zinatengeneza na kujenga mifupa inayotegemeza mwili.
Seli za mfumo wa fahamu, zinatuma na kupeleka jumbe mbali mbali kwenye ubongo na sehemu za mwili ili kazi nyingi zitendeke.
Seli za damu, hubeba na kupeleka hewa ya oksijeni mwilini, na husaidia pia mfumo wa kinga ya mwili kufanya kazi yake.
Seli za mbegu ya mwanamme na yai la mwanamke huungana ili kutengeneza mtoto.
Ujumbe wa kijenetiki ulio katika kila aina ya seli hutumika kama mwongozo wa kila shughuli.
Kila aina ya seli ni muhimu na inapaswa kulindwa isiharibiwe.
Kula mlo kamili, fanya mazoezi, Pata usingizi wa kutosha, dhibiti msongo wa mawazo na epuka kukutana na sumu
Leave feedback about this