SINDANO ZA KILA MWEZI ZA KUZUIA MIMBA

Sindano za Kila Mwezi za Kuzuia Mimba ni Nini?

Sindano za kila mwezi za kuzuia mimba zina vichocheo – projestini na estrojeni – kama vilivyo vichocheo vya asili vya projestini na estrojeni kwenye mwili wa binadamu. (Vidonge vyenye vichocheo viwili pia vina aina hizi za vichocheo).

 • Pia zinajulikana kama dawa mseto ya sindano kuzuia mimba, sindano.
 • Kimsingi hufanya kazi kwa kuzuia mayai yasipevuke na kutoka kwenye ovari (uovuleshaji).

Mambo Muhimu kuhusu sindano za kila mwezi za kuzuia mimba

 • Mabadiliko ya hedhi ni ya kawaida lakini hayana madhara. Kwa kawaida, hedhi ya matone matone, siku chache za hedhi, hedhi isiyotabirika au isiyokuwa ya mfululizo.
 • Kurejea kwa wakati. Kurejea kila wiki 4 ni muhimu ili kupata ufanisi mkubwa zaidi.
 • Sindano zinaweza kuwahi mapema au kuchelewa siku 7. Ni vizuri urudi hata kama umechelewa.

Sindano za kila mwezi za kuzuia mimba zina Ufanisi Kiasi Gani?

Ufanisi hutegemea kurudi mapema. Hatari ya mimba ni kubwa wakati mwanamke anapochelewa au kukosa sindano.

 • Kama ilivyozoeleka, hutokea karibu mimba 3 kwa wanawake 100 wanaotumia sindano za kila mwezi kwa mwaka wa kwanza. Hii ina maana kuwa wanawake 97 kati ya 100 wanaotumia sindano hawatapata mimba.
 • Wanawake wanapochoma sindano kwa wakati, kutakuwa na chini ya mimba moja kwa wanawake 100 wanaotumia sindano za kila mwezi kwa mwaka wa kwanza (wanawake 5 kati ya 10,000).

Kurudi uwezo wa kushika mimba baada ya kuacha kuchoma sindano: Wastani wa karibu mwezi mmoja zaidi kuliko njia nyingine.

Kuhusu Athari za sindano za kila mwezi za kuzuia mimba

Madhara yanayofahamika zaidi Hedhi ya matone matone na hedhi ya siku chache, hedhi isiyotabirika, na kupata hedhi mara chache.
Kuongezeka uzito, maumivu ya kichwa, kizunguzungu, maumivu ya matiti, na hata madhara mengine.
Ufafanuzi kuhusu madhara haya Madhara si dalili za ugonjwa.
Kawaida hupungua au kukoma ndani ya miezi michache ya mwanzo baada ya kuanza sindano.
 Ni ya kawaida, lakini baadhi ya wanawake hawayapati.
Unaweza kurudi kituo cha afya kwa ajili ya kupata msaada kama madhara yanakubughudhi sana

Faida na Hasara za kutumia sindano za kila mwezi

Faida za Kiafya

 • Husaidia kukulinda dhidi ya:
  • Hatari ya kupata mimba
  • Saratani ya kizazi (endometrial cancer)
  • Saratani ya ovari
  • Dalili za Ugonjwa wa Uvimbe wa pelvisi (PID)
 • Zinaweza kusaidia kukinga dhidi ya:
  • Uvimbe wa ovari
  • Anemia kutokana na Ukosefu wa madini ya chuma
 • Hupunguza:

Hasara  Kiafya

Nani Anaweza Kutumia Sindano za Kila Mwezi

Karibu wanawake wote wanaweza kutumia sindano za kila mwezi kwa usalama na ipasavyo, ikiwa ni pamoja na wanawake ambao:

 • Wameshazaa au hawajawahi kupata watoto
 • Hawajaolewa
 • Wa umri wowote, pamoja na vijana na wanawake wenye umri zaidi ya miaka 40
 • Wametoka kutoa mimba au mimba imeharibika
 • Wanavuta idadi yoyote ya sigara kila siku na wana umri chini ya miaka 35
 • Wanavuta sigara chini ya 15 kila siku na wana umri zaidi ya miaka 35
 • Wana anemia wakati huu au waliwahi kuwa na anemia siku za nyuma
 • Wana vena zilizojikunjakunja na kutanuka Wameambukizwa VVU, kama anapata au hapati tiba ya dawa za kupunguza makali ya UKIMWI “antiretroviral”

Nani hawezi kutumia sindano za kila mwezi?

Ikiwa jibu ni “Ndio”, kwa maswali yafuatayo, haupaswi kutumia sindano za kila mwezi

 1. Je unanyonyesha mtoto mwenye umri chini ya miezi sita? NDIYO
 • Kama ananyonyesha wakati wote au karibu wakati wote: Anaweza kuanza miezi 6 baada ya kujifungua au wakati maziwa ya mama yanapokuwa si chakula kikuu cha mtoto – chochote kitakachotangulia
 • Kama ananyonyesha kiasi fulani: Anaweza kuanza sindano za kila mwezi mapema wiki sita baada ya kujifungua
 1. Je umewahi kupata mtoto katika wiki 3 za hivi karibuni na kuwa hunyonyeshi? NDIYO- Anaweza kuanza sindano za kila mwezi mapema wiki 3 baada ya kujifungua
 2. Je unavuta sigara 15 au zaidi kwa siku?NDIYO- Kama ana umri wa miaka 35 au zaidi na anavuta zaidi ya sigara 15 kwa siku, usimpatie sindano za kila mwezi. Mhimize aache kuvuta sigara na msaidie kuchagua njia nyingine ya uzazi wa mpango.
 3. Je unasumbuliwa na sirosisi kali ya ini, ugonjwa wa ini, au uvimbe wa ini? (Je macho au ngozi yake ina rangi ya manjano isivyo kawaida? [dalili za umanjano]) NDIYO -Kama ataripoti kuugua ugonjwa mkali wa ini (umanjano, hepatitisi, sirosisi kali, uvimbe wa ini), usimpatie sindano za kila mwezi. Msaidie kuchagua njia isiyokuwa na vichocheo. (Kama amewahi kuwa na sirosisi kidogo au ugonjwa wa kibofu cha nyongo, anaweza kutumia sindano za kila mwezi)
 4. Je una shinikizo la juu la damu? NDIYO- Kama huwezi kupima shinikizo la damu na anaripoti historia ya shinikizo la juu la damu, au kama anaendelea kutibiwa shinikizo la juu la damu, usimpatie sindano za kila mwezi. Apewe rufaa aende kupima shinikizo la damu kama inawezekana au asaidiwe kuchagua njia nyingine isiyokuwa na estrojeni.
  • Pima shinikizo lake la damu kama inawezekana:
   • Kama shinikizo la damu ni la chini ya 140/90 mm Hg. mpatie sindano za kila mwezi.
   • Kama shinikizo la damu sistoli ni 140 mm Hg au juu zaidi au shinikizo la damu diastoli ni 90 au juu zaidi, usimpatie sindano za kila mwezi. Msaidie kuchagua njia isiyokuwa na estrojeni, lakini pia isiwe sindano zenye kichocheo kimoja kama shinikizo la damu sistoli ni 160 au zaidi au shinikizo la damu diastoli likiwa 100 au zaidi.
  • (Kipimo cha mara moja cha shinikizo la damu kati ya 140-159/ 90-99 mm Hg hakitoshi kutambua shinikizo la juu la damu. Mpatie kinga atumie hadi atakaporejea tena kwa ajili ya kupima tena shinikizo la damu, au msaidie kuchagua njia nyingine sasa kama atapendelea. Iwapo kipimo cha safari nyingine cha shinikizo la damu kitakuwa chini ya 140/90, anaweza kutumia sindano za kila mwezi).
 1. Umewahi kuugua kisukari kwa zaidi ya miaka 20 au kupata uharibifu wa ateri zako, uwezo wa kuona, fi go, au mfumo wa neva uliosababishwa na kisukari? NDIYO- Usimpatie sindano za kila mwezi. Msaidie kuchagua njia isiyokuwa na estrojeni lakini pia isiwe sindano zenye kichocheo kimoja.
 2. Je umewahi kupata kiharusi, damu kuganda kwenye miguu au mapafu yako, moyo kushindwa kufanya kazi, au matatizo mengine makubwa ya moyo? NDIYO- Kama anaripoti kupata matatizo ya moyo kushindwa kufanya kazi vizuri, ugonjwa wa moyo kutokana na kuziba au kupungua njia ya ateri, au kiharusi, usimpatie sindano za kila mwezi. Msaidie kuchagua njia isiyokuwa na estrojeni, lakini pia isiwe sindano zenye kichocheo kimoja. Kama ataripoti kuganda kwa damu kwenye vena zilizo ndani kwenye miguu au kwenye mapafu (si kuganda kidogo), msaidie kuchagua njia isiyokuwa na vichocheo.
 3. Je una au umewahi kupata saratani ya matiti? NDIYO- Usimpatie sindano za kila mwezi. Msaidie kuchagua njia isiyokuwa na vichocheo.
 4. Je wakati fulani imewahi kutokea ukaona mwanga mkali na kushindwa kuona kabla ya kuanza kupata maumivu makali ya kichwa (kipandauso na aura)? Je unaumwa kichwa chenye kupwita, maumivu makali sana, mara nyingi ya upande mmoja wa kichwa, ambayo huendelea kwa saa chache hadi siku kadhaa na kinaweza kusababisha kichefuchefu au kutapika (kipandauso)? Maumivu haya ya kichwa mara nyingi huzidishwa na mwanga, kelele, au kutembea. NDIYO- Kama anapata kipandauso na aura katika umri wowote, usimpatie sindano za kila mwezi. Kama anakuwa na kipandauso bila aura na ana umri wa miaka 35 au zaidi, usitoe sindano za kila mwezi. Wasaidie wanawake hawa kuchagua njia isiyokuwa na estrojeni. Kama umri wake ni chini ya miaka 35 na hupata kipandauso bila aura, anaweza kutumia sindano za kila mwezi
 5. Je unapanga kufanyiwa upasuaji mkubwa ambao utakufanya usiweze kutembea kwa muda wa wiki moja au zaidi? NDIYO -Kama ndivyo, anaweza kuanza sindano za kila mwezi wiki mbili baada ya upasuaji. Mpaka itakapofi ka kuwa anaweza kuanza sindano za kila mwezi, aendelee kutumia kinga.
 6. Je una hali fulani ambayo inaweza kukuongezea uwezekano wa kupata ugonjwa wa moyo (ugonjwa wa ateri koronari) au kiharusi, kama uzee, kuvuta sigara, shinikizo la juu la damu, au kisukari? NDIYO -Usimpatie sindano za kila mwezi. Msaidie kuchagua njia isiyokuwa na estrojeni, lakini pia isiwe sindano zenye kichocheo kimoja.
 7. Jee unatumia Laotrigine kuzuia kifafa? NDIYO Usimpe shindano za kila mwezi kwa sababu itapunguza nguvu za dawa unazotumia kwa maradhi yake.

Kwa kawaida mwanamke mwenye tatizo lolote kati ya yale yaliyoorodheshwa asitumie sindano za kila mwezi. Hata hivyo, katika hali maalum, inapokuwa hakuna njia nyingine sahihi au inayofaa kwake, mtoa huduma za afya mwenye utaalamu ambaye kwa kawaida anaweza kutathmini hali na mazingira maalum ya mwanamke anaweza kuamua kumpatia sindano za kila mwezi. Mtoa huduma za afya anaweza kufi kiria ukubwa wa tatizo lake na, kwa matatizo mengi, kama ataweza kupata huduma za ufuatiliaji.

Wakati Gani wa Kuanza Kudungwa sindano za kila mwezi

Mwanamke anaweza kuanza kudunga sindano wakati wowote anapotaka kama kuna uhakika wa kutosha kuwa hana mimba. Kama utachomwa sindano ndani ya siku 7 baada ya hedhi kuanza, hauhitaji njia nyingine kujikinga na mimba. Kama umechomwa sindano siku 7 baada ya hedhi kuanza, unapaswa kuacha kushiriki ngono au kutumia njia nyingine ya kuzuia mimba kwa siku 7 zinazofuata ili kuipa muda sindano kuanza kufanya kazi.

Hali ya mwanamke Aanze lini kutumia
Asiyepata hedhi Unaweza kuanza kuchomwa sindano yenye kichocheo kimoja  muda wowote kama kuna uhakika wa kutosha kuwa si mjamzito
Unapaswa kuepa kushiriki ngono au kutumia njia nyingine ya uzazi wa mpango kwa angalau siku 7 zinazofuata
Aliyejifungua na Ananyonyenya Kma una nyonyesha wakati wote- Chelewesha sindano ya mwanzo mpaka miezi sita baada ya kujifungua au wakati mtoto atakapokuwa hategemei maziwa ya mama kama chakula kikuu – chochote kitakachotangulia
Kama mtoto ameanza kula na vyakula vingine – anaweza kuanza sindano wakati wowote kukiwa na uhakika wa kutosha kuwa hana mimba. Atahitaji kinga kwa siku saba za mwanzo baada ya sindano.
Aliyejifungua na hanyonyeshi Anaweza kuanza sindano wakati wowote katika siku 21-28 baada ya kujifungua. Hakuna haja ya kinga
Kama utaanza sindano baada ya siku 28 kupita baada ya kujifungua, unapaswa kuepa kushiriki ngono au kutumia njia nyingine ya uzazi wa mpango kwa angalau siku 7 zinazofuata
Baada ya mimba kuharibika  Mara moja. Atahitaji njia mbadala kwa siku 7 za kwanza za kumeza vidonge.
Kubadili kutoka njia yenye vichocheo Mara moja, kama umekuwa akitumia njia yenye vichocheo wakati wote na kwa usahihi au vinginevyo kukiwa na uhakika wa kutosha kuwa hana mimba. Hakuna haja ya kutumia kinga (kondomu).
kubadili kutoka njia isiyo ya vichocheo Anaweza kuanza kuchomwa sindano yenye kichocheo kimoja wakati wowote kukiwa na uhakika wa kutosha kuwa hana mimba. Atahitaji kinga kwa siku 7 za kwanza baada ya kuchomwa sindano.
Baada ya kumeza vidonge vya dharura kuzuia mimba Unaweza kuanza sindano siku hiyohiyo uliyomeza vidonge vya dharura kuzuia mimba. Hakuna haja ya kusubiri kipindi kingine cha hedhi ili kuchoma sindano. utahitaji kutumia kinga kwa siku 7 za mwanzo baada ya sindano

Utaratibu wa Kuchoma Sindano (Mhudumu wa afya)

1.      Kunawa Mhudumu atanawa mikono kwa sabuni na maji, kama inawezekana
2.      Andaa kichupa MPA/estradiol cypionate: Tikisa vizuri viali.
NET-EN/estradiol valerate: Hakuna haja ya kutikisa viali.
Kama viali ina ubaridi, ipashe joto hadi kufi kia joto la mwili kwa kuishika kabla ya kuchoma sindano.
3.      Jaza bomba la sindano Toboa sehemu ya juu ya kichupa na sindano iliyo safi na jaza bomba la sindano dozi sahihi
4.      Fomula ya kuchoma sindano Ingiza sindano ndani ya nyonga (misuli ya ventrogluteal), mkono (msuli wa deltoid), matako (gluteal muscle, upper outer portion), au sehemu ya nje (anterior), paja, sehemu yoyote atakayopendelea mwanamke. Ingiza dawa iliyo kwenye sindano.
 Usichue mahali palipochomwa sindano.
5.      Tupa bomba na sindano mahali salama Usifunike, usipindishe au kuvunja sindano kabla ya kutupa.
Ziweke kwenye kasha lisiloweza kutoboka.

 

Nini cha Kufanya baada ya Kuchelewa Kuchoma Sindano

 • Kama umechelewa kurudia kuchoma sindano kwa muda usiozidi siku 7, unaweza kuchoma sindano yako inayofuata. Hakuna haja ya kupima, kuchunguza, au kutumia kinga.
 • Kama umechelewa kuchoma sindano inayofuata kwa zaidi ya siku 7 unaweza kuchoma sindano inayofuata kama: –
  • Hujafanya ngono tangu siku 7 baada ya siku aliyostahili kuchoma sindano yako ya mwisho, au
  • Umetumia kinga au Umemeza vidonge vya dharura kuzuia mimba baada ya tendo lolote la ngono bila kinga tangu siku 7 baada ya siku aliyostahili kuchoma sindano iliyofuata.
  • Utahitaji kutumia kinga kwa siku 7 za mwanzo baada ya sindano.
 • Kama Umechelewa zaidi ya siku 7 na hakutimiza vigezo hivi, hatua za ziada zinaweza kuchukuliwa ili kuwa na uhakika wa kutosha kuwa huna mimba

Imani potofu zilizopo kwenye jamii

Sindano za kila mwezi:

 • Zinaweza kusababisha kukosa hedhi, lakini hii haileti madhara. Ni sawa na kukosa hedhi wakati wa ujauzito. Damu haijengeki ndani ya mwili wa mwanamke.
 • Hazipo katika awamu ya majaribio ya utafiti. Wakala wa serikali amezithibitisha.
 • Hazimfanyi mwanamke kuwa mgumba.
 • Hazisababishi kukoma kwa hedhi mapema.
 • Hazisababishi kuzaliwa na ulemavu au kuzaa watoto wengi.
 • Hazisababishi kuwashwa.
 • Hazibadili mwenendo wa mwanamke kuhusu ngono

Vyanzo

https://medlineplus.gov/birthcontrol.html#:~:text=Birth%20control%2C%20also%20known%20as,cervical%20caps%2C%20and%20contraceptive%20sponges.

Leave a Reply

Your email address will not be published.

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.

Jiunge Nasi