Last Updated on October 13, 2023 by Dr Mniko
Sindano Zenye Kichocheo Kimoja (Sindano za kila baada ya miezi 3) ni Nini?
Sindano zenye kichocheo kimoja za kuzuia mimba ni sindano za kupanga uzazi anazochomwa mwanamke kila baada ya miezi mitatu ili kuzuia mimba. Aina mbili za sindano hizi ni Depot medroxyprogesterone acetate (DMPA) na norethisterone enanthate (NET-EN) kila moja ina projestini kama kilivyo kichocheo cha asili cha progesterone kwenye mwili wa mwanamke. (Kinyume na hii, sindano za kila mwezi zina estrojeni na projestini).
- Hazina estrojeni, na hivyo zinaweza kutumiwa wakati wote wa kunyonyesha maziwa ya mama pia na wanawake ambao hawawezi kutumia njia zenye estrojeni.
- DMPA, ndiyo sindano yenye kichocheo kimoja inayotumiwa zaidi, pia inajulikana kama “the shot”, “the jab”, the injection, Depo, Depo-Provera, Megestron, na Petogen.
- NET-EN pia inajulikana kama norethindrone enanthate, Noristerat, na Syngestal.
- Hutolewa kwa kudunga sindano kwenye misuli. Kisha kichocheo hutolewa polepole na kuingia kwenye mfumo wa damu. Fomula tofauti ya DMPA inaweza kuchomwa chini ya ngozi.
- Kimsingi hufanya kazi ya kuzuia mayai yasiruhusiwe kutoka kwenye ovari (uovuleshaji).
Mambo Muhimu kuhusu sindano zenye kichocheo kimoja
- Mabadiliko ya hedhi ni ya kawaida lakini hayana madhara. Kwa kawaida, hutokea kupata hedhi zisizotabirika kwa miezi kadhaa ya mwanzo na baadaye damu za hedhi huisha hazitoki tena.
- Rudi kwa ajili ya sindano mara kwa mara. Kurudi kila baada ya miezi 3 (wiki 13) kwa ajili ya sindano ya DMPA au kila miezi 2 kwa ajili ya NET-EN ni muhimu ili kupata mafanikio makubwa.
- Sindano inaweza kudungwa wiki 2 kabla au baada ya muda kufika. Mteja arudi hata kama amechelewa.
- Kuongezeka uzito ghafl a ni jambo la kawaida.
- Kawaida huchelewesha kushika mimba. Huchukua wastani wa miezi kadhaa zaidi kupata mimba baada ya kuacha kudunga sindano zenye kichocheo kimoja kuliko njia nyingine za uzazi wa mpango.
Sindano zenye kichocheo kimoja zina Ufanisi Kiasi Gani?
Ufanisi unategemea utakavyochoma sindano mara kwa mara: Hatari ya kupata mimba ni kubwa kama mwanamke ataacha kuchoma sindano.
- Kama ilivyozoeleka, hutokea karibu mimba 3 kwa wanawake 100 wanaotumia sindano zenye kichocheo kimoja kwa mwaka wa kwanza: Hii ina maana kuwa wanawake 97 kati ya 100 wanaotumia sindano zenye kichocheo kimoja katika mwaka wa kwanza hawatapata mimba.
- Wanawake wakipata sindano kwa wakati, kutakuwa na chini ya mimba 1 kwa wanawake 100 wanaotumia sindano zenye kichocheo kimoja katika mwaka wa kwanza (wanawake 3 kwa 1,000). Uwezo wa kushika mimba husitishwa: Wastani wa karibu miezi 4 kwa DMPA na mwezi mmoja kwa NET-EN kuliko njia nyingine.
Kuhusu Athari za sindano zenye kichocheo kimoja
Madhara yanayofahamika zaidi | Kwa miezi kadhaa ya mwanzo, atapata hedhi isiyotabirika, inayoendelea kwa muda mrefu, mara kwa mara, inayochelewa, kukosa hedhi. |
Katika mwaka mmoja, kukosa hedhi na kupata hedhi ya vitone vitone. | |
Kuongezeka uzito (karibu 1 -2 kg kwa mwaka), maumivu ya kichwa, kizunguzungu, mabadiliko ya hisia, kupungua kwa hamu ya ngono, tumbo kujaa na kukosa raha. | |
Ufafanuzi kuhusu madhara haya | Madhara si dalili za ugonjwa |
Hutokea mara nyingi, lakini baadhi ya wanawake hayawapati | |
Unaweza kurudi kituo cha afya kutafuta msaada iwapo madhara yatakuwa yanakusumbua. | |
Fanya yafuatayo ukipata madhara haya | Hedhi isiyotabirika – Ili kupata unafuu wa kiasi fulani, meza 800 mg za ibuprofen mara tatu kwa kila siku au 500 mg za mefenamic acid mara 2 kila siku baada ya mlo kwa siku 5, kuanzia wakati hedhi isiyotabirika inapoanza. |
Kama uzito wako unaongezeka– Chunguza mlo wako na ufuatilie ushauri wa mlo sahihi | |
Kupata Hedhi ya Damu Nyingi au ya Muda Mrefu (mara mbili zaidi ya kawaida au inayochukua muda mrefu zaidi ya siku 8) | |
Baadhi ya wanawake wanaotumia sindano zenye kichocheo kimoja hupata hedhi nyingi au huchukua muda mrefu zaidi. Haina madhara na kawaida hupungua au kukoma baada ya miezi michache. | |
Iwapo hedhi inazidi kiasi cha kutishia maisha au kama unataka, daktari atakusaidia kuchagua njia nyingine. Wakati huo anaweza kukuandikia vidonge vyevye vichocheo viwili ili kupunguza kutokwa damu. |
Faida na Hasara za kutumia sindano zenye kichocheo kimoja
Faida za Kiafya
- DMPA
- Husaidia kukinga dhidi ya:
- Hatari ya kupata mimba
- Saratani ya kizazi
- Uvimbe wa kizazi
- Zinaweza kukinga dhidi ya:
- Dalili za ugonjwa wa uvimbe wa nyonga
- Upungufu wa madini ya chuma kwenye damu
- Hupunguza:
- Tatizo la seli mundu miongoni mwa wanawake wenye upungufu wa damu kutokana na seli mundu
- Dalili za endometriosisi (maumivu ya nyonga, hedhi isiyotabirika)
- Husaidia kukinga dhidi ya:
- NET-EN
- Husaidia kukinga dhidi ya upungufu wa damu kutokana na upungufu wa madini ya chuma
Hasara Kiafya
- Hakuna
Nani Anaweza Kutumia Sindano zenye kichocheo kimoja
Karibu wanawake wote wanaweza kutumia sindano zenye kichocheo kimoja kwa usalama na ipasavyo, ikiwa ni pamoja na wanawake ambao:
- Wameshawahi au hawajawahi kupata watoto
- Hawajaolewa
- Wa umri wowote, pamoja na vijana na wanawake wenye umri unaozidi miaka 40
- Wametoa mimba au mimba imeharibika
- Wanaovuta sigara, bila kujali umri wa mwanamke au idadi ya sigara alizokwishavuta
- Wanaonyonyesha (kuanzia wiki sita baada ya kujifungua)
- Wameambukizwa VVU, kama wanatumia au hawatumii vidonge vya kupunguza makali ya UKIMWI
Nani hawezi kutumia sindano yenye kichocheo kimoja?
Ikiwa jibu ni “Ndio”, kwa maswali yafuatayo, haupaswi kutumia sindano yenye kichocheo kimoja
- Je unanyonyesha mtoto mwenye umri chini ya wiki 6? NDIYO – Anaweza kuanza kutumia sindano zenye kichocheo kimoja mapema wiki sita baada ya kujifungua
- Je unaugua sirosisi kali ya ini, ugonjwa wa ini, au uvimbe wa ini? (Je macho au ngozi yake kawaida ni ya manjano [dalili za umanjano]? NDIYO – Kama utaripoti kuwa na ugonjwa mkali wa ini (umanjano, hepatitisi kali, sirosisi kali, uvimbe wa ini), usimpatie sindano yenye kichocheo kimoja. Uasaidiwa kuchagua njia isiyokuwa na vichocheo.
- Je una shinikizo la juu la damu? NDIYO – Kama huwezi kupima shinikizo la damu na unaripoti kuwa umeshawahi kupata shinikizo la juu la damu siku za nyuma, utapewa sindano zenye kichocheo kimoja. Utapimwa shinikizo la damu kama inawezekana:
-
- Kama kwa wakati huo unaendelea na tiba ya shinikizo la juu la damu na limedhibitiwa vya kutosha, au shinikizo lako la damu lipo chini ya 160/100 mm Hg, utachomwa sindano zenye kichocheo kimoja.
- Kama shinikizo la damu la sistoli ni 160 mm Hg au zaidi au shinikizo la damu la diastoli ni 100 au zaidi, HAUTACHOMWA sindano yenye kichocheo kimoja. Utasaidiwa kuchagua njia nyingine – isiyokuwa na estrojeni.
- Je umekuwa na kisukari kwa zaidi ya miaka 20 au uharibifu wa ateri zako, uwezo wa kuona, fi go, au mfumo wa neva uliosababishwa na kisukari? NDIYO – Hautachomwa sindano zenye kichocheo kimoja. Utasaidiwa kuchagua njia nyingine – isiyokuwa na estrojeni.
- Je umewahi kupata matatizo ya kiharusi, damu kuganda kwenye miguu au mapafu yako, kukwama kwa moyo? NDIYO – Kama utaripoti kukwama moyo, ugonjwa wa moyo kutokana na kuziba au kusinyaa kwa ateri, au kiharusi, hautachomwa sindano zenye kichocheo kimoja. Utasaidiwa kuchagua njia nyingine – ile isiyokuwa na estrojeni. Kama utaripoti kuwa damu inaganda ndani ya vena za miguu au kwenye mapafu, utasaidiwa uchague njia isiyotumia vichocheo.
- Je unapata hedhi isiyotabirika? NDIYO – Kama unapata hedhi isiyotabirika ambayo inaonyesha dalili ya mimba au hali ya ugonjwa, sindano zenye kichocheo kimoja zinaweza kufanya uchunguzi na ufuatiliaji wa matibabu kuwa mgumu. Utasaidiwa kuchagua njia ya kutumia wakati ukichunguzwa na kutibiwa.
- Je una au umewahi kupata saratani ya matiti? NDIYO – Usimpatie sindano zenye kichocheo kimoja. Utasaidiwa kuchagua njia isiyokuwa na vichocheo.
- Je una magonjwa kadhaa ambayo yanaweza kukuzidishia uwezekano wa kupata ugonjwa wa moyo (ugonjwa wa ateri koronari) au kiharusi, kama vile shinikizo kubwa la damu na kisukari? NDIYO – Usimchome sindano yenye kichocheo kimoja. Utasaidiwa kuchagua njia nyingine – ile isiyokuwa na vichocheo.
Kwa kawaida, wanawake wenye hali zilizoorodheshwa hapo juu inafaa wasitumie sindano yenye kichocheo kimoja. Hata hivyo, katika hali ya kipekee, iwapo hakuna njia nyingine sahihi au haziwezekani kwake kutumia njia hiyo, mtoa huduma mwenye utaalamu ambaye anaweza kuchunguza kwa makini matatizo maalum na hali ya mwanamke anaweza kuamua kama anaweza kutumia.
Wakati Gani wa Kuanza Kudungwa sindano zenye kichocheo kimoja
Mwanamke anaweza kuanza kudunga sindano wakati wowote anapotaka kama kuna uhakika wa kutosha kuwa hana mimba. Kama utachomwa sindano ndani ya siku 7 baada ya hedhi kuanza, hauhitaji njia nyingine kujikinga na mimba. Kama umechomwa sindano siku 7 baada ya hedhi kuanza, unapaswa kuacha kushiriki ngono au kutumia njia nyingine ya kuzuia mimba kwa siku 7 zinazofuata ili kuipa muda sindano kuanza kufanya kazi.
Hali ya mwanamke | Aanze lini kutumia |
Asiyepata hedhi | Unaweza kuanza kuchomwa sindano yenye kichocheo kimoja muda wowote kama kuna uhakika wa kutosha kuwa si mjamzito |
Unapaswa kuepa kushiriki ngono au kutumia njia nyingine ya uzazi wa mpango kwa angalau siku 7 zinazofuata | |
Aliyejifungua na Ananyonyenya | Unaweza kuchomwa sindano yenye kichocheo kimoja muda wowote (hata mara tu baada ya kujifungua) kama kuna uhakika wa kutosha kuwa si mjamzito |
Kama ni chini ya miezi 6 baada ya kujifungua, haujaanza kupata hedhi na unanyonyesha maziwa ya mama pekee – hauhitaji njia mbadala ya kukukinga na ujauzito | |
Kama umejifungua zaidi ya siku 21 zilizopita na haunyonyeshi wakati wote – mwanao anakula vyakula vingine – Unapaswa kuepa kushiriki ngono au kutumia njia nyingine ya uzazi wa mpango kwa angalau siku 7 zinazofuata | |
Aliyejifungua na hanyonyeshi | Unaweza kuanza kuchomwa sindano yenye kichocheo kimoja muda wowote (hata mara tu baada ya kujifungua) kama kuna uhakika wa kutosha kuwa si mjamzito |
Kama ataanza kuchomwa sindano kabla ya siku 21 baada ya kujifungua – hatahitaji njia mbadala ya kuzuia ujauzito | |
Kama ataanza kutumia baada ya siku 21 baada ya kujifungua – Unapaswa kuepa kushiriki ngono au kutumia njia nyingine ya uzazi wa mpango kwa angalau siku 7 zinazofuata | |
Baada ya mimba kuharibika au kutoa mimba | Unatakiwa kuanza kutumia vidonge ndani ya siku 7 baada ya kuharibika kwa mimba |
Unapaswa kuepa kushiriki ngono au kutumia njia nyingine ya uzazi wa mpango kwa angalau siku 7 zinazofuata | |
Kubadili kutoka njia yenye vichocheo | Mara moja, kama umekuwa akitumia njia yenye vichocheo wakati wote na kwa usahihi au vinginevyo kukiwa na uhakika wa kutosha kuwa hana mimba. Hakuna haja ya kutumia kinga (kondomu). |
kubadili kutoka njia isiyo ya vichocheo | Anaweza kuanza kuchomwa sindano yenye kichocheo kimoja wakati wowote kukiwa na uhakika wa kutosha kuwa hana mimba. Atahitaji kinga kwa siku 7 za kwanza baada ya kuchomwa sindano. |
Namna ya kuchoma Sindano (Mhudumu wa afya)
1. Kunawa | Mhudumu atanawa mikono kwa sabuni na maji, kama inawezekana |
2. Anda kichupa | DMPA: Tikisa vizuri kichupa. |
NET-EN: Hakuna haja ya kutikisa kichupa Hakuna haja ya kufuta sehemu ya juu ya kichupa na dawa ya kuua vijidudu. | |
Kama kichupa ni cha baridi, kipashe joto kufi kia joto la mwili kabla ya kuchoma sindano | |
3. Jaza bomba la sindano | Toboa sehemu ya juu ya kichupa na sindano iliyo safi na jaza bomba la sindano dozi sahihi |
4. Fomula ya kuchoma sindano | Ingiza sindano iliyo safi ndani ya nyonga (msuli wa nyonga), mkono (msuli wenye pembetatu), au matako (msuli wa tako, sehemu ya juu), popote anapopenda mwanamke. Sukumiza dawa iliyo kwenye bomba iingie kwenye misuli. |
Usichue mahali palipochomwa sindano | |
5. Tupa bomba na sindano mahali salama | Usifunike, usipindishe au kuvunja sindano kabla ya kutupa. |
Ziweke kwenye kasha lisiloweza kutoboka. |
Jambo la Kufanya Kutokana na Kuchelewa Kuchoma Sindano
- Kama umechelewa kuchoma sindano kwa muda usiozidi wiki 2, unaweza kupata sindano yako inayofuata. Hakuna haja ya kupima, kuchunguza, au kutumia kinga.
- Kama umechelewa kuchoma zaidi ya wiki 2 unaweza kupata sindano yake inayofuata kama: –
- Hujafanya ngono kwa wiki 2 baada ya tarehe ambayo ulitakiwa kuchoma sindano inayofuata, au
- Ulitumia kinga au umemeza vidonge vya dharura kuzuia mimba baada ya ngono yoyote bila kinga tangu wiki mbili baada ya siku aliyostahili kuchoma sindano, au
- Unanyonyesha wakati wote au wakati mwingi na tangu ujifungue haijapita miezi 6.
- Utahitaji kutumia kinga kwa siku 7 za mwanzo baada ya kuchoma sindano.
- Kama umechelewa zaidi ya wiki mbili na hutimizi vigezo hivi, hatua za ziada zinaweza kuchukuliwa ili kuwa na uhakika wa kutosha kuwa hauna mimba. Hatua hizi zitasaidia sana kwa sababu wanawake wengi ambao wamekuwa wakitumia sindano zenye kichocheo kimoja hawatakuwa wakipata hedhi angalau kwa miezi kadhaa hata baada ya kuacha kuchoma. Hivyo, kumwomba arudi wakati wa hedhi inayofuata ina maana sindano yake inayofuata itachelewa, na inawezekana kumfanya asiwe na kinga ya kuzuia mimba.
- Ni muhimu kujadiliana na mtaalamu wa afya kwa nini ulichelewa na kutafuta suluhisho. Kama kurudi mapema ni tatizo, jadili njia ya kutumia kama atachelewa kuchoma sindano inayofuata, kumeza vidonge vya dharura kuzuia mimba, au kuchagua njia nyingine.
Kuweka Sawa Mambo kuhusu imani potofu zilizopo kwenye jamii
Sindano zenye kichocheo kimoja:
- Zinaweza kuzuia hedhi, lakini hii haina madhara. Ni sawa na kukosa hedhi wakati wa ujauzito
- Damu haijikusanyi ndani ya mwili wa mwanamke.
- Hazivurugi mimba iliyopo.
- Hazimfanyi mwanamke kuwa mgumba
Leave feedback about this