KITANZI CHENYE KICHOCHEO KIMOJA (LEVONORGESTREL)
Kitanzi Chenye Levonorgestrel ni Nini? Kitanzi chenye kichocheo kimoja (levonorgestrel) ni kiplastiki chenye umbo la T ambacho hutoa kiasi kidogo cha kichocheo cha levonorgestrel kila siku. (Levonorgestrel ni projestini inayotumika sana kwenye vipandikizi au vidonge vya kumeza kuzuia mimba). Mtoa huduma ya afya aliyepata mafunzo maalum huingiza kitanzi kwenye kizazi cha mwanamke kupitia ukeni na […]