Maelezo ya jumla kuhusu fizi kuvuja damu
Tatizo la fizi kuvuja damu au kutokwa na damu kwenye fizi huwa ni ishara kuwa zimevimba au zina ugonjwa wa fizi ‘’gingivitis’’. Fizi zenye afya huwa zina rangi iliyofifia na huwa imara, lakini kama fizi zina matatizo yoyote zinabadilika rangi na kuwa za zambarau au nyekundu, zinavimba na zinakuwa zinang’aa na zinatokwa au kuvuja damu unapopiga mswaki. Mdomo wako unaweza kuwa unatoa harufu mbaya sana. Sababu ya tatizo hili mara nyingi huwa ni mkusanyiko au kujengeka kwa utando wa uchafu kwenye fizi , uchafu huu unajengwa na mabaki ya vipande vya chakula, mate na bakteria kwenye shina la meno kwa sababu ya usafi duni wa meno. Unaweza pia kuvuja damu kutoka kwenye fizi kwa sababu ya kusugua meno yako kwa nguvu au kwa fujo sana au kama una meno ya bandia ambayo hayakai ‘’fit’’ vizuri kwenye kinywa
Mwone daktari kama
Kama kuna fizi kuvuja damu na unaona mambo yafuatayo, panga kumwona daktari
- Kama meno yako yanauma au yamelegea
- Kama damu inavilia au kuvujia ndani ya ngozi kwa urahisi na unajihisi uchovu mkubwa kila mara
- Kama unatumia madawa ya kudhibiti damu kuganda ‘’anticoagulant’’ ambayo yanaweza kusababisha fizi zako kuvuja damu. Usiache kutumia dawa uliyopewa na daktari bila kuwasiliana na daktari
Unachoweza kufanya wewe mwenyewe fizi zikiwa zinavuja damu
Unaweza kufuata taratibu zifuatazo ili kusaidia fizi zinazokuja damu kupona a kuzuia madhara zaidi kwenye fizi zako na meno
- Kama unavuja damu sana, jaribu kuweka kipande cha ‘’gauze’’ au pamba iliyolowekwa kwenye maji baridi ya barafu kwenye fizi inayovuja kwa dakika kadhaa, itasaidia kupunguza kuvuja kwa damu
- Fanya usafi wa kinywa kwa usahihi. Piga mswaki meno yako taratibu kwa kutumia mswaki mpya, laini na ukihakikisha kuwa haukwangui fizi zako. Unaweza pia kutumia nyuzi za Hariri ili kuondoa uchafu katikati ya meno yako. ‘’floss’’ inasaidia kuondoa uchafu uliokwamwa katikati ya meno ambao hauwezi kufikiwa na mswaki kwa urahisi
- Usitumie vijiti vya kuchokonoa meno ‘’toothpicks’’ kusafisha katikati ya meno yako, kwa sababu vinaweza kuumiza fizi zako
- Acha kuvuta sigara, kwa sababu tumbaku inazidisha zaidi tatizo la kuvuja damu
Njia bora ya kusafisha kinywa fizi kuvuja damu
Ukifuata hatua zifuatazo wakati wa kufanya usafi wa kinywa, itasidia kupunguza hatari ya magonjwa ya fizi na kuzuia meno kuoza. Piga mswaki angalau mara mbili kwa siku na badilisha mswaki wako kila baada ya miezi 2-3. Safisha katikati ya meno yako kwa kutumia nyuzi za Hariri ‘’floss’’.
- Piga mswaki kabla ya kwenda kulala na unapoamka asubuhi au baada ya kupata kifungua kinywa. Tumia dawa ya mswaki yenye madini ya magadi ‘’fluoride’’ na mswaki laini. Hakikisha unasafisha sura zote za meno, hasa sehemu meno yanapokutana na fizi kwa kuvuta mswaki kwenda kuu
- Unaweza kutumia nyuzi za Hariri ‘’floss’’ ili kusafisha kati kati ya meno mara moja kwa siku. Funga upande wa nyuzi kwenye kidole cha mkono mmoja na upande mwingine kwenye mkono mwingine na kisha telezesha uzi juu mpaka chini kwenye shina, juu mpaka chini kwenye upande wa kila jino na ukitumia kipande kipya kwa kila jino unalopita
”flossing”
Fizi zinapovuja damu tafuta msaada wa daktari kama
Panga kumwona daktari kama:
- Kama fizi zako zinaendelea kuvuja damu baada ya kujaribu njia zote tulizoeleza hapa bila mafanikio kwa siku 7-10
- Kama una dalili nyingine zozote
Leave feedback about this