TATIZO LA KUCHEZA KAMARI:Sababu,dalili,matibabu

Maelezo ya jumla

Tatizo la kucheza kamari (pathological gambling) ni hali ya kushindwa kujizuia kucheza kamari. Kushindwa kuzuia msukumo wa kutaka kucheza kamali kunaweza kusababisha matatizo makubwa ya kibnafsi na kwa jamii pia.

Ni zipi dalili tatizo la kucheza kamari?

 • Watu wenye tatizo la kucheza kamari mara nyingi wanaona aibu au kujisikia hatia, na kwa sababu hii hawapendi watu wengine wajue kuwa wana tatizo.
 • Shishirikisho la matatizo ya akili la Marekani linamtambua mtu kuwa ana tatizo la kucheza kamari kama ana tano au zaidi ya dalili zifuatazo:
  • Anafanya uhalifu ili kupata pesa ya kucheza kamari
  • Anajisikia vibaya au kutokutulia akijaribu kupunguza au kuacha kucheza kamari.
  • Anacheza kamari ili kukwepa matatizo au hisia za huzuni au woga alionao
  • Anacheza kamari kwa pesa nyingi sana kwa kusudi la kujaribu kurudisha alizopoteza
  • Maejaribu mara kadhaa kupunguza au kuacha kabisa kucheza kamari lakini hajafanikiwa
  • Amepoteza kazi, mahusiano, au elimu au fursa fulani kwa sababu ya kucheza kamari
  • Anaongopa kuhusu muda na kiasi cha pesa anachotumia kucheza kamari
  • Anahitaji kukopa pesa kwa sababu ya kupoteza pesa nyingi
  • Anahitaji kucheza kamari kwa pesa nyingi sana ndiyo ajisikie raha
  • Anatumia muda mwingi akifikira kuhusu kucheza kamari, kama vile kujikumbusha kuhusu uzoefu au njia za zamani alizotumia kupata pesa nyingi ili kucheza kamari.

Ni nini husababisha tatizo la kucheza kamari?

 • Matatizo ya kucheza kamari kwa kawaida yanaanza mwanzoni mwa umri wa balehe kwa wanaume, na katikati ya miaka ya 20 na 40 kwa wanawake.
 • Matatizo ya kucheza kamari mara nyingi yanahusisha tabia ya kurudiarudia mambo. Mtu mwenye tabia ya kupenda kurudiarudia mambo wanapata shida sana kudhibiti au kuzuia hamu ya kucheza kamari.
 • Japo ina dalili zinazofanana na tatizo la akili linaloitwa obsessive compulsive disorder, tatizo la kucheza kamari ni tofauti.
 • Kwa watu wanaopatwa na tatizo la kucheza kamari, kwa mara chache wanaweza kufanya tatizo la kucheza kamari kuwa tabia. Msongo wa mawazo unaweza kusababisha matatizo ya kucheza kamari kuwa makubwa zaidi.

Ni wakati gani unapaswa kuomba msaada wa kitabibu?

Ongea na daktari kama unadhani una dalili za tatizo la kucheza kamari.

Utambuzi wa tatizo la kucheza kamari

Tathmini ya hali ya akili na historia inaweza kutumika kufanya utambuzi wa tatizo la kucheza kamari.

Uchaguzi wa matibabutatizo la kucheza kamari

 • Matibabu ya tatizo la kucheza kamri linaanza baada ya utambuzi kuwa una tatizo. Tatizo la kucheza kamari linaambatana na kukataa kuwa hauna tatizo. Watu wenye ugonjwa huu hukataa na huwa ngumu kukubali kuwa wana tatizo au wanahitaji matibabu.
 • Watu wengi wenye tatizo la kucheza kamari huanza matibabu kwa sababu ya shinikizo la watu walio karibu yao, wengi hawakubali wenyewe kupewa matibabu.
 • Chaguzi za matibabu ni pamoja na:
  • Cognitive behavioral therapy inaonekana kufaa
  • Njia zinazotumiwa kuacha kutumia aina nyingine za vilevi kama pombe, sigara zinaweza kutumika:
  • Zimefanyika tafiti chache kutumia dawa za kudhibiti sonona kwa matibabu ya tatizo la kucheza kamari. Matokeo ya mwanzo ya kutumia antidepressants na dawa aina ya opiod antagonists (naltrexone) kutibu tatizo la kucheza kamari yanaonesha kuwa zinaweza kudhibiti dalili. Lakini bado, haijafahamika kwa hakika kama zitawafaa watu wote.

Matarajio

 • Kama ilivyo kwa pombe au madawa ya kulevya, tatizo la kucheza kamari ni tatizo gumu kudhibiti kama usipopata matibabu na linaweza kuendelea kuwa kubwa zaidi.
 • Hata kama ukipata matibabu, ni kawaida kuanza tena kucheza kamri (kuirudia tabia ulioiacha). Hata hivyo,watu wengi wenye matatizo ya kucheza kamari wanaweza kuidhibiti wakipata matibabu sahihi.

Matatizo yanayoweza kutokea ukiwa na tatizo la kucheza kamari

Matatizo yanayoweza kutokea ni pamoja na:

Kupata matibabu yanayofaa itasaidia

Kuzuia

 • Kama unakaa katika maeneo yenye sehemu za kucheza kamari sana inaweza kuongeza uwezekano wa kuwa na tatizo. Kupunguza kukutana na sehemu za kucheza kamari au watu wanaocheza kamari kutasaidia kupunguza hatari.
 • Umma unazidi kuwekwa akaribu zaidi na nyenzo za kucheza kamari, lotteries, kucheza kamari mtandaoni, na casino kila kona. Kupata matibabu mapema unapoona dalili itasaidia kuzuia tatizo lisiwe kubwa zaidi.

Vyanzo

https://medlineplus.gov/compulsivegambling.html

Leave a Reply

Your email address will not be published.

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.

Jiunge Nasi