TATIZO LA KUKOSA HEDHI: Sababu,matibabu, kuzuia

Tatizo la kukosa hedhi ni nini?

Tatizo la kukosa hedhi ni hali ya kutokuanza kupata damu ya hedhi unapofikia balehe au damu kuacha kutoka kabla umri wa damu kukata kufika.

Tatizo la kukosa hedhi husababishwa na nini?

Chochote kinachovuruga kiwango cha homoni mwilini kinaweza kusababisha ukakosa hedhi. Hii inaweza kusababishwa na kukonda ghafla, kuanza kujinyima kula (diet) kwa ajili ya kupunguza uzito au mazoezi au msongo mkali wa mawazo. Hali hii inaweza pia kutokea kama una uke, mji wa mimba au ovari zenye matatizo. Lakini hii haimaanishi kuwa tatizo hili ni la kudumu. Unaweza pia kuwa na tatizo hili kama ovari hazifanyi kazi vizuri au kama kuna tatizo kwenye tezi dundumio iliyopo sehemu ya mbe ya shingo au kwenye tezi ya pituitary iliyopo kwenye ubongo.Tatizo la kukosa hedhi

Daktari anaweza kuagiza vipimo vifuatavyo?

Kwanza daktari atakuuliza kuhusu historia ya matibabu na dalili ulizonazo. Daktari anaweza kuagiza ufanye vipimo kama una miaka zaidi ya 15 na haujaanza kupata au kama umekosa kupata hedhi kwa zaidi ya miezi mitatu mfululizo. Itapendeza kama utakuwa unajua kama dada au mama yako alianza kupata hedhi akiwa na umri gani na kama walipata tatizo kama lako. Baada ya hapo, daktari anaweza kupima kiwango cha homoni mwilini. Anaweza pia kuagiza vipimo vingine maabara. Kwa baadhi ya visa, dakatari anaweza kuagiza upigwe picha ya ultrasound ya tumbo na nyonga.

Tatizo la kukosa hedhi linatibiwaje?

Inategemea na sababu. Wakati mwingine daktari anaweza kupendekeza upunguze uzito kama ni mkubwa au uongeze uzito kama umekonda sana. Hii inaweza kuhusisha mabadiliko kwenye mlo na mazoezi unayofanya. Daktari anaweza pia kukuandikia dawa za kusaidia afya ya mifupa na kurekebisha homoni mwilini. Baadhi ya wanawake wanahitaji madini ya ziada ya kalsiamu na vitamin Dtatizo la kukosa hedhi

Kujikinga na tatizo la kukosa hedhi?

  • Tunza kumbukumbu kwenye daftari ni lini damu ya hedhi inaanza na inadumu kwa muda gani.
  • Dhibiti uzito wa mwili na kula mlo kamili. Jitahidi kufanya mazoezi kwa angalau siku tano za wiki kwa angalau dakika 20 mpaka 60 kila siku. Kukimbia, kutembea au kuendesha baiskeli ni njia nzuri.
  • Kumbuka, bado unaweza kupata ujauzito japo hedhi haitoki mara kwa mara.

Vyanzo

https://medlineplus.gov/ency/imagepages/17088.htm

Leave a Reply

Your email address will not be published.

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.

Jiunge Nasi