TATIZO LA KULA SANA KUPITA KIASI

Maelezo ya jumla

Tatizo la kula sana kupita kiasi (binge eating) ni pale mtu anpokula kiasi kikubwa cha chakula katika kipindi kifupi ukilinganisha na ilivyo kawaida yake. Wakati anapokula kupita kiasi, mtu huyu hujihisi kuwa hawezi kujizuia.

Ni zipi dalili za tatizo la kula sana kupita kiasi?Kula sana kupita kiasi

 • Kwa kawaida, mtu mwenye tatizo la kula kupita kiasi:
  • Anakula kati ya kalori 5000 – 15000 kwa wakati mmoja
  • Anakula vitafunwa mara kwa mara, japo amekula milo mitatu kwa siku
  • Anakula kula sana siku nzima, sio tu kula kiwango kikubwa cha chakula kwa wakati mmoja
  • Anakula chakula chakula kingi kwa wakati mmoja, kwa mfano kila baada ya masaa 2
  • Mgonjwa hujihisi kuwa hawezi kujizuia au kuacha kula
  • Anakula chakula haraka sana kila anapokula
  • Anaendelea kula japo anajihisi kushiba au anakula mpaka tumbo linamuuma
  • Anakula japo hana njaa
  • Anakula mwenyewe (kwa siri)
  • Anajisikia vibaya, mwenye hatia, anaona aibu, au sonona baada ya kula
 • Tatizo la kula sana kupita kiasi mara nyingi husababisha mtu kuwa na uzito mkubwa wa mwili
 • Tatizo la kula sana kupita kiasi linaweza kutokea lenyewe au pamoja na ugonjwa wa ulaji unaoitwa bulimia. Watu wenye ugonjwa wa bulimia hula kiwango kikubwa cha chakula, hasa kwa siri. Baada ya kula kiwango hiki kikubwa cha chakula, wanajilazimisha kutapika au wanatumia dawa za kusaidia kuharisha.

Ni nini husababisha tatizo la kula sana kupita kiasi?

Sababu ya kula sana kupita kiasi haifamiki. Hata hivyo, kula sana mara nyingi huanza wakati au baada tu ya kujinyima sana chakula/kujilazimisha kufanya diet.

Ni wakati gani unapaswa kuomba msaada wa kitabibu?kula sana kupita kiasi

Onana na daktari kama unadhani una viashiria kuwa una tatizo la kula sana kupita kiasi au una ugonjwa bulimia wa kula sana na kisha kujitapisha au kutumia dawa za kusababisha uharishe.

Utambuzi wa tatizo la kula sana kupita kiasi?

 • Daktari atafanya uchunguzi wa mwili na kuuliza maswali kuhusu ulaji na dalili ulizonazo
 • Vipimo vya damu vinaweza kufanyika

Uchaguzi wa matibabu

 • Dawa mara nyingi hazihitajiki katika kutibu tatizo hili. Hata hivyo, daktari anaweza kukuandikia dawa za kudhibiti sonona kama unaonekana una woga au una ugonjwa wa sonona.
 • Tiba maongezi (talk therapy) inashauriwa.

Vyanzo

https://medlineplus.gov/ency/article/003265.htm

Leave a Reply

Your email address will not be published.

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.

Jiunge Nasi