Maelezo ya jumla
Karibu kila mmoja wetu anatokwa jasho kuliko kawaida anapokuwa anafanya mazoezi au wakati wa joto kali. Lakini kuna baadhi ya watu ambao wanatokwa jasho jingi kuliko kawaida muda wote. Mara nyingi kutokwa jasho huongezeka sana wakati wa balehe, lakini kwa baadhi ya watu kunaweza kuendelea maisha yote. Na kwa sababu hiyo kusababisha harufu mbaya ya mwili ambayo inaweza kuharibu mahusiano kazini na hata ya kijamii. Watu wanaotokwa na jasho jingi pia wanakuwa na hatari ya kupata magonjwa ya ngozi yanayosababishwa na fangasi.
Japo watu wengine wamezaliwa na hili tatizo, mambo mengine yenye mchango mkubwa katika kulisababisha ni msongo wa mawazo au uoga ulipitiliza. Tatizo hili pia huwa linawapata wanawake unapofikia wakati wa damu kukata au kama una tatizo la tezi dundumio)
Ni vizuri kumwona daktari kama:
- Unaona unatokwa jasho kwa muda mrefu au jingi kuliko kawaida
- Kama unaona uzito wako wa mwili unapungua
Unaweza kufanya mambo yafuatayo kupata nafuu
Unaweza kufanya mambo yafuatayo ili kujaribu kupunguza kutokwa jasho sana na kupunguza harufu mbaya ya mwili
- Jaribu kuoga angalau mara moja kwa siku kwa kutumia maji ya uvuguvugu (maji yasiwe ya moto). Jikaushe vizuri kwa taulo baada ya kuoga
- Jaribu kutumia dawa za kupunguza kutokwa jasho (antiperspirant) au unaweza kutumia antiperspirant ambayo imeongezwa deodorant ili kupunguza harufu mbaya ya mwili pia. Ukitumia antipersipirant inafanya kazi ya kuziba vijitundu vinavyotoa jasho kwa hiyo jasho linapungua, na deodorant kazi yake ni kuwaharibu bakteria ambao huwa wanasababisha harufu mwilini. Bidhaa nyingi ambazo ziko madukani huwa zina huu mchanganyiko kwa pamoja. Kwa hiyo jipake baada ya kuoga. iwapo ngozi yako itakuwa irritated, yaani kupata harara baada ya kuzitumia, jaribu kutafuta aina ya bidhaa ambazo siko kali sana ambazo hazileti mzio kwako (hypoallergenic). Kwenye miguu pia kuna powder maalumu zenye deodorant, kwa hyo zitumie kama unauhitaji.
- Kama ukiona hizi bidhaa za kawaida hazikusaidii, kuna mchanganyiko maalumu wa Aluminum chloride ambao huwa unatumika kwa hali kali sana. Huwa inapatikana kwa roll-on , jipake kwenye ngozi safi wakati wa usiku kabla ya kulala. Unaweza kuoga kesho yake asubuhi. Ukijipaka huu mchanganyiko mara moja, unaweza kuzuia kutokwa jasho kwa siku nyingine 3 au zaidi. Ila inabidi kuwa makini usipake huu mchanganyiko sehemu yenye kidonda au kama umwenyoa hivi karibuni, usipake pia.
- Unapaswa pia kuvaa nguo na nguo za ndani safi kila siku. Ni vizuri ukavaa nguo zenye nyuzi za asili kama vile pamba na ni muhimu kuepuka nguo zinazobana sana
- Kama miguu yako inapata jasho pia, vaa viatu baada ya kuvaa soksi zuilizotengenezwa kwa pamba, na
ukumbuke kuzibadilisha mara kwa mara. Kama inawezekana vaa ndala/sandals au tembea peku kila inapowezekana
- Kunywa maji angalau glasi 8 kwa siku ili kurejesha maji yanayopotea. Jaribu kupunguza pombe, na vinywaji vyenye caffeine kama kahawa, hasa vikiwa vya moto.
- Epuka kula vyakula vyenye viungo vikali kama pilipili, kwa sababu vinaweza kusababisha utokwe jasho, lakini pia epuka vitungu maji au swaumu kwa sababu ya harufu yake.
- Kama unatokwa jasho sana ukiwa na woga, endelea kuwa nasi nitakupatia njia za kupunguza msongo hivi karibuni
- Na mwisho, kama una uzito mkubwa, jaribu kuupunguza
Mwone daktari kama:
- Unaendelea kusumbuliwa na hili tatizo hata baada ya kufanya yote niliyokueleza
- Kama una dalili nyingine zinazoambatana na kutokwa jasho
Leave feedback about this