TATIZO LA KUVUJA/KUTOKWA MAZIWA KWENYE MATITI

Tatizo la kuvuja/kutokwa maziwa kwenye matiti?

Tatizo la kuvuja/kutokwa maziwa kwenye matiti ni tatizo la kuvuja maziwa kutoka kwenye matiti na wakati haunyonyeshi au linalotokea angalau mwaka mmoja baada ya kuacha kunyonyesha. Kwa kawaida maziwa huvuja kutoka kwenye matiti yote, lakini kwa baadhi yanaweza kutoka kwenye titi moja tu. Maziwa yanaweza kutoka yenyewe au ukigusa matiti. Wanaume wanaweza kupata tatizo hili pia, lakini mara nyingi linawapata wanawake .

Nini husababisha tatizo la kuvuja/kutokwa maziwa kwenye matiti

Kwa kawaida inasababishwa na kuongezeka kwa homoni ya prolactin mwilini. Homoni ya prolactin ni homoni inayoongeza utengenezaji wa maziwa. Homoni hii inatengenezwa na tezi iliyoko kwenye ubongo inayoitwa pituitari. Baadhi ya matatizo yanayoweza kusababisha ongezeko la homini ya prolactin mwilini ni pamoja na:

 • Ujauzito
 • Usumbufu wa sehemu ya kifua au chuchu – kuvaa nguo zinazoweza kusababisha ujikune, mashati yanayokwaruza kwaruza au sidiria/bra zinazobana
 • Kujikagua sana matiti – kuyashishika kila siku
 • Madawa – kama vile dawa za kutibu kurukwa na akili (antipsychotics), Dawa za kudhibiti sonona (antidepressants), vidonge vya kupanga uzazi, na baadhi ya dawa za kutibu shinikizo la juu la damu
 • Dawa za kienyeji/asili
 • Dawa za kulevya kama vile bangi na opiates
 • Kama tezi dundumio (tezi iliyoko sehemu ya mbele ya shingo) haifanyi kazi vizuri – hypothyroidism
 • Ugonjwa wa figo
 • Uvimbe kwenye tezi ya pituitari iliyoko kwenye ubongo (Uvimbe unaosababisha tatizo la kuvuja maziwa kwa watu wengi unaitwa prolactinoma, ni uvimbe haujasababishwa na kansa)
 • Matatizo mengine kwenye hypothalamus ambayo ni sehemu ya ubongo inayofanya kazi ya kuiongoza pituitari inaweza kusababisha.
 • Kwa baadhi ya Watoto, homoni za mama zitaingia kwake akiwa tumboni na kusababisha atoe maziwa

Wakati mwingine sababu ya kuvuja/kutokwa maziwa kwenye matiti inaweza isipatikane

Tatizo la kuvuja/kutokwa maziwa kwenye matiti

Ni zipi dalili za ongezeko la kiwango cha homoni ya prolactin mwilini?

 • Kutokwa na majimaji meupe mazito kama maziwa kwenye chuchu (wakati mwingine yanaweza kuwa ya njano au kijani). Kama majimaji yanayotoka ni mekundu au yanaonekana yana damu, inawezekana sio tatizo la kuvuja maziwa. Daktari anaweza kuhitaji kukupima ili kujua sababu ni nini.
 • Maumivu ya kichwa (kama una uvimbe kwenye pituitari)
 • Uwezo wa kuona unabadilika (kama una uvimbe kwenye pituitari)
 • Kukosa damu ya hedhi au kama vipindi vya damu ya hedhi havitabiriki
 • Unakosa hamu ya kushiriki ngono
 • Unashindwa kusimamisha uume
 • Mifupa yako inakuwa myepesi na rahisi kuvunjika (Hii inasababishwa na kupungua kwa homoni za kike au kiume, homoni kama vile estrojeni au androjeni kunakosababishwa na ongezeko la homoni ya prolactin)

Mwone daktari kama una tatizo la kuvuja/kutokwa maziwa kwenye matiti kama:

Tatizo la kuvuja/kutokwa maziwa kwenye matiti

Utahitaji kufanya vipimo gani ukiwa na tatizo la kuvuja/kutokwa maziwa kwenye matiti?

Daktari anaweza kufanya vipimo vya damu ili kuona kama kiwango cha homoni ya prolactin kimeongezeka. Kama imeongezeka, vipimo vingine vinahitajika ili kutambua ni nini kinasababisha homoni ya prolactin kuongezeka. Vipimo kama vya ujauzito na vipimo vya kuangalia tezi dundumio (thyroid tests na vipimo vya kuangalia kazi ya figo hufanyika. Kama sababu maalumu haitapatikana, dakatari anaweza kuagiza upige picha ya MRI (Magnetic resonance imaging) ya kichwa kuangalia kama kuna uvimbe au tatizo lolote kwenye tezi ya pituitary.

Tatizo la kuvuja/kutokwa maziwa kwenye matiti hutibiwaje?

Matibabu kwa kawaida hutegemea kilichosababisha tatizo la kuvuja/kutokwa maziwa kwenye matiti. Kama tatizo hili halikusumbui, halihitaji matibabu. Kama kuna aina fulani ya dawa unayotumia na inasababisha tatizo hili, daktari anaweza kukuandikia dawa nyingine mbadala.

Watu wengi wenye matatio ya kuvuja maziwa kunakosababishwa na uvimbe sio kansa na hupona kwa kutumia dawa. Upasuaji huhitajika kwa mara chache sana.

Vyanzo

https://medlineplus.gov/ency/article/001515.htm

Leave a Reply

Your email address will not be published.

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.

Jiunge Nasi