TATIZO LA NGOZI KAVU AU KUPASUKA

Maelezo ya jumla

Ngozi kavu sana au kupasuka: Ngozi yako inapokosa unyevu inaanza kuwasha, kukakamaa na inakuwa dhaifu na rahisi kupasuka. Ngozi inaweza kuonekana nyekundu, yenye mikunjomikunjo na kuwa kama una magamba, na katika hali kali sana inaweza kupasuka kabisa na kuvimba. Sehemu za miguu, mikono na mgongo ndio zenye uwezekano mkubwa kuwa na ngozi kavu kwa sababu sehemu hizi hazitengenezi mafuta mengi ya kulainisha ngozi. Kadri umri unavyoongezeka na ngozi yako inazidi kuwa kavu zaidi, hasa damu ya hedhi inapokata. Unaweza pia kuwa na ngozi inayouma, yenye mikunjo na iliyopasuka kwenye uso wako kama hali ya hewa ni kavu, baridi au kama uso wako unalowa mara kwa mara na haujikaushi vizuri.

Unachoweza kufanya unapokuwa na ngozi kavu

ngozi kavu
Water based cream

Jaribu kufanya mambo yafatayo ili kupunguza shida inayoletwa na kuwa na ngozi kavu inayowasha na kuboresha mwonekano wako.

  • Oga si zaidi ya mara 1 kwa siku kwa kutumia maji ya uvuguvugu, maji yasiwe ya moto. Usitumie sabuni zenye dawa au zenye perfume kali (zinaondoa mafuata)
  • Tumia moisturizer cream au mafuta badala ya sabuni –mosturizers zinaweza kutumika wakati wa kuoga na kuiweka ngozi yako kuwa nyororo. Unaweza kutumia water based cream or emulsifying ointiment, badala ya kutumia bidhaa zenye marashi makali unapooga, kisha jimwagie maji ili itike yote. Usijifute maji kwa taulo baada ya kuoga, badala yake jipeti ili kujikausha, hii itasaidia kuaa unyevu kidogo kwenye ngozi yako. Baada ya hapo jipake mafuta (petroleum jelly) ili kuubakiza huo unyevu kwenye ngozi. Unaweza kuendeea kutumia moisturizer mara kwa mara kwa siku nzima ili kuhakikisha ngozi yako haikauki, hasa kwenye mikono na uso, hasa baada ya kunawa au kama uko nje kwa muda mrefu wakati wa baridi. Ni vizuri kuwa na chupa ya moisturizer ndani ya nyumba na kazini ili uendelee kuitumia

Kuzuia ngozi kavu au kupasuka kwa ngozi

Unaweza kupunguza uwezekano wa kuwa na ngozi kavu kwa kufanya mambo yafuatayo

  • Kwa wale wenzetu waokaa maeneo yenye baridi, kuwa makini hau – overheat nyumba yako, kama inawezekana funga humidifiers au radiators
  • Vaa gloves unapokuwa ukifanya usafi wa ndani ya nyumba au gloves wakati wa kufanya kazi kwenye bustani au kazi nyingine unazofanya nje
  • Punguza kukaa kwenye jua
  • Suuza vizuri nguo zako baada ya kuzifua

Kama una ngozi tafuta msaada wa daktari kama:

  • Kama bado una ngozi kavu, iliyo na makunyanzi baada ya kujaribu yote haya niliyosema
  • Kama ngozi yako imevimba au inatokwa na damu

Vyanzo:

https://medlineplus.gov/ency/article/000835.htm

Leave a Reply

Your email address will not be published.

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.

Jiunge Nasi