TATIZO LA SAUTI KUKWARUZA AU KUPOTEA

TATIZO LA SAUTI KUKWARUZA AU KUPOTEA

 • February 13, 2021
 • 0 Likes
 • 91 Views
 • 2 Comments

Maelezo ya jumla

Tatizo la sauti kukwaruza au kupotea ”hoarsness of voice” ni shida inayokera, sauti yako inakua inakwaruza kwaruza na inakuwa ngumu wewe kusikika unapoongea. Sababu ya kawaida huwa ni kuvimba kwa sanduku la kutengenezea sauti ‘’voice box’’ kwa sababu ya maambukizi kama vile mafua. Koo lako linaweza kuwa linawasha au kuuma na unaweza kuwa unahisi kama kuna uvimbe kooni. Unaweza kupoteza sauti yako ghafla kwa sababu ya matumizi mabaya ya sauti – kwa mfano kama unaongea kwa nguvu sana au unashangilia kwa nguvu sana wakati wa mechi ya mpira wa miguu. Ukiona tatizo la kukwaruza kwaruza sauti linaanza taratibu linaweza kuwa limesababishwa na matumizi mabaya ya sauti, kuvuta sigara au kucheua kwa asidi ya tumbo ambayo pia inasababisha kiungulia na kusumbua sanduku la kutengenezea sauti kooni. Kwa kesi chache tu, kukwaruza kwaruza kwa sauti kunaweza kuwa dalili ya mwanzo ya kansa ya koo.

Unachoweza kufanya wewe mwenyewe

Kwa kawaida tatizo la kukwaruza au kupotea kwa sauti huwa ni la muda na huwa halidumu zaidi ya wiki moja. Ukifuata njia zifuatazo itasaidia kurudi haraka kwa sauti yako

 • Pumzisha sauti yako kadri inavyowezekana. Usiongee au kunong’oneza. Kunong’oneza kunaweza kusababisha misuli ya koo kukaza zaidi kuliko hatanukiongea kawaida.
 • Kunywa maji ya kutosha ili kupooza koo lako, kunywa angalau glass 6-8 za maji ili kuepuka koo kukauka sana. Usinye vinywaji vyenye caffeine kama vile kahawa, cola, chai au pombe
 • Kula vyakula laini ambavyo vitakuwa rahisi kumeza
 • Epuka kukaa maeneo yaliyo makavu sana au yenye moshi mwingi ambao unaweza kukausha zaidi koo na kusababisha hali ya sauti kuwa mbaya zaidi
 • Kama koo lako linauma sana, tumia dawa za kupunguza maumivu, madawa kama vile ‘’acetaminophen’’ yatasaidia kupunguza maumivu ya koo na kukwaruza kwaruza kwa sauti
 • Unaweza pia kujifukiza ili kupunguza kuvimba kwa koo na kuongeza unyevu kooni. Weka maji ya moto kwenye bakuli na kisha chukua kitambaa jifunike kichwani ukiwa umeinamia maji hayo ya moto (yasiwe yanachemka yakakuunguza). Vuta pumzi kupitia pumzi zako ili kuruhusu mvuke uingie
 • Usi-gogomoe ‘’gargling’’ – haisaidii, madawa ya kikohozi pia hayasaidii kurudi kwa sauti pia

  Kugogomoa

Mwone daktari kama

Kama una tatizo la sauti kuwaruza au kupotea panga kumwona daktari kama:

 • Kama sauti yako bado inakwaruza kwa zaidi ya wiki 2 hata baada ya kufuata ushauri ulio hapo juu
 • Kama sauti yako inakwaruza au imesha na unapata shida ya kupumua au unapata shida kumeza

Kuzuia

Unaweza kulinda koo lako kama unapata tatizo la sauti kukwaruza au kupotea mara kwa mara. Jaribu kufanya mambo yafuatayo ili kupunguza  uwezekano wa kujirudia

 • Kunywa mai angalau glass 6-8 za maji kwa siku. Weka chupa ya maji karibu yako ukiwa kazini au nyumbani, piga pafu ndogo ndogo kila wakati
 • Kama kazi yako inahusiana na kuongea na watu darasani au kwenye kikundi, jitahidi usiongee kwa nguvu au kukaza sana sauti. Panga makundi madogo madogo na kaeni akibu. Kama unapanga kuongea na kundi kubwa omba kipaza sauti
 • Kupayuka au kuongea kwa nguvu kunaongeza mkazo mkubwa kwenye misuli ya kooni, jaribu kudhibiti hasira au wasiwasi wako kama unakufanya utumie vibaya sauti yako
 • Acha kuvuta sigara na epuka kukaa kwenye mazingira yenye moshi mwingi
 • Jitahidi usikohoe au kusafisha koo lako kwa nguvu
 • Jaribu kuvuta pumzi kupitia kwenye pua zako. Ukivuta hewa ya baridi na kavu kupitia kwenye mdomo unasababisha mdomo na koo kukauka na kusababisha tatizo liwepo
 • Kama unaishi eneo lenye baridi sana na unahitaji kupasha chumba chako tumia ‘’humidifier’’ au chukua bakuli la maji liweke karibu na ‘’radiator’’ ili kuongea unyevu chumbani

Vyanzo

https://medlineplus.gov/ency/article/003054.htm

 

 

 

 • Share:

2 Comments

 •  2 wiki ago

  Thanks dr KWA elimu… Wikielimu n fire 💪

  •  2 wiki ago

   Asante sana Dr. , karibu tuuelimishe umma

Leave Your Comment