Matumizi ya tovuti
WikiElimu , Inc inaendesha tovuti ya www.wikielimu.com inayofuata sera hii ya matumizi. Tunatoa huduma inayowezesha watoa huduma kutoa huduma ya afya mtandaoni. Watumiaji huwezeshwa kutoa historia ya kimatibabu na kuwasiliana na watoa huduma wa afya ili kupata huduma ya afya. Unapoamua kutumia tovuti yetu, basi umekubali kufuata na kutekeleza sera ya matumizi ya WikiElimu. Kama haungependa kufuata na kutekeleza yaliyo katika sera hii, tafadhali usitumie tovuti hii au huduma zetu nyingine.
Huduma za kiafya
Watoa huduma wanaotoa huduma katika tovuti yetu ya WikiElimu wanajitegemea, ni wataalamu waliobobea na kusajiliwa na mabaraza ya taaluma husika. WikiElimu inc. Haitoi huduma ya afya na haina leseni ya kutoa huduma nyingine yoyote, na haiingilii utendaji kazi wa mtaalamu wa afya au mtaalamu mwingine, kila mtaalamu anawajibika kutoa huduma kwa kufuata miongozo na maadili ya taaluma yake. WikiElimu na washiika wake wanaoitangaza hawatawajibika kwa ushauri wowote usiofaa utakaotolewa na mtaalamu yoyote kupitia tovuti yao.
Maudhui yaliyomo kwenye tovuti
Maudhui yaliyomo kwenye tovuti (isipokuwa taarifa unazopata moja kwa moja kutoka kwa mtaalamu wa afya) yasichukuliwe kama ushauri wa kitabibu, maudhui yote, kurasa na makala zote zimekusudiwa kutoa elimu na si kama ushauri wa kitabibu.
Akaunti binafsi
Unaweza kutumia huduma zetu bila kufungua akaunti yako binafsi. Lakini kama itahitajika, utapaswa kuweka jina lako kamili, barua pepe, namba ya siri na taarifa nyingine muhimu zitakazohitajika. Ili kuunda akaunti unapaswa kuwa na umri zaidi ya miaka 18. Unakubali kuwa taarifa zote utakotoa wakati wa usajili wa akaunti na utakazoendelea kutoa wakati wa matumizi zitakuwa sahihi kwa kadri unavyojua wakati wote. Haupaswi kugawa au kuchangia akaunti au neno la siri na mtu mwingine au kufungua akaunti zaidi ya moja. Una wajibu wa kutunza namba yako ya siri ili kulinda shughuli zote zinazofanyika katika akaunti yako. WikiElimu inabakiza uhalali na uwezo wa kuchukua hatua yoyote inayoona inafaa na kukubalika ili kulinda usiri wa tovuti na akaunti yako. WikiElimu haitawajibka iwapo utapata madhara au hasara yatakayotokana na matumizi yako mwenyewe au mtu mwingine. Usitumie akaunti ya mtu mwingine
Watoto wanapotumia huduma zetu
Huduma zetu zipo tayari kwa kutumiwa na watoto, lakini hawataruhusiwa kuwa washirika wa moja kwa moja. Watoto hawataruhusiwa kutumia huduma zetu bila uangalizi wa mzazi au mlezi. Kama utajisajili kama mzazi au mlezi kwa niaba ya motto, utawajibika kutekeleza sera zoe za WikiElimu.
Haki ya kurekebisha
Tunabakiza uwezo wa kubadili, kuongeza au kufuta vipengele katika sera hii ya matumizi kwa wakati wote wa matumizi. Kuendelea kutumia huduma zetu hata baada ya kupata taarifa ya mabadiliko itaashiria kuwa uko tayari kufuata na kutekeleza mabadiliko yaliyowekwa.