Watoto

TETEKUWANGA:Sababu,dalili,matibabu

tetekuwanga

Maelezo ya jumla

Tetekuwanga (Chicken pox) ni maambukizi ya virusi yanayosababisha mtu kupata malengelenge yanayowasha mwili mzima. Tetekuwanga ulikuwa ugonjwa uliowapata watoto wengi sana kabla ya kugunduliwa kwa chanjo

Je, nini dalili za tetekuwanga?

 • Watoto wengi wenye tetekuwanga huwa na dalili zifuatazo kabla ya kutokea kwa vipele:
 • Upele wa tetekuwanga hutokea siku 10 hadi 21 baada ya kukutana na mtu mwenye ugonjwa huo. Mtoto hutokewa na vima-lengelenge vidogo kati ya 250 mpaka 500 vinavyowasha, vinavyozungukwa na madoa mekundu kwenye ngozi.
 • Malengelenge mara nyingi hutokea usoni, kifuani, mgongoni, kichwani na kisha mwili mzima huanza kuwasha
 • Baada ya siku moja au mbili, malengelenge huwa na weupe na kisha kutengeneza kigaga. Malengelenge mapya hutokea kwa makundi. Mara nyingi hutokea kwenye kope za macho, mdomo na uke.
 • Malengelenge huwatokea watoto wenye ukurutu
 • Huwa hakuna makovu yanayotengenezeka, isipokuwa kama mgonjwa alipata maambukizi ya bakteria baada ya kujikuna.
 • Licha ya kupata chanjo, watoto wengine bado wanaweza kupata tetekuwanga. Kesi za aina hii ya tetekuwanga huwa si kali sana na hupona haraka. Aina hii ya kesi ni ngumu kuzitambua. Lakini bado watoto hawa wanaweza kuwaambukiza wengine.

Ni nini husababisha Tetekuwanga?tetekuwanga

 • Kwa watoto,tetekuwanga husababishwa na virusi wanaoitwa Varicella-zoster. Aina hii ya virusi husababisha ugonjwa wa mkanda wa jeshi (herpes zoster) kwa watu wazima.
 • Ugonjwa huu husambaa kwa urahisi, kwa kugusa au kushika majimaji yanayotoka kwenye malengelenge ya mtu mwenye ugonjwa huu au kama mtu mwenye tetekuwanga atakohoa au kupiga chafya karibu yako. Watu wenye dalili za kadri wanaweza kuambukiza wengine.
 • Mtu mwenye ugonjwa huu anaweza kuambukiza watu wengine siku ya 1 au 2 kabla ya malengelenge kuonekana. Mtu mwenye tetekuwanga anaweza kuambukiza wengine mpaka malengelenge yote yanapokauka
 • Kesi nyingi za tetekuwanga huwapata watoto wenye umri chini ya miaka 10. Ugonjwa huwa wa kadri, japo wakati fulani unaweza kusababisha matatizo makubwa. Watoto wakubwa na watu wazima hupata ugonjwa mkali zaidi kuliko watoto wadogo.
 • Watoto waliozaliwa na akina mama waliokwisha kuugua ugonjwa huu au waliopokea chanjo, uwezekano wa kupata tetekuwanga kabla ya mwaka 1 hupungua sana. Hata hivyo, kama watoto hawa wakipata tetekuwanga, huwa na dalili za kadri tu. Hii ni kwa sababu kinga ya mwili ya mama huwalinda watoto hawa kwa kipindi hicho. Watoto walio chini ya mwaka 1 waliozaliwa na akina mama ambao hawajawahi kuugua  au ambao hawajawahi kupata chanjo, wanaweza kuugua ugonjwa wenye dalili kali sana.
 • Kama unaugua ugonjwa fulani au kama unatumia madawa fulani yanayopunguza kinga ya mwili kama tibakemikali au steroids yanaweza kusababisha uugue ugonjwa wenye dalili kali sana za tetekuwanga.

Nani yuko kwenye hatari zaidi?

Kwa sababu tetekuwanga ni ugonjwa wa kuambukiza, mtu yeyote aliye karibu na mgonjwa yuko kwenye hatari ya kuambukizwa

Utambuzi

Mtoa huduma wa afya anaweza kugundua kuwa una tetekuwanga kwa kuangalia upele na kuuliza maswali kadhaa kuhusu historia yako. Vi- malengelenge vidogo kwenye kichwa mara nyingi huthibitisha utambuzi huu.

Wakati gani utafute matibabu ya haraka?

Fika kwenye kituo cha afya kama unadhani mwanao ana tetekuwanga au kama mwanao ana zaidi ya miezi 12 na bado hajapata chanjo dhidi ya tetekuwanga

Uchaguzi wa matibabu ukiwa na tetekuwanga

Matibabu mara nyingi hufanyika ili kumpunguzia mgonjwa taabu na shida. Jaribu kufanya yafuatayo:

 • Inashauriwa kuepuka kujikuna au kujisugua maeneo yanayowasha.
 • Hakikisha kucha zako ni fupi ili kuepuka kujichubua ngozi unapojikuna
 • Vaa nguo nyepesi zisizobana na epuka kuvaa nguo nzito zinazokwaruza katika maeneo yanayowasha, hii inaweza kusababisha ujikune zaidi.
 • Oga kwa kutumia maji ya vuguvugu na sabuni na kisha jisuuze vyema baada ya kuoga.
 • Mafuta ya majimaji (moisturizer) husaidia kulainisha na kupunguza ukavu wa ngozi.
 • Epuka kukaa kwenye joto kali na maeneo yenye unyevu mwingi
 • Dawa aina ya Antihistamine kama vile diphenhydramine  hutumika kupunguza muwasho, lakini unapaswa kutambua kuwa zinaweza kusababisha matokeo mabaya kama usingizi.
 • cream ya hydrocortisone pia hutumika sana kupunguza muwasho kwenye maeneo yanayowashwa
 • Madawa yanayothibiti virusi vinavyosababisha tetekuwanga yanaweza kutumika ndani ya masaa 24 ili kupata matokeo bora
 • Watu wazima na vijana, ambao wako kwenye hatari ya kupata dalili kali zaidi, wanaweza kufaidika na matumizi ya dawa za kudhibiti virusi. Watoto wenye afya njema hawahitaji dawa hizi za kudhibiti virusi -kwa sababu hawana dalili kali.
 • Dawa za kudhibiti virusi huwafaa zaidi watu wenye magonjwa ya ngozi (kama vile ukurutu), matatizo ya mapafu (kama vile pumu) au wanaotumia steroids
 • USIMPATIE mgonjwa wa tetekuwanga asprin au Matumizi ya asprin yanaweza kusababisha ugonjwa mbaya unaoitwa Reye’s syndrome. Ibuprofen imehusishwa na ugonjwa wenye dalili kali zaidi. Acetaminophen (paracetamol) inaweza kutumika.
 • Matumizi ya glavu au soksi mikononi ni muhimu ili kupunguza maambukizi yanayotokana na kujikuna hasa usiku unapokuwa umelala.
 • Watoto wenye tetekuwanga hawapaswi kwenda shule au kucheza na wengine mpaka malengelenge yatakapokauka kabisa. Watu wazima pia hawaruhusiwi kurudi kazini mpaka malenglenge yatakapokauka.
 • Dawa za kudhibiti virusi zinaweza kutolewa kwa watu wanoishi na mgonjwa nyumba moja. Hii ni kwa sababu wako kwenye hatari zaidi ya kuambukizwa na wanaweza kupata dalili kali zaidi.

Nini cha kutarajia ukiwa na tetekuwanga?

 • Katiaka hali ya kawaida, mtu hupona bila matatizo yoyote.
 • Baada ya kupata tetekuwanga, virusi hubakia mwilini maisha yako yote. 1 kati ya watu wazima 10 hupata mkanda wa jeshi virusi hivi vinapojiinua wakati wa msongo au wakati wa upungufu wa kinga ya mwili.

Matatizo yanayoweza kutokea

Kwa mara chache, maambukizi ya bakteria yanaweza kusababisha ubongo kuvimba-encephalitis. Matatizo mengine yanayoweza kutokea ni pamoja na:

 • Reye’s syndrome (huhusishwa na matumizi ya Aspirini).
 • Kuvimba kwa misuli ya moyo
 • Nyumonia
 • Yabisi kavu
 • Wanawake wajawazito wenye tetekuwanga wanaweza kuwaambukiza watoto wakiwa tumboni. Watoto wachanga wako kwenye hatari ya kupata maambukizi yenye dalili kali sana
 • Matatizo yanayowapata watu wengi ni pamoja na maambukizi kwenye ngozi, ambayo kama hayatatibiwa yanaweza kusababisha nyumonia au maambukizi kwenye damu.

Kuzuia tetekuwanga

 • Funika mdomo wako unapokohoa au kupiga chafya
 • Hakikisha kuwa nguo na taulo zinazotumiwa na mgonjwa wa tetekuwanga hazitumiwi na mtu mwingine
 • Nawa mikono yako mara kwa mara na kila baada ya kumhudumia mgonjwa wa tetekuwanga
 • Epuka kumpeleka mtoto shuleni au maeneo ya mkusanyiko ambapo mtoto anaweza kukutana na wengine-epuka kusambaza maambukizi.
 • Kwa sababu tetekuwanga inaweza kusambaa kwa hewa hata kabla upele na malengelenge hayajatokea, inaweza kuwa ngumu kujikinga.
 • Chanjo ya kuzuia tetekuwanga kwa watoto ni muhimu
 • Kwa kawaida chanjo huzuia kabisa ugonjwa wa tetekuwanga au hufanya ugonjwa huo kuwa na dalili za kawaida.
 • Ongea na mtoa huduma wa afya kama unadhani mwanao amekutana na mtoto mwenye tetekuwanga. Kupewa chanjo mara baada tu ya kuambukizwa kunaweza pia kupunguza makali ya dalili.

Vyanzo

http://www.nlm.nih.gov/medlineplus/ency/article/001592.htm

  • 2 years ago (Edit)

  Dr elimu inatufika asante uzidi kubalikiwa

   • 2 years ago

   Asante kwa mrejesho, endelea kuwa nasi

  • 2 years ago (Edit)

  Ni elimu nzuri,
  Natumaini itakuwa msaada mkubwa kwa kukuza uelewa wa watu kuhusu tetekuwanga

   • 2 years ago

   Asante, endelea kuwa nasi

Leave feedback about this

 • Quality
 • Price
 • Service

PROS

+
Add Field

CONS

+
Add Field
Choose Image
Choose Video
X