Maelezo ya jumla
Kila mmoja wetu anajihisi kuchoka baada ya shughuli za kimwili au kazi ngumu. Kulala vizuri usiku mara nyingi ni tiba kamili ya uchovu, lakini wakati mwingine utajikuta unahisi uchovu unakuwepo kwa siku kadhaa na unaweza kukuta shughuli zako zinaharibika kabisa.
Sababu ya wazi kabisa ya uchovu huwa ni kukosa usingizi, lakini pia, unaweza kuwa na uchovu kama una msongo wa mawazo, unajihisi kushuka moyo au kama unaomboleza baada ya kufiwa au kuachishwa kazi na matatizo kama hayo.
Kama hauli mlo wa afya na haufanyi mazoezi, mara nyingi ni sababu pia ambazo zinaweza kuchangia. Magonjwa yanayosababishwa na virusi kama vile mononucleosis na mafua yanaweza kusababisha ukabakia mchovu kwa wiki kadhaa hata baada ya kupona.
Wakati mwingine uchovu unaweza kuwa unatokana na upungufu wa damu au matatizo ya tezi dundumio
Ni vizuri ukamwona daktari kama uchovu;
- Uchovu unakuwepo kwa muda mrefu na japo unalala vizuri tu
- Kama huwa unajihisi mchovu bila sababu ya msingi
Unaweza kufanya nini ukiwa na uchovu?
Kama unajihisi mchovu kila wakati, unaweza kufanya mambo yafuatayo ili kukusidia kupata nguvu tena
- Hata kama una kazi kiasi gani, pata wakati wa kulala vizuri usiku. Usifanye kazi sana siku za wiki ili ulipizie kwa kulala wakati wa weekend, ukifanya hivi inasababisha kupoteza routine ya usingizi wako, na hii itakuacha ukiwa mchovu zaidi.
- Hakikisha unapata kifungua kinywa asubuhi. Ongeza mbogamboga, matunda na nafaka ambazo hazijakobolewa kwenye mlo wako. Punguza vyakula vyenye mafuta mengi kama vile jibini na nyama nyekundu. Epuka pia kuongezea chumvi na sukari mezani.
- Jichunguze, angalia kama uzito wako ni mkubwa au kama umekonda sana. Kama unahitaji kupunguza uzito, punguza, kama unahitaji kuongeza uzito, fanya hivyo taratibu na kwa hatua.
- Jitahidi kupata hewa safi nje, usikae ndani tuu siku nzima. Fanya mazoezi mara kwa mara, hasa kama unafanya kazi ya ofisini ambayo haikushughulishi sana.
- Kama unahisi usingizi wakati wa mchana au unapokuwa unaendesha gari jaribu hii technique ‘ inaitwa ‘’power nap’’
- Nadhani kila mmoja wetu amewahi kusinzia mchana, hasa wakati unaendesh gari, hapa ndipo power nap inapohusika, kujilaza tu kwa muda mfupi kutakusaidia u- function vizuri zaidi.
- Unaweza ukajilaza kwa dakika 10-15, lakini hata dakika 5 za usingizi zitakuacha ukiwa vizuri zaidi. Kulala zaidi ya dakika 15 kutakusaidia lakini kunaweza kukuacha ukiwa umechoka na ukilala zaidi ya dakika 30, itasababisha usilale vizuri usiku.
- Ni vizuri kujilaza kila siku wakati huo huo ili mwili wako uzoee. Tumia alarm ambayo itakuamsha ili usipitilize na kulala muda mrefu zaidi ya ulivyopanga.
- Usijilaze wakati wa jioni au kusinzia unapokuwa unaangalia TV joini, ukifanya hivi itasababisha upate shida kulala usiku
- Kama unamaambukizi yanayosababishwa na virusi kama mafua, inaweza kuchukua wiki kadhaa kurudi katika hali yako ya kawaida. Kama unaweza omba ruhusa kutoka kazini au shuleni, pata muda wa kupumzika.
- Kama msongo wa mawazo umechangia kuleta uchovu, jaribu kutenga muda kwa ajili ya kujiburudisha au kuungana na watu unaowapenda kama familia au marafiki. Jaribu deep breathing exercise na relaxation exercise yatakusaidia, kama hauyafahamu, endelea kuwa nasi, nitakwambia jinsi ya kufanya hapahapa.
Ukiwa na uchovu mwone daktari kama
- Umejaribu njia hizi zote kwa wiki 2-3 bila mabadiliko au kama unaona kuna dalili nyingine zinajitokeza
Leave feedback about this