Maabara|Vipimo

UCHUNGUZI WA NJIA YA HAJA KUBWA KWA KIDOLE

Last Updated on October 13, 2023 by Dr Mniko

Digital rectal examination (DRE) ni uchunguzi wa njia ya haja kubwa kwa kidole unaofanywa na daktari au mtaalamu wa huduma ya afya.uchunguzi wa njia ya haja kubwa kwa kidole
Mgonjwa huwekwa katika mkao unaomruhusu daktari kufanya uchunguzi wa sehemu ya ndani ya njia ya haja kwa kutumia kidole cha mkono (mgonjwa anaweza kulala upande, anaweza kuchuchuma kwenye meza ya kupimia, anaweza pia kuinama kwenye meza, nk).  Daktari huingiza kidole kilichopakwa kilainishi kupitia kwenye mkundu ili kugusa na kuchunguza sehemu ya ndani ya rektamu.
Uchunguzi wa sehemu ya ndani ya haja kubwa kwa kutumia kidole ”DRE” haitoshi kuwa chaguo wakati wa kuchunguza saratani ya koloni na rektamu, kwa sababu kidole cha daktari hufikia 10% ya rektamu. Hata hivyo, kipimo hiki ni sehemu muhimu wakati wa uchunguzi wa magonjwa ya njia ya haja kubwa na rektamu.
Uchunguzi huu unaweza kutumika:

  • kwa ajili ya utambuzi wa uvimbe au saratani kwenye njia ya haja kubwa.
  • kwa wanaume, kwa utambuzi wa matatizo ya tezi dume.
  • kwa ajili ya utambuzi wa kibole (appendicitis) au matatizo mengine ya tumbo
  • Kwa kupima mkazo wa kizibo cha mkundu (sphincter anal), hasa mtu anapokuwa anashindwa kuzuia kinyesi au ana ugonjwa wa mfumo wa neva.
  • kwa ajili ya uchunguzi wa ugumu na rangi ya kinyesi (hasa kwa mtu aliyefunga choo)
  • kabla ya colonoscopy au
  • kutathmini bawasiri (haemorrhoids)
  • N.k
    Mikao wakati wa kipimo

    Vyanzo

  • https://medlineplus.gov/ency/article/003869.htm

Leave feedback about this

  • Quality
  • Price
  • Service

PROS

+
Add Field

CONS

+
Add Field
Choose Image
Choose Video
X