UFANYE NINI UNAPONYANYASWA KWENYE MAHUSIANO

Nitajuaje kama ninafanyiwa unyanyaswaji kwenye mahusiano?

Unaponyanyaswa kwenye mahusiano – unaweza kujihisi uoga au kutojiami unapokuwa pamoja na mwenzi wako. Unaweza kuwa katika mahusiano yenye unyanyasaji hata kama mwenzi wako hakupigi. Kuna aina nyingi ya unyanyasaji:

  • Unyanyasaji wa kimwili (kupigwa mwili, kupigwa ngumi, kupigwa mateke)
  • Unyanyasaji wa kingono (kubakwa, kulazimishwa kushiriki ngono)
  • Unyanyasaji wa kihisia (Kuitwa majina mabaya, kutukanwa, au kupewa vitisho)
  • Tabia ya kukudhibiti usiweze kufanya lolote (anakuzuia kuwa na pesa zako au hataki uwe na pesa, anakuzuia kutoka nje ya nyumba au kuingia ndani ya nyumba u kutumia gari)
Unaponyanyaswa kwenye mahusiano
 

Ninapaswa kujua nini unaponyanyaswa kwenye mahusiano?

Kufanyiwa vurugu na mwenzi ni kosa la jinai. Kama unanyanyaswa, kumbuka kwamba sio kosa lako, haujakosa kitu, kwa hiyo usijilaumu. Hakuna mtu anayepaswa kunyanyaswa. Wanawake wawili kati ya watano Afrika wamewahi kunyanyaswa kijinsia katika Maisha yao. Unyanyasaji katika mahusiano unaweza kutokea katika mahusiano ya aina yoyote – walioolewa au wanaochumbiana. Watu wa umri, rika, kabila, au kipato au elimu yoyote wanaweza kunyanyaswa katika mahusiano. Kama mpenzi wako anatumia pombe au madawa ya kulevya, yanaweza kusababisha hali kuwa mbaya zaidi.Unaponyanyaswa kwenye mahusiano

Ufanye nini unaponyanyaswa kwenye mahusiano

Zungumza swala hili na mtu unayemwamini (mwanafamilia, Rafiki, mchungaji, nesi au daktari). Jaribu kufahamu vilipo vielelezo vyako muhimu na vya Watoto wako kama ikitokea ukaamua kuondoka katika uhusiano huo. Vielelezo muhimu kama vile rekodi au kadi za benki, vyeti vya kuzaliwa, vitambulisho vya taifa, bima, kura na nyaraka nyingine muhimu. Weka vielelezo vyako mahala salama. Utavihitaji ili kupata pesa, makazi na huduma nyingine kwa ajili yako na Watoto wako. Weka mpango wa kwenda mahala salama, unaweza kwenda kwenye kambi za wanawake (kuna maeneo ziko karibu) au kwenye nyumba ya mwanafamilia.

Kama unahisi kuwa uko kwenye hatari kubwa, piga kelele kuomba msaada au piga simu polisi kama unaweza. Unaweza pia kuchukua hati ya mahakama ya kumkataza mtu huyo anayekunyanyasa kuwa karibu yako. Hii inaitwa ‘’order of protection’’.

Vyanzo

https://medlineplus.gov/ency/patientinstructions/000816.htm

Leave a Reply

Your email address will not be published.

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.

Jiunge Nasi