UGONJWA UNAOTOKANA NA KUWA KATIKA ENEO LILILO JUU SANA KUTOKA USAWA WA BAHARI

UGONJWA UNAOTOKANA NA KUWA KATIKA ENEO LILILO JUU SANA KUTOKA USAWA WA BAHARI

 • December 20, 2020
 • 1 Like
 • 26 Views
 • 0 Comments

Maelezo ya jumla

Ugonjwa unaotokana na kuwa katika maeneo yaliyo juu sana kutoka usawa wa bahari  (altitude sickness), huu ni ugonjwa unaowapata watu wanaopanda milima, wanaoruka angani kwa parachuti au wanaosafiri kwenda kwenye maeneo yaliyo juu sana kutoka usawa wa bahari (kwa kawaida juu sana kuliko futi 8000 u mita 2400).

Nini dalili za ugonjwa huu?

Dalili za ugonjwa wa kadiri unaotokana na kuwa juu sana kutoka usawa wa bahari ni pamoja na:

Dalili za ugonjwa mkali unaotokana na kuwa juu sana kutoka usawa wa bahari ni pamoja na:

 • Ngozi kugeuka rangi na kuwa ya bluu
 • Kubanwa kifua
 • Kuchanganyikiwa
 • Kukohoa
 • Kukohoa damu
 • Kusinzia sinzia ovyo
 • Kushindwa kutembea vizuri au kushindwa kutembea kabisa
 • Kushindwa kupumua au kuishiwa pumzi hata wakati umepumzika

Ni nini kinasababisha ugonjwa huu?

Ugonjwa unaotokana na kuwa katika maeneo yaliyo juu sana kutoka usawa wa bahari husababishwa na kupungua kwa mkandamizo wa hewa na kupungua kwa hewa ya okisijeni unaotokea kadiri unapokwenda juu kutoka usawa wa bahari. Dalili zinaweza kuwa za kadiri au zinaweza kuwa kali mpaka kutishia maisha, mfumo wa neva, mapafu, misuli, na moyo vinaweza kuathirika.

Mara nyingi dalili zake si kali. Lakini katika hali kali mapafu yanaweza kujaa maji na kusababisha upate shida kupumua. Hali hii hupunguza zaidi kiasi cha oksijeni kinachoingia katika damu na kwenye viungo na tishu za mwili. Ubongo unaweza pia kuvimba. Hii inaweza kusababisha kuchanganyikiwa, koma na kama hautatibiwa kifo.

Takribani asilimia 20 ya watu watapata dalili za kadiri wanapofikia futi 6,300 hadi 9,700, lakini katika usawa huu wa bahari ni nadra sana mapafu kujaa maji na kuvimba ubongo. Hata hivyo, watu wengi hupata dalili za kadiri wanapofikia futi14,000. Watu wengine wanapokaa katika usawa huu wa bahari, mapafu yao hujaa maji na kuvimba ubongo.

Nani yuko kwenye hatari zaidi?

Hatari ya kupata ugonjwa unaotokana na kuwa juu kutoka usawa wa bahari huongezeka kadiri kasi ya kupanda juu inavyoongezeka. Kadiri unavyopanda kwenda juu kwa haraka zaidi ndivyo na hatari ya kupata ugonjwa huu inavyoongezeka. Ukali wa ugonjwa huu unategemea pia unajikaza kiasi gani na kwa kasi kiasi gani unapanda kwenda juu. Watu ambao wanaishi kwenye au karibu na usawa wa bahari wako kwenye hatari kubwa ya kupata  ugonjwa huu.

Wakati gani utafute matibabu ya haraka?

Mwone mtoa huduma ya afya kama una dalili za ugonjwa unaotokana na kuwa juu sana kutoka usawa wa bahari, hata kama umepata nafuu baada ya kurudi/kushuka chini.

Omba msaada kufika kituo cha afya kama unapata shida kupumua au unaanza kupoteza fahamu, unakohoa damu au dalili nyingine kali. Kama hakuna mtu wa kukusaidia, jaribu kushuka haraka iwezekanavyo.

Utambuzi

Daktari atasikiliza kifua chako kwa kifaa cha kusikilizia ( stethoscope). Kifaa hiki humsaidia daktari kusikia sauti zinazoitwa crackles ambazo huashiria mapafu yamejaa maji.  Daktari anaweza kuagiza ufanye eksirei pia.

Uchaguzi wa matibabu

Tiba kuu ya ugonjwa huu ni kushuka chini, shuka chini ya usawa wa bahari kwa haraka na kwa usalama kadiri uwezavyo. Kama kuna oksijeni, mgonjwa apewe ya ziada. Watu wanaoumwa sana wanaweza kulazwa hospitalini.

Acetazolamide ni dawa inayosaidia upumuaji na kupunguza dalili zingine. Dawa hii inaweza kusababisha ukojoe sana. Unapotumia dawa hii, hakikisha unakunywa maji ya kutosha na usinywe pombe.

Mapafu yaliyojaa maji hutibiwa na oksijeni, dawa ya kudhibiti shinikizo la damu nifedipine na katika hali kali mashine ya kukusaidia kupumua.

Madawa aina ya steroid kama vile dexamethasone yanaweza kusaidia kupunguza uvimbe kwenye ubongo.

Nini cha kutarajia ?

Kwa sababu mara nyingi kesi hizi si kali sana, dalili hupungua haraka baada tu ya kurudi kwenye usawa wa bahari. Kesi kali sana zinaweza kusababisha kifo kwa sababu ya kushindwa kupumua na kuvimba kwa ubongo.

Katika maeneo ya mbali, hasa maeneo yasiyofikika kwa urahisi, uokoaji na huduma za dharura zinaweza kuchelewa sana au kushindwa kufika kabisa. Hali hii inaweza kuathiri matokeo.

Matatizo yanayoweza kutokea

Vyanzo

http://www.nlm.nih.gov/medlineplus/ency/article/000133.htm

Leave Your Comment