Magonjwa ya akili

UGONJWA WA AKILI: Sababu,dalili,matibabu,kuzuia

ugonjwa wa akili

Last Updated on October 12, 2023 by Dr Mniko

Ugonjwa wa akili ni nini?

Ugonjwa wa akili kwa kiasi kikubwa huathiri kufikiri kwa mtu, hali ya hisia na tabia, na kuvuruga uwezo wa mtu kufanya kazi au kutekeleza shughuli nyingine. Madhara kwa maisha ya mtu yanaweza kuwa makubwa.

Mtazamo wa jamii kuhusu ugonjwa wa akili?

Watu wengi, hufikiri kwamba ugonjwa wa akili unaweza kuwapata watu masikini, wajinga ua watu waliochanganyikiwa pekee. Lakini ukweli ni kwamba, mtu yeyote anaweza kupata ugonjwa wa akili. Ukianza kuona unaanza kutokufanya kazi vizuri, masomo, familia na mahusiano mengine ya kijamii, unaweza kuwa anakabiliwa na ugonjwa wa akili. Ugonjwa wa akili kama yalivyo magonjwa mengine, unatambuliwa na kutibiwa na wataalamu wa huduma za afya.

Ukweli kuhusu ugonjwa wa akili

ugonjwa wa akili

 • 10% ya watu wote duniani wanaishi na aina moja ya ugonjwa wa akili
 • Mtu anaweza kupata magonjwa ya akili tofauti tofauti katika vipindi tofauti tofauti vya maisha yake
 • Mtu anaweza kupata magonjwa ya akili zaidi ya moja kwa wakati mmoja
 • Baadhi ya watu wanapata ugonjwa wa akili mara moja tu na kupona kabisa
 • Kwa watu wengine, ugonjwa wa akili unaweza kuja na kuondoka mara kadhaa katika kipindi cha maisha yao

Mambo ambayo yanaathiri jinsi ugonjwa wa akili unavyoweza kukuathiri

Mgonjwa ya akili yanayopata watu wengiugonjwa wa akili

Ugonjwa wa sonona/kunyong’onyea

Sisi wote huwa tunajihisi vibaya au huzuni mara kwa mara – ni sehemu ya kuwa mwanadamu. Huzuni ni matokeo ya kitu fulani, kwa mfano kufukuzwa kazi. Sonona ina maana kwamba hisia ya huzuni huchukua muda mrefu kuliko kawaida, huathiri sehemu nyingi za maisha ya mtu na kushidwa kufurahia vitu walivyovizoea na kuvifurahia.

Dalili za ugonjwa wa sonona ni pamoja na;

 • Hisia ya huzuni na hasira
 • Kupoteza nia na uwezo wa kufurahia shughuli ulizokuwa unafurahia
 • Kuongezeka au kupungua kwa hamu ya kula
 • Kupata shida kupata usingizi au kulala kitandani siku nzima
 • Kuwa na hisia za woga na wasiwasi mwingi
 • Kujisikia vibaya, mwenye hatia na usiye na thamani
 • Kuwa na mawazo mabaya yaliyojaa giza, hii ni pamoja na mawazo ya kifo au kujiua
 • Maumivu ya kichwa, maumivu ya misuli
 • Kujitenga na marafiki au wanafamilia
 • Kuongezeka kwa matumizi ya pombe au dawa za kulevya
 • Kukosa kujiamini, kushindwa kufanya maamuzi na hasira

Ugonjwa wa wasiwasi uliozidiugonjwa wa akili

Kila mmoja wetu atajihisi mwenye wasiwasi katika kipindi fulani cha maisha yake, hata hivyo wasiwasi unaweza kuwa tatizo kama hisia za woga, wasiwasi na kutokujiamini zinadumu kwa muda mrefu  na kuanza kuathiri shughuli au maisha ya kila siku.

Baadhi ya dalili za mtu mwenye ugonjwa wa wasiwasi ni kama zifuatazo:

 • Kuwa na hisia kuwa huu ndio mwisho, hakuna namna
 • Hasira, kuchanganyikiwa
 • Kupata shida ya usingizi
 • Kuwa na mawazo ya wasiwasi na woga ambayo huwezi kuyadhibiti au kuyaondoa kichwani
 • Kupata shida kufanya maamuzi
 • Kuongeza matumizi ya pombe na dawa za kulevya
 • Kujisikia kuchanganyikiwa au kutojiamini unapokuwa mbele za watu
 • Kupata dalili za kimwili kama vile moyo kwenda mbio, maumivu ya kifua, kupaliwa, kichefuchefu na kizunguzungu

Ugonjwa wa akili na utumiaji wa pombe

Baadhi ya watu wanatumia pombe kama njia ya kujisahaulisha madhira yanayowakumba. Japo pombe na dawa za kulevya zinaweza kukupatia namna ya kujificha kwa muda mfupi, lakini kadri muda unavyokwenda, pombe na dawa za kulevya;

 • Husababisha dalili za ugonjwa wa sonona na wasiwasi kuwa mbaya zaidi
 • Husababisha matibabu yasifanikiwe
 • Huleta athari hasi katika Nyanja nyingine zote za maisha yako, kama vile kazi, familia na afya kwa ujumla
 • Inaweza kusababisha mtu kupata matatizo mengine yanayosababishwa na unywaji wa pombe au utumizi wa dawa za kulevya

Matibabu ya ugonjwa wa akiliugonjwa wa akili

Sehemu kubwa ya magonjwa ya akili yanaweza kutibiwa na kupona kabisa. Ni muhimu kupata matibabu mapema. Kadri matibabu yanavyowahi ndivyo na uwezekano wa kupona unavyoongezeka.

Ugonjwa wa akili, unatambuliwa na kutibiwa na wataalamu wa afya. Matibabu ya uhakika yanajumuisha kuonana na daktari wa magonjwa ya akili, kupata ushauri muhimu kuhusu ugonjwa wako, mikutano ya mara kwa mara ya wagonjwa na dawa. Matibabu yanatolewa kwa usiri sana.

Vyanzo

https://mhima.org.au/

Leave feedback about this

 • Quality
 • Price
 • Service

PROS

+
Add Field

CONS

+
Add Field
Choose Image
Choose Video
X