Magonjwa ya ndani ya mwili

UGONJWA WA CHIKUNGUNYA: Sababu,dalili,matibabu

Ugonjwa wa chikungunya

Last Updated on October 13, 2023 by Dr Mniko

Maelezo ya jumla

Ugonjwa wa chikungunya ni ugonjwa unaosababishwa na virusi wanaoenezwa na mbu.

Ni zipi dalili za ugonjwa wa chikungunya

 • Watu wengi wanaoambukizwa ugonjwa wa chikungunya wanapata dalili kadhaa
 • Dalili kwa kawaida huanza siku 3 – 7 baada ya kuumwa na mbu mwenye maambukizi
 • Dalili zinazowapata watu wengi ni homa na maumivu ya viungo
 • Dalili nyingine ni pamoja na kuumwa kichwa, maumivu ya misuli, kuvimba viungo, au upele
 • Ugonjwa wa chikungunya kwa kawaida hausababishi kifo, lakini dalili zinaweza kuwa kali na kusababisha shida kubwa
 • Wagonjwa wengi huanza kujisikia vizuri ndani ya wiki moja. Kwa baadhi ya watu dalili zinaweza kuendelea kwa miezi kadhaa.

Ni nini sababu za ugonjwa wa chikungunya?Ugonjwa wa chikungunya

 • Virusi vya chikungunya vinaambukizwa kwa watu baada ya kuumwa na mbu mwenye maambukizi
 • Mbu wanapata maambukizi baada ya kumuuma/ kumng’ata mtu mwenye maambukizi
 • Mbu walioambukizwa wanaweza kusambaza virusi wa chikungunya wanapowang’ata watu
 • Virusi wa chikungunya wanasambazwa zaidi na mbu aina ya Aedes aegypti na Aedes albopictus
 • Hawa ni aina ya mbu wale wale wanaohusika na kueneza ugonjwa wa dengue
 • Mbu hawa wanauma zaidi wakati wa mchana

Ni nani yuko kwenye hatari zaidi

 • Watu walio kwenye hatari ya zaidi ya kupata ugonjwa mkali ni pamoja na watoto wachanga wanaoambukizwa mara tu baada ya kuzaliwa, wazee (wenye umri zaidi ya miaka 65), na watu wenye magonjwa sugu kama vile ugonjwa wa kisukari, shinikizo kubwa la damu, au ugonjwa wa moyo
 • Wasafiri wanaotembelea nchi zifuatazo za visiwa vya Karibea wako kwenye hatari pia ya kuambukizwa ugonjwa wa chikungunya
  • Anguilla
  • Antigua
  • British Virgin Islands
  • Dominica
  • Dominican Republic
  • French Guiana
  • Guadeloupe
  • Guyana
  • Haiti
  • Martinique
  • Puerto Rico
  • Saint Barthelemy
  • Saint Kitts
  • Saint Lucia
  • Saint Martin (French)
  • Saint Vincent and the Grenadines
  • Sint Maarten (Dutch)
 • Watu wanaosafiri pia kuja nchi za Afrika, Asia, na visiwa vilivyoko katika bahari ya hindi na mashariki mwa pasifiki wako kwenye hatari pia, kwa sababu virusi wanapatikana kwenye mengi ya maeneo yao.
 • Mbu wanaobeba na kueneza virusi wa chikungunya wanauma watu mchana na usiku, ndani nan je ya nyumba, na mara nyingi wanaishi karibu na makazi ya watu mijini.

Utambuzi

 • Dalili za ugonjwa wa chikungunya zinafanana sana na ugonjwa wa dengue, huu ni ugonjwa mwingine unaoenezwa na mbu.
 • Kama umesafiri hivi karibuni kwenda chenye eneo lenye hatari, mwambie daktari
 • Daktari ataagiza vipimo vya damu ili kutafuta ugonjwa wa chikungunya au magonjwa mengine yanayofanana nao.

Wkati gani uombe msaada wa kitabibu haraka?

Onana na daktari kama umepata dalili zifuatazo:

Uchaguzi wa matibabu

 • Hakuna dawa ya kutibu maambukizi au ugonjwa wa chikungunya
 • Madaktari hujaribu kudhibiti na kupunguza dalili za ugonjwa mpaka utakapopona mwenyewe kwa:
  • Kupumzika vizuri
  • Kunywa maji ya kutosha ili kuzuia kuishiwa maji mwilini
  • Tumia dawa. Kama vile ibuprofen, naproxen, acetaminophen, au paracetamol ili kupunguza homa na maumivu

Kuzuia ugonjwa wa chikungunya

 • Hakuna chanjo ya kuzuia maambukizi au ugonjwa wa chikungunya
 • Kuepuka kuumwa na mbu ndio njia bora zaidi ya kujikinga na maambukizi ya chikungunya
 • Mbu wanaoeneza ugonjwa wa chikungunya wanauma watu zaidi wakati wa mchana
 • Njia bora zaidi za kujikinga na ugonjwa huu ni zile zinazopunguza uwezekano wa kukutana na ugonjwa – hasa mbu wenye maambukizi. Hizi ni pamoja na kutumia dawa za kufukuza mbu zenye DEET au permethrin, kuvaa nguo za mikono mrefu na suruali ili kujifunika vizuri, kuweka milango na wavu kwenye madirisha ya nyumba. Ni muhimu pia kuondoa maji yaliyotwana ili kuzuia mazalia ya mbu.

Namna ya kujikinga mwenyewe na mbumbu waenezae chikungunya

 • Weka wavu kwenye madirisha au milango ili kuhakikisha mbu hawaingii ndani ya nyumba
 • Kama hauwezi kujikinga binafsi na mbu ukiwa ndani ya nyumba, lala chini ya neti iliyotiwa dawa
 • Saidia kuondoa mazalia ya mbu nje ya nyumba kwa kufunika madimbwi yenye maji na kumwanga maji yaliyomo kwenye makopo, vyungu vya maua au ndoo.
 • Kama hali ya hewa inaruhusu, vaa nguo zenye mikono mirefu na suruali
 • Tumia dawa za kufukuza mbu, dawa za kufukua mbu zina DEET, picaridin, IR3535, nan a mafuta ya lemon eucalyptus na para-methane-diol products provide long lasting protection.
  • Usipulizie dawa za kufukuza mbu kwenye ngozi inayofunikwa na nguo zako
  • Unaweza kuchovya nguo zako kwenye permethrin au nunua nguo zilizotiwa dawa ya kuua mbu kabisa
  • Hakikisha unafuata maelekezo muda wote unapotumia dawa za kufukuza mbu

Matarajio

 • Mara nyingi dalili za mtu aliyeambukizwa huwa za kawaida na maambukizi yanaweza yasitambuliwe, au mtu anaweza kuambiwa ni ugonjwa wa dengue wakati ana ugonjwa wa chikungunya, hasa maeneo ambayo ugonjwa wa dengue unapatikana
 • Wagonjwa wengi wenye ugonjwa wa chikungunya wanapona kabisa, lakini maumivu ya viungo yanaweza kuendelea kuwepo kwa miezi kadhaa, au hata miaka.
 • Baada ya mtu kuugua, anajenga kinga kiasi kwa ugonjwa huu – inakuwa ngumu kidogo kuambukizwa tena

Matatizo yanayoweza kutokea ukiwa na ugonjwa wa chikungunya

 • Kumekuwepo na matukio au visa vya matatizo ya macho, mfumo wa fahamu, moyo na matatizo ya mfumo wa chakula. Matatizo makubwa sio ya kawaida, lakini kwa wazee, ugonjwa huu unaweza kuchangia kusababisha kifo.

Vyanzo

https://medlineplus.gov/ency/patientinstructions/000821.htm

Leave feedback about this

 • Quality
 • Price
 • Service

PROS

+
Add Field

CONS

+
Add Field
Choose Image
Choose Video
X