UGONJWA WA HIMOFILIA (HEMOPHILIA):Sababu,dalili,matibabu

Maelezo ya jumla

Ugonjwa wa himofilia (hemophilia) ni kundi la matatizo ya damu yanayosababisha damu kuchukua muda mrefu sana kuganda kuliko ilivyo kawaida.

Ni zipi dalili za ugonjwa wa himofilia (hemophilia)?Himofilia

  • Dalili kuu ya ugonjwa wa himofilia (hemophilia) ni kuvuja damu. Baadhi ya visa vya ugonjwa wa himofilia visivyo na dalili kali vinaweza visitambuliwe mpaka mgonjwa amekuwa mtu mzima, vinaweza kutambuliwa wakati anafanyiwa upasuaji au baada ya kupata jeraha.
  • Kwa visa vya ugonjwa wa himofilia (hemophilia) vyenye dalili kali, mgonjwa anaweza kuvuja damu nyingi sana bila sababu yoyote. Mgonjwa anaweza kuvuja damu ndani kwa ndani sehemu yoyote. Kuvuja kwa damu kwenye viungo vya mwili ni jambo la kawaida.

Ni nini husababisha ugonjwa wa himofilia (hemophilia)?

  • Mtu anapoanza kuvuja/kutokwa damu, mwili unaruhusu mchakato wa mfululizo wa matukio kadhaa ili kusababisha damu kuganda na kuziba panapovuja damu isiendelee kutoka. Mchakato huu unaijulikana kama mchkato wa kuganda kwa damu. Mchakato huu unahusisha aina kadhaa maalumu za protini ambazo husaidia damu kuganda. Inapotokea kuwa, mtu amezaliwa na upungufu wa moja au zaidi yap rotini hizi maalumu, huongeza uwezekano wa kuendelea kuvuja damu.
  • Ugonjwa wa himofilia (hemophilia) unatokana na mtu kukosa au kuwa na upungufu wa Factor VII au IX. Kwa visa vingi, ugonjwa wa himofilia (hemophilia) unarithiwa kati ya wanafamilia. Ni ugonjwa unaowapata zaidi wanaume.

Utambuzi wa ugonjwa wa himofiliaUgonjwa wa himofilia (hemophilia)

Kwa kawaida, ugonjwa himofilia unatambuliwa baada ya mtu kuvuja damu nyingi sana au kama mtu anayo historia ya kuwepo ugonjwa huu katika familia yake.

Uchaguzi wa matibabu ya ugonjwa wa himofilia

  • Utaratibu wa kawaida wa matibabu unahusisha kuongezewa viambata vya kusababisha kuganda kwa damu mtu anavyokosa kupitia kwenye mishipa.
  • Kutambuliwa kuwa una ugonjwa wa kuvuja damu nyingi ni muhimu sana ili kumsaidia daktari kupanga mpango mzuri wa matibabu hasa unapohitaji upasuaji, na unaweza kukupima na kuwataarifu wanafamlia wengine ambao wanaweza kuwa na ugonjwa huu pia.

Mtararajio

  • Watu wengi wenye ugonjwa wa himofilia (hemophilia) wanaweza kuishi maisha ya kawaida kabisa. Hata hivyo, baadhi ya wagonjwa wana matukio makubwa ya kuvuja damu sana, hasa kuvujia kwa damundani ya viungo vya mwili.
  • Asilimia chache za watu wenye ugonjwa wa himofilia (hemophilia) wanaweza kufa kutokana na kuvuja damu nyingi sana.

Vyanzo

https://medlineplus.gov/genetics/condition/hemophilia/

Leave a Reply

Your email address will not be published.

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.

Jiunge Nasi