UGONJWA WA HOMA YA INI A :Dalili, Matibabu…

Maelezo ya jumla

Ugonjwa wa homa ya ini A ni ugonjwa wa ini unaosababishwa na virusi wanaoitwa hepatitis A.

Dalili za ugonjwa wa homa ya ini A

Homa huanza ghafla, uchovu, kupoteza hamu ya chakula na kichefuchefu. Mkojo unaweza kuwa na rangi kama chai au soda ya cocacola, kinyesi chenye rangi iliyofifia, na manano kwenye macho au ngozi hutokea siku chache baadae. Watoto wengi wenye umri chini ya mika 6 haoneshi dalili zozote baada ya kuambukizwa. Mara nyingi watoto wakubwa na watu wazima wanapoambukizwa, hupata dalili, hii ni pamoja na manjano.

Jinsi ugonjwa unavyoambukizwa

Virusi wa hepatitis A wanasambazwa na kinyesi. Kama ukishika kinyesi au kitu kilichochafuliwa na kinyesi na kisha ukashika au kuweka vidole au kitu kilichochafuliwa mdomoni utaambukizwa virusi vya hepatitis A. Mammbukizi haya yanaweza kusambaa kama watu hawanawi mikono baada ya kutoka chooni na kisha kushika au kuandaa chakula.

Kumbuka kuwa mtu aliyeambukizwa asiyekuwa na dalili yoyote anaweza bado kukuambukiza ugonjwa huu.

Inachukua muda gani dalili  kuanza kuonekana

Inaweza kuchukua siku 15 mpaka 50, kwa kawaida siku 28, toka ulipoambukizwa mpaka unapoanza kuona dalili.

Wakati gani unaweza kuambukiza wengine ugonjwa wa homa ya ini A

Unaweza kuambukiza wengine ugonjwa huu kuanzia wiki ya 2 kabla ya dalili kuanza mpaka wiki mbili baada ya dalili kuanza. Hatari ya kuambukiza wengine inapungua sana baada ya manjano kuanza.

Utambuzi wa  ugonjwa wa homa ya ini A

Utafanyiwa kipimo cha damu (Hepatitis A IgM antibody test)  ili kuangalia kama umepatwa na maambukizi hivu karibuni.

Matibabu ugonjwa wa homa ya in A

Hakuna matibabu maalum ya kutibu ugonjwa huu.

Kujikinga au kuzuia ugonjwa wa homa ya ini A

Chanjo ya hepatitis A inapendekezwa kwa watoto wa miezi 12 mpaka 23 na inashauriwa kwa watu walio kwenye hatari zaidi ya kuambukizwa. Watu wanaosafiri kwenda maeneo yenye maambukizi kwa wingi, wanaume wanaoshiriki ngono na wanaume wenzao, watumiaji wa madawa ya kulevya na watu wanaofanya kazi zinazowaweka kwenye hatari ya kuambukizwa. Chanjo inashauriwa pia kwa watu wenye ugonjwa wa ini kwa sababu wako kwenye hatari ya kupata ugonjwa mkali zaidi.

  • Nawa mikono vizuri baada ya kutoka chooni na kabla ya kula au kuandaa chakula
  • Safisha kwa uangalifu vyoo na maeneo yanayozunguka vyoo kwa angalau mara 1 kwa siku

Angalia pia:

Vyanzo

https://medlineplus.gov/spanish/hepatitisa.html

Leave a Reply

Your email address will not be published.

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.

Jiunge Nasi