UGONJWA WA HOMA YA INI B :Dalili, Sababu..

Maelezo ya jumla

Ugonjwa wa homa ya ini B ni ugonjwa unaosababishwa na virusi vya hepatitis B. Sio rahisi kwa watoto kuambukizwa ugonjwa huu wa homa ya ini B, isipokuwa watoto walioambukizwa wakati wa ujauzito au wakati wa kuzaliwa. Watoto walioambukizwa wanaweza kubakia na maambukizi ya ugonjwa huu maisha yao yote.

Nini dalili za ugonjwa wa homa ya ini B

Zifuatazo ni dalili za homa ya ini B

 • Kupoteza hamu ya kula
 • Uchovu
 • Maumivu ya tumbo
 • Kichefuchefu
 • Kupata mkojo wenye rangi nyeusi kama coca-cola
 • Kupata kinyesi chenye rangi iliyofifia
 • Na wakati mwingine kuwa na upele na maumivu ya viungo.
 • Manjano kwenye macho au ngozi inaweza kutokea kwa watu wazima japo ni nadra kwa watoto.

Dalili zinatofautiana sana kati ya mgonjwa mmoja na mwingine, mmoja anaweza asipate kabisa dalili, ila mwingine akapata ugonjwa mkali sana.

Namna maambukizi yanavyosambaa

Virusi wa hepatis B wanapatikana kwenye damu na vimiminika vingine vya mwili vinavyoweza kuwa na damu. Ugonjwa huu unaweza kuambaa kama damu iliyoathirika itaingia mwilini kupitia jeraha, kurukiwa na damu kwenye macho au mdomoni au kwa kuchangia vitu vyenye ncha kali:

 • Wakati wakujidunga madawa
 • Kuchora tattoo
 • Kutoboa matundu kwa ajili vipini au hereni
 • Kupitia kujamiiana

Japo virusi hawa wanapatikana kwenye mate, sio rahisi kuambukizwa kwa kupitia mate.  Kiasi cha virusi kilichopo kwenye mate ni kidogo sana. Maambukizi yanaweza pia kusambaa kutoka kwa mama kwenda mtoto wakati wa ujauzito au kujifungua.

Muda kabla ya dalili kuanza

Inaweza kuchukua wiki 6 mpaka miezi 6, kwa kawaida huchukua miezi 2 mpaka 3, tangu ulipoambukizwa virusi vya hepatitis B mpaka kuanza kuona dalili.

Muda ambao unaweza kumbukiza wengine ugonjwa wa homa ya ini B

Unaweza kuwaambukiza wengine ugonjwa huu wiki nyingi kabla ya dalili kuanza. Utaendelea kuwa na uwezo wa kuwaambukiza wengine kwa miezi 4 mpaka 6 baada ya dalili kuanza. Baaadhi ya watu wanaweza kuwa na ugonjwa sugu wa homa ya ini B. Wagonjwa wenye ugonjwa sugu wanaweza kuwaambukiza wengine maisha yao yote.

Utambuzi wa ugonjwa wa homa ya ini B

Ugonjwa huu unaweza kutambuliwa baada ya kufanya vipimo vya damu

Matibabu ya ugonjwa wa homa ya ini B

Matibabu yapo kwa ajili ya ugonjwa huu. Ni vizuri kumwona daktari akakushauri zaidi nini cha kufanya. Anaweza kukuandikia dawa kama vile Tenofovir, Entecavir au lamivudine utakazohitajika kutumia maisha yako yote.

Kujikinga au kuzuia ugonjwa wa homa ya ini B

Njia zifuatazo zinaweza kutumika kujkinga au kuzuia kuambukizwa ugonjwa wa homa ya ini B

 • Watoto wote wanapaswa kupewa chanjo zote 3 za ugonjwa huu wa homa ya ini B kama ilivyo elekezwa kwenye mpango wa taifa wa chanjo.
 • Chanjo ya homa ya ini B inashauriwa pia kwa vijana walio kwenye balehe na watu wazima ambao hawajawahi kupata chanjo na wako kwenye hatari zaidi ya kuambukizwa.
 • Kama mtu amerukiwa na damua au majimaji yoyote ya mwili kutoka kwa mtu aliyeambukizwa, anapaswa kumwona daktari haraka kuangalia kama kuna uwezekano wa kupewa chanjo. Anaweza pia kuongezewa majimaji yenye kinga dhidi ya maambukizi ya homa ya ini B (Hepatitis B immune globulin (HBIG))
 • Safisha na takasa maeneo yote yaliyodondokewa na dama au majimaji ya mwili
 • Safisha kwa sabuni na dawa za kusafishia haraka iwezekanavyo maeneo na vyombo vyote vilivyo chafuliwa kwa damu au majimaji ya mwili. Virusi wa hepatitis B wanaweza kupatikana kwenye damu ya mtu yoyote hata kama hajaanza kuonesha dalili.
 • Vaa mipira ya kujikinga (gloves) unapokuwa ukitoa huduma ya kwanza (kuvuja damu puani, kujikata). Vaa gloves pia unaposhika vitu, maeneo au nguo zilizochafuliwa na damu au majimaji ya mwili, hasa yenye damu: vidonda, mikato, mikwaruzo n.k.
 • Nawa mikono mara kwa mara. Ni njia bora ya kupunguza kusambaa kwa magonjwa ya kuambukizwa. Nawa mikono kwa sabuni na maji yanayotiririka.
 • Usichangie vifaa kama vile miswaki, vikata kucha au nyembe.
 • Tumia kondomu unapojamiiana

Angalia pia:

Vyanzo

https://medlineplus.gov/ency/article/000279.htm

Leave a Reply

Your email address will not be published.

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.

Jiunge Nasi