UGONJWA WA HOMA YA INI C : Dalili, Matibabu…

Maelezo ya jumla

Sio rahisi kwa watoto kuambukizwa ugonjwa wa homa ya ini C, isipokuwa wanaoambukizwa wakati wa kuzaliwa. Watu wengi wanaoambukizwa ugonjwa wa homa ya ini C hubakia na maambukizi maisha yao yote (ugonjwa sugu).

Nini sababu ya ugonjwa wa homa ya ini C

Virusi wa hepatitis C

Nini dalili za ugonjwa wa homa ya ini C

Watoto wadogo na watu wazima wengi wanaoambukizwa ugonjwa wa homa ya ini C wanaweza wasiwe na dalili zozote. Ni 20% tu ya watu wazima huonesha dalili baada tu ya kuambukizwa. Dalili hizi ni pamoja na:

Watu wazima wanaweza wasiwe na dalili zozote kwa muda wa miaka 10 mpaka 30 ya ugonjwa sugu wa homa ya ini C.

Maambukizi ya virusi vya hepatitis C yanasambaaje?

Maambukizi yanasambaa kupitia damu na majimaji ya mwili. Unaweza kuambukizwa kama damu ya mtu aliyeambukizwa itangia mwilini kupitia kidonda au kwa kuchangia vitu vyenye ncha kali wakati wa:

 • Kujidunga madawa
 • Kutoboa ngozi kwa ajili ya tattoo, kuweka kipini au hereni n.k

Japo uwezekano ni mdogo, unaweza kuambukizwa kwa kujamiiana na mtu mwenye maambukizi. Ugonjwa wa homa ya ini C hauambukizwi kwa busu au kwa kugusana. Hatari ya mama kumwambukiza mwanae ni ndogo, ila inawezekana.

Ni muda gani unapita kabla dalili kuonekana

Inaweza kuchukua muda wa wiki 2 mpaka miezi 6, kwa kawaida inachukua wiki 6 mpaka 7  tangu kuambukizwa virusi vya hepatitis C mpaka dalili kuanza kuonekana.

Ni kipindi gani nitaweza kuambukiza wengine

Kipindi chote utakachokuwa na virusi vya hepatis C kwenye damu yako. Karibu 80% ya watu wenye ugonjwa homa ya ini C hubakia na maambukizi maisha yao yote. Wanapatwa na ugonjwa sugu.

Utambuzi wa ugonjwa wa homa ya ini C

Ugonjwa wa homa ya ini C unaweza kutambuliwa baada ya kufanya vipimo vya damu. Kama umekutana na damua au majimaji ya mtu aliyeambukizwa, mwone daktari ili ufanyiwe uchunguzi na vipimo vya damu haraka.

Matibabu ya ugonjwa wa ini C

Hakuna chanjo ya ugonjwa wa homa ya in C. Watu wote wenye maambukizi ya virusi vya hepatitis C wanapaswa kupata chanjo ya homa ya ini A, na watoto wanapaswa kupata chanjo ya homa ya in B.

Kama umegundulika kuwa na maambukizi ya ugonjwa homa ya ini C, daktari anaweza kupendekeza utumie dawa kama Ledpasvir + Sufosbuvir + Ribavirin kwa wiki 12 mpaka 24.

Matatizo yanayotokana na ugonjwa wa ini C

Maambukizi ya homa ya ini C yanayokuwepo kwa muda mrefu huanza kusababisha matatizo kama yafuatayo:

 • Kutengeneza makovu kwenye ini (liver cirrhosis) – kwa sababu ya maambukizi na uvimbe wa muda mrefu unaosababishwa na maambukizi ya virusi vya hepatitis C. Kwa sababu ya makovu haya, inaweza kuwa ngumu kwa ini kufanya kazi yake.
 • Saratani ya ini – Baadhi ya watu wachache wenye maambukizi ya ugonjwa wa ini C hupatwa na kansa ya ini.
 • Kushindwa kwa ini kufanya kazi –kwa sababu ya uharibifu mkubwa na makovu yaliyosababishwa na virusi wa hepatitis C ini hushindwa kwabisa kufanya kazi.

Kujikinga au kuzuia maambukizi

Jikinge na maambukizi ya virusi wa hepatis C kwa kuchukua tahadhariz ifuatazo:

 • Safisha na takasa maeneo yote yaliyodondokewa na dama au majimaji ya mwili
  • Safisha kwa sabuni na dawa za kusafishia haraka iwezekanavyo maeneo na vyombo vyote vilivyo chafuliwa kwa damu au majimaji ya mwili. Virusi wa hepatitis B wanaweza kupatikana kwenye damu ya mtu yoyote hata kama hajaanza kuonesha dalili.
  • Vaa mipira ya kujikinga (glavu) unapokuwa ukitoa huduma ya kwanza (kuvuja damu puani, kujikata). Vaa glavupia unaposhika vitu, maeneo au nguo zilizochafuliwa na damu au majimaji ya mwili, hasa yenye damu: vidonda, mikato, mikwaruzo n.k.
  • Nawa mikono mara kwa mara. Ni njia bora ya kupunguza kusambaa kwa magonjwa ya kuambukizwa. Nawa mikono kwa sabuni na maji yanayotiririka.
 • Usichangie vifaa kama vile miswaki, vikata kucha, nyembe, au vifaa vya kutoboa ngozi.
 • Japo uwezekano wa kuambukizwa virusi vya hepatitis C kupitia ngono ni mdogo, mambo yafutayo yanaongeza hatari ya kuambukizwa kama usipotumia kondomu:

Angalia pia:

Vyanzo

https://medlineplus.gov/hepatitisc.html[/vc_column_text][/vc_column][/vc_row]

Leave a Reply

Your email address will not be published.

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.

Jiunge Nasi