Magonjwa ya ndani ya mwili

UGONJWA WA JONGO/GAUTI: dalili,sababu,matibabu

Last Updated on October 13, 2023 by Dr Mniko

Ugonjwa wa jongo (gout) ni nini?

Ugonjwa wa jongo ni ugonjwa unaotokana na kuwa na kiasi kikubwa cha uric acid mwilini. Uric acid inaweza kurundikana mwilini na kutengeneza mawemawe. Mawemawe haya yanaweza kusababisha mawe kwenye figo, maumivu kwenye maungio/viungo yanayotokana na kuvimba kwa viungo au mawemawe haya yanaweza kurundikana chini ya Ngozi (tophi).

ugonjwa wa jongo

Nani anaweza kupatwa na ugonjwa wa jongo (gout)?

Wanaume wenye umri zaidi ya miaka 30 wana uwezekano mkubwa wa kupata jongo. Wanawake wanaweza kupata ugonjwa wa jongo, ila ni mpaka baada ya damu ya hedhi kukoma (menopause).

Una uwezekano mkubwa zaidi wa kupata ugonjwa wa jongo kama una uzito mkubwa sana wa mwili, unakunywa pombe au kama unatumia dawa za kupunguza shinikizo la damu zinazosababisha ukojoe sana (diuretics). Pia, una uwezekano mkubwa kupata jongo kama unatumia madawa fulani baada ya kupandikiziwa kiungo kutoka kwa mtu mwingine (transplant).

Shambulio la jongo (gout) ni nini?

Shambulio la ugonjwa wa jongo ni unapopata maumivu ya ghafla, wekundu na kuvimba kwa kiungo. Mara nyingi inatokea kwenye wayo wa kidole gumba cha mguu, lakini linaweza kutokea kwenye viungo vingine pia. Maumivu ni makali kiasi kwamba, hata kupagusa na nguo tu hakuvumiliki.

Daktari atatambuaje kama nina ugonjwa wa jongo?

Daktari akikuona, anaweza kuhisi kuwa una ugonjwa wa jongo kutokana na dalili zako. Daktari anaweza kufanyia vipimo damu na kufanyia uchunguzi majimaji kutoka kwenye maungio yenye ugonjwa ili kuhakikisha.

Ugonjwa wa jongo (gout) unatibiwaje?

Dawa zinaweza kupunguza maumivu na harara ya maungio wakati wa shambulio la jongo. Kama ukiendelea kuwa na mashambulio ya ugonjwa wa jongo, daktari anaweza kukupatia dawa za kupunguza kiwango cha uric acid mwilini. Unapaswa kuendelea kutumia dawa hizi hata kama utapata shambulio jingine.

Kudhibiti uzito wa mwili unapunguza uwezekano wa kupata mashambulio mara kwa mara. Kama daktari atakuruhusu, tembea kwa dakika 20 kila siku kama mazoezi. Usinye pombe (hasa bia) au kula nyama nyekundu kwa wingi au Samaki / mazao ya baharini.

Vyanzo

https://medlineplus.gov/gout.html

Leave feedback about this

  • Quality
  • Price
  • Service

PROS

+
Add Field

CONS

+
Add Field
Choose Image
Choose Video
X